MFUKO WA PENSHENI WA LAPF WAFIKIA HADI BILIONI 830.
Meneja
wa Takwimu,Tathmini na Hadhari toka Mfuko wa Pensheni wa LAPF
bw.Aboubakar Ndwata akiwaeleza waandishi wa habari leo Jijini Dar es
salaam kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali unaofanywa na mfuko huo
ukiwemo wa jengo linalokadiriwa kuwa refu zaidi jijini Dar es salaam
lenye urefu wa gorofa 30 ambalo limejengwa kijitonyama jijini Dar es
salaam likiwa na thamani ya Shilingi bilioni 58, kulia ni Meneja Masoko
na Mawasiliano wa Mfuko huo Bw.James Mlowe na kushoto ni meneja
Matekelezo Bw. Victor Kikoti.

Mfuko wa Pensheni wa LAPF umekua na kuongezeka ambapo thamani
yake imefikia Sh. bilioni 830 hivyo kuwa ni mfuko unaokua kwa kasi zaidi
hapa nchini.
Hayo yamesemwa jana jijini Dar es salaam na Meneja wa Takwimu,Tathmini na Hadahari toka LAPF bw. Aboubakar Ndwata wakati wa Ziara ya waandishi wa habari katika moja ya miradi inayotekelezwa na mfuko huo katika eneo la kijitonyama Jijini Dar es salaam.
Akifafanua kuhusu mafanikio ya Mfuko huo Ndwata amesema moja ya miradi inayotekelezwa ni ujenzi wa jengo la kisasa katika jiji la Mwanza wenye thamani ya bilioni 60 ambao utaongeza na kukuza shughuli za kiuchumi katika jiji hilo.
“Mradi wa eneo la mabasi wa msamvu Mkoani Morogoro ambao unakadiriwa kutumia Sh. bilioni 35 ambapo michoro imeshakamilika na shughuli za kutangaza zabuni zinaendelea” alisema Ndwata.
Katika mradi wa ujenzi wa Mabweni Katika chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Ndwata amesema awamu ya kwanza ya mradi huo iliyogharimu bilioni 39 imekamilika na awamu ya pili michoro yake imekamilika na inakadiriwa kutumia Sh. bilioni 15.
Pia LAPF imetekeleza mradi wa ujenzi wa Shule ya Afya katika chuo Kikuu Dodoma ambapo mradi huo ulikamilika Agosti 2010 ukiwa na thamani ya Sh. bilioni 22.
Mfuko huo pia unajenga Jengo la Kisasa kwa ajili ya ofisi ya Dodoma lenye thamani ya Sh. Bilioni 47 ambapo mradi huo ulianza mwaka 2012 na unatarajiwa kukamilika mwaka huu.
Katika hatua nyingine Ndwata alisema Makao makuu ya Mfuko huo yako Dodoma na ofisi za Kanda ya kati zinajumuisha Mikoa ya Dodoma, Singida,Tabora, Kigoma na Kanda ya Mashariki inayojumuisha Mikoa ya Dar es salaam, Mtwara, Lindi, Morogoro na Pwani.
Kwa Upande wa Kanda ya Kaskazini Ndatwa alisema kuwa inajumuisha Mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjarao,Tanga na Kanda ya Ziwa Mwanza, Kagera, Mara, Geita, na Shinyanga.
Naye Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko huo Bw. James Mlowe alisema mfuko huo umekuwa ukitoa fao la elimu kwa njia ya mkopo kwa wanachama wake ambao umeanza rasmi agosti mwaka 2014.
Aidha, Mlowe ameongeza kuwa LAPF inaendelea kutoa mafao bora kwa wanachama wake tangu kuanzishwa kwake hadi sasa.
Mfuko wa pensheni wa LAPF unaendeshwa chini ya Sheria ya LAPF ( The Local Authorities Pensions Fund Act No 9 of 2006) ambapo sheria hii imefanyiwa marekebisho kukidhi mahitaji ya sheria ya usimamizi wa Hifadhi ya Jamii ya Mwaka 2008 (SSRA).

0 comments:
Post a Comment