Followers

VIDEO: B.O.B N' MICHARAZO - KAZI KWANZA

Hatari nyingine town kutoka kwa B.O.B MICHARAZO 'kazi kwanza'

.

TZEE MODAL APATA DILI SOUTH AFRICA

Calisah amepata shavu kutoka kampuni moja ijulikanayo kama Ice Model ambayo inadeal modelling...

VIDEO: NEY WA MITEGO - SINA MUDA

Audio from Free Nation / Mr. T - Touch, Video Production : Joowzey

VIDEO: MESEN SELEKTA - SWEET LOVE

Music video by Mesen Selekta performing 'Sweet love'. Video directed by Ivan (Shine Studioz).

VIDEO: RABIT KING KAKA FT RICH MAVOKO - NJOO

Video mpya kutoka kwa Rabbit King Kaka featuring Rich Mavoko. iitwayo 'Njoo'.

Showing posts with label BURUDANI. Show all posts
Showing posts with label BURUDANI. Show all posts

Sunday, 31 May 2015

MIAKA 16 YA NATURE NI SHIIDAAH, TAZAMA PICHA ZOTE ZA TUKIO HILO HAPA


Jana ilikuwa ni siku maalumu kwa msanii mkongwe Juma Kassim Nature aka Kibra alikuwa anatimiza miaka 16 kwenye mziki wa Bongo fleva, E fm na Nature wakamua kufanya bonge la Show kwenye ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala huku akisindikizwa na wasanii kadhaa

Wednesday, 15 April 2015

SHAMSA AFUNGUKA UKWELI KUMUHUSU NAY SOMA HAPA

Bongo Movies star Shamsa Ford aliye hit sana katika film ya chausiku na kujizolea umaarufu
Shamsa pia ambae siku za hivi karibuni alikanusha waziwazi alipokuwa akihojiwa na vyombo mablimbali vya habari juu ya kuwa na mahusiano ya kimapenzi wa Staa Nay wa Mitego hatimaye jana kupitia ukurasa wake mtandaoni alibandikaa picha yake pamoja na ya Nay na kuandika maneno ya kimahada yaliyosomeka

Monday, 13 April 2015

HILI NDIO JINA JIPYA ALILOLITOA DIVA

Diva sio Loveness tena kuanzia sasa! Mtangazaji huyo wa Clouds FM amebadilisha jina lake mahakamani na kuwa ‘Diva Gissele D. Malinzi’
Diva ameaimbia Bongo5 kuwa kuanzia Jumatatu ijayo atabadilisha kila kitu kilichokuwa na jina lake la zamani ‘Loveness’ baada ya kula kiapo mahakamani cha kubadilisha jina.Kwenye kiapo hicho, Diva amedai ameamua kubadilisha jina hilo kwa sababu za kikazi kwakuwa amekuwa akitumia jina ‘Diva’ kwa kipindi kirefu sasa.

ALICHO KISEMA RIYAMA KUHUSU TATIZO LA WEMA SEPETU

Baada ya hapo jana Staa mrembo wa Bongo Movies, Wema Sepetu kueleza kuwa anatamani sana kupata mtoto lakini hana uwezo huo,Staa mwenzake ambae ni mama wa mtoto mmoja, Riyama Ally ampa neno hili la faraja na matumani.
“Naomba hapa unisikie kwamakini nabii ibrahim alimpata na bii ismail akiwa na umri mkubwa sana utuuzimani wema bado mdogo muda utafika inshallah mola atakupa mume mwenye kheri na wewe uzae jike na dume usiumie mama mungu hukupa akujaalialo na sio umuombalo watoto ni kudra za mola na sio jitihada za wana dama atakupa maa muda ikifika

Tuesday, 20 January 2015

H.BABA NA MKEWE FLORA WATEGEMEA KUPATA MTOTO MWINGINE

H.Baba akiwa na mke wake Frora MvungiAkizungumza na 255 ya XXL , H. Baba amesema miongoni mwa mafanikio aliyopata mwaka jana ni pamoja na kumpa ujauzito mwingine mke wake,              "Faida ya mwaka jana ni mwana mama Flora Mvungi kujaa tena,” alisema. “Nikwambie kitu kimoja mimba huwa haipigiwi kelele, wala mimba sio kwenye magazeti. Mimi mimba huwa inaonekana,

Tuesday, 13 January 2015

ALICHO KISEMA JOKATE KUHUSU KUTOKA KIMAPENZI NA MILLARD AYO


 

Mwanamitindo na mwigizaji, Jokate Mwegelo ameucho molea vilivyo uvumi uliozagaa kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mtangazaji Millard Ayo wa Clouds FM.
Uvumi huo ulianzia mitandaoni ambapo mwanahabari wetu alipomtafuta Jokate juzikati, aliweka plain ukaribu wake na Millard ambaye ni mtangazaji mwenye mvuto mkubwa kwa jamii.

Thursday, 8 January 2015

Anti Lulu; NAWASIHI WASANII WENZANGU WAPIME ILI WAGUNDUE AFYA ZAO

  Ni siku chache zimepita tangu mwaka wa 2015 uanze, mwanadada mwenye umbo matata Bongo, Lulu Semagongo ‘Anti Lulu’ amekiri kuuanza vizuri baada ya kupima ngoma.Akipiga  stori na gazeti hili, Anti Lulu alisema anafurahi kwa kuwa ameuanza mwaka vizuri baada ya kwenda kupima Ukimwi akiongozana na mama yake na kujikuta yupo salama.

Saturday, 6 December 2014

DIAMOND AWASILI WASHINGTON DC KWA AJILI YA SHOO YA UHURU TAZAMA HAPA.

 Diamond akiwasili kwenye uwanja wa kimataifa wa Dulles muda huu tayari kwa makamuzi ya sharehe ya Uhuru itayofanyika muda si mrefu Sheraton, ya Downtown Silver Spring, Maryland.

 Diamond akimsalimia mwenyeji wake hayupo pichani mara tu alipowasili Dulles.

 Kushoto ni Dj Romy Jones, Diamond na mmoja wa waratibu wa sherehe ya Uhuru Bwn. Phanuel Ligate 

    Soma zaidi...

Thursday, 4 December 2014

HII SI YAKUKOSA NI USIKU WA WAFALME DAR LIVE CHRISTMAS HII

Monday, 27 October 2014

ORIJINO KOMEDI KUTUMBUIZA VILIVYO ARUSHA KATIKA TAMASHA LA TIGO WELCOME PACK

A

 Wasanii wa kikundi cha Ngoma cha Manyara Group  Mkoani Arusha kikiwapa burudani wakazi wa mkoa huo waliofurika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Adeid mwishoni mwa wiki kushuhudia tamasha la Tigo welcome pack, Kampuni ya Tigo imeanzisha kifurushi cha welcome pack kitakachomwezesha mtumiaji wa Tigo kupata muda wa maongezi wa dakika 20, MB175, SMS bila kikomo na pesa shilingi mia 500 kwenye akaunti yake ya Tigopesa, yote hayo kwa shilingi 1000 mteja atakaponunua laini yake ya Tigo.

B

Wasanii wa kikundi cha Original Komedi kikiwapa burudani wakazi wa mkoa wa Arusha waliofurika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Adeid mwishoni mwa wiki kushuhudia tamasha la Tigo welcome pack, Kampuni ya Tigo imeanzisha kifurushi cha welcome pack kitakachomwezesha mtumiaji wa Tigo kupata muda wa maongezi wa dakika 20, MB175, SMS bila kikomo na pesa shilingi mia 500 kwenye akaunti yake ya Tigopesa, yote hayo kwa shilingi 1000 mteja atakaponunua laini yake ya Tigo.

C

Msanii Ibrahim Mussa Maarufu Roma Mkatoliki akiwapa burudani wakazi wa mkoa wa Arusha waliofurika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Adeid mwishoni mwa wiki hii ni moja ya sehemu  burudani zitolewazo kwenye kampeni ya kifurushi kipya cha Tigo cha welcome pack. Kampuni ya Tigo imeanzisha kifurushi cha welcome pack kitakachomwezesha mtumiaji wa Tigo kupata muda wa maongezi wa dakika 20, MB175,SMS bila kikomo na pesa shilingi mia 500 kwenye akaunti yake ya Tigopesa, yote hayo kwa shilingi 1000 mteja atakaponunua laini yake ya Tigo.

D

Meneja wa mauzo wa Tigo Mkoani Arusha Bw. Aidan Komba akiongea na wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha kubwa la Tigo welcome pack uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha mwishoni mwa wiki.

DSC_1470

Msanii Joseph Haule maarufu kama Professor J akiwapa raha wakazi wa mkoa wa Arusha waliofurika kwa wingi kwenye tamasha la welcome pack uwanja wa Sheikh Amri Adeid mwishoni mwa wiki hii ni moja ya sehemu  burudani zitolewazo kwenye kampeni ya kifurushi kipya cha Tigo cha welcome pack.

DSC_1217

Mmoja kati ya watu waliojitokeza kwenye tamasha la welcome pack akipokea zawadi toka kwa mfanyakazi wa Tigo.

Sunday, 26 October 2014

MATUKIO YA PICHA SIKU YA MSANII MLIMANI CITY.

Mgeni rasmi katika Siku ya Msanii Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiongea jambo katika siku ya Msanii Mlimani city.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiongea jambo.

Wafanyakazi wa Global Publishers, Mhariri wa gazeti la Risasi Jumamosi, Eric Evarist (kushoto) akiwa na Andrew Carlos (katikati).(P.T)

Kikundi cha ngoma za kinyeji kikitoa burudanu usiku huu Siku ya Msanii Mlimani City.

LUNDENGA:"MISS TANZANIA HAJAJIUZULU"


HMB_3760


MKURUGENZI wa Kampuni ya Lino International Agency, Hashim Lundenga, amekanusha uvumi uliosambaa kwenye mitandao ya kijamii mapema leo, kuwa Sitti Abbas Mtemvu (pichani katikati) amelazimika kuvua taji la Uremo la Tanzania (Redd’s Miss Tanzania 2014).

Uvumi wa Sitti kuvua taji hilo umetokana na taarifa zilizotolewa kupitia akaunti ya Facebook mrembo huyo anayelalamikiwa kughushi vyeti vya kuzaliwa, akisema kutokana na vidole vya lawama anavyooshewa kiasi cha kuosa amani, amelazimika kuvua taji ili awe huru.

“Habari za jioni Watanzania wenzangu, kutokana na kuwa nimekuwa nikisemwa sana, maneno mengi yasio na tija juu ya hili taji la U-Miss anzania 2014,,mpaka kupelekea nisiwe na amani na uhuru ndani ya nchi yangu Tanzania, kwa roho safi nimeamua mwenyewe kujivua taji hilo na kuacha wanaye ona anastahili taji hili apewe ili niendelee na maisha yangu kwa amani ,isiwe shida sana kwani sitegemei taji hili ili kuishi!!” imeandikwa katika ukurasa huo.

misstz1

Akizungumzia uvumi huo, Lundenga alisema hakuna ukweli juu ya taarifa hiyo, na kwamba kama lingekuwa na ukweli ni wazi kwamba Sitti angeiarifu kampuni yake, inayoratibu kinyang’anyiro hicho kilichotimiza miaka 20 mwaka huu.

“Hakuna taarifa iliyotufikia hadi sasa kuhusiana na taarifa hizo. Sitti anajua anapaswa kufanya nini kama anaamua kulitema taji, ambapo anapaswa kutuarifu sisi kabla ya kuripoti hilo mahali popote. Kwa kuwa hajafanya hivyo, tunaamini hilo halipo nab ado tunamtambua kuwa mrembo wetu,” alisema Lundenga.

Kwa upande wa mama wa mrembo huyo, alisema ameshtushwa na taarifa za mwanaye kujiuzulu na kusema si za kweli, kwani kama angepanga kufanya hivyo asingefanya kwa kificho, badala yake angeitisha mkutao na wanahabari: “Hawezi kujiuzulu kienyeji hivyo na hata mimi mama yake sina taarifa hizo, hayo ni matumizi mabaya ya mitandao.”

Thursday, 23 October 2014

MAHOJIANO MAPYA YA T.I MAREKANI AONGEA MENGINE KUHUSU TANZANIA.


T.IClifford Joseph Harris, Jr. a.k.a T.I mkali kutoka Marekani aliyeangusha show ya nguvu katika jukwaa la Serengeti Fiesta 2014 siku ya Jumamosi Oktoba 18 mwaka huu katika viwanja vya Leaders Club Dar es Salaam, bado ameendelea kuyasimulia mazuri na makubwa ya kuvutia aliyojionea Tanzania.

Katika mahojiano aliyofanya jijini New York na kituo cha redio cha Power 105.1 kwenye kipindi cha Breakfast Club, T.I amesema tangu aanze kufanya muziki hajawahi kufanya show kwenye jukwaa lolote mbele ya mashabiki zaidi ya 50,000.

T.I amelinganisha idadi hiyo ya kutisha kuwa ni sawa na kufanya show katika uwanja wa mpira wa miguu na kuujaza kwa show moja, kitu ambacho sio rahisi kutokea.

Swali la kuhusu Ebola bado liliulizwa kwa T.I, ambaye amesema hakuwa anahofu chochote alipokuja Tanzania, zaidi zaidi alikuwa akifikiria kuhusu mpenzi wake.

“Afrika ni Kubwa ukilinganisha Nigeria ambayo kiukubwa ni kama Texas, idadi ya watu waliopo Nigeria inalingana nawatu waliopo Marekani. Sasa pata picha watu wote tuliopo Marekani tukusanyike Texas. Kama kuna waathirika wanne, idadi hiyo yote haiwezi kuathirika..”—T.I

Tuesday, 21 October 2014

SIASA ZA MISS TANZANIA

Siasa zisiingizwe Miss Tanzania

OKTOBA 11 mwaka huu zilifanyika fainali za Shindano la Urembo Tanzania ‘Miss Tanzania’ na kushirikisha warembo kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini.

Katika fainali hizo, mrembo Sitti Mtemvu alitangazwa kuwa ndiye Miss Tanzania 2014 na kukata tiketi ya kuipeperusha bendera ya Tanzania katika mashindano ya Dunia ‘Miss World’.

Lakini, tangu Sitti ambaye ni mtoto wa Mbunge wa Temeke jijini Dar es Salaam, Abbas Mtemvu atangazwe mshindi, wadau mbalimbali wa masuala ya urembo walianza kupinga ushindi wake wakidai kuna upendeleo.

Mengi yamesemwa kuhusiana na ushindi huo ikiwemo madai ya kuzidi umri uliopangwa kwa washiriki, ambao ni kuanzia miaka 18 na usizidi 24.

Katika kutetea hoja zao, wadau hao wameanika katika mitandao ya kijamii pasi yake ya kusafiria na leseni ya gari zikionyesha ana miaka 25.

Pia wanadai siku ya shindano mrembo huyo alikiuka maelekezo baada ya kuchagua lugha ya kiingereza katika kujibu swali lakini baadaye akatumia Kifaransa.

Jinsi malalamiko hayo yalivyozidi, Kamati ya Miss Tanzania imejitokeza kumtetea na kudai wao wanatambua kuwa ana miaka 23 na alishinda kwa vigezo stahiki.

Lakini kubwa lililotusukuma Tanzania Daima kuandika tahariri hii, jinsi baba mzazi wa Sitti, kulihusisha na masuala ya kisiasa.

Mtemvu akiwa katika majukumu yake ya kuwatumia wananchi wa jimbo lake mwishoni mwa wiki iliyopita, aliwatuhumu watu kadhaa kuwa ndio wanaoliratibu kwa maslahi ya kisiasa.

Mbunge alikaririwa kuwa, jambo hilo linaratibiwa mahasimu wake kisiasa ambao wana nia ya kugombea nafasi hiyo mwakani.

Sisi Tanzania Daima hatuungani na utetezi huu na kama hakuna ushahidi wa kumtetea Sitti, siasa zisitumike kama kichaka.

Mtemvu kama baba mzazi, tulitegemea aanike ukweli ikiwamo utata wa umri wa mwanaye na si kukimbilia kuwa ni masuala ya kisiasa.

Hoja zijibiwe kwa hoja na si vinginevyo. Familia ya Mtemvu na Kamati ya Miss Tanzania, wajipange kwa hoja na ushahidi wa uhakika ili kurejesha imani kwa jamii ambayo ina ukakasi na ushindi wa mrembo huyo na si kutumia siasa kichaka cha kuzima hoja za wanaodai kuna ulakini katika ushindi wa Sitti.

SOMA HII VITA YA UBUNGE NA MISS TANZANIA

Vita ya ubunge yaingia kashfa Miss Tanzania

Miss Tanzania 2014 na baba yake, Abbas MtemvuWAKATI mtoto wa mbunge wa Temeke, Sitti Mtemvu akiandamwa na kashfa ya kughushi umri baada ya kushinda Miss Tanzania 2014, baba mzazi wa mrembo huyo, Abbas Mtemvu, ameibuka na kudai sakata hilo ni vita ya kisiasa inayoratibiwa na wapinzani wake ndani ya CCM.

Tangu Sitti atangazwe mshindi Miss Tanzania katika shindano lililofanyika Oktoba 11 katika ukumbi wa Mlimani City, wadau mbalimbali wa urembo wamekuwa wakipinga ushindi wake wakidai hakustahili kutokana na kukosa sifa ikiwamo ya kutokuwa na umri stahiki.
Akizungumza mwishoni mwa wiki katika uzinduzi wa Vicoba kwenye klabu ya Jogging ya Temeke A jijini Dar es Salaam, Mtemvu alisema inasikitisha watu wanaolitaka jimbo hilo kumwandama kwa kashfa binti yake kwa maslahi yao binafsi ya kisiasa.
Mbunge huyo, alisema kama mtu anataka jimbo hilo aende kwa hoja na sio kwa majungu na kubainisha kwamba, yeye alichaguliwa na wana- Temeke, hivyo anayelitaka jimbo hilo aende kwa hoja kwa wananchi na si kupakana matope.
“Sikilizeni…hili jambo lisifanywe kisiasa, yule binti wanamdhalilisha sana, inasikitika mtu anaratibu majungu, tena ni matusi makubwa. Sitti wanamchafua tena wanamwambia kuwa binti niliyemzaa mimi eti mtoto wake, ambaye ni Tamia Abbas Mtemvu…haya ni matusi, kisa siasa,” alisema Mtemvu na kuongeza.
Wanapita wanasema Mtemvu kahonga milioni 62 za jimbo, jamani hivi fedha za mfuko wa jimbo zinatoka kwa namna hiyo, haya yote ni…MNEC (mjumbe wa NEC), kama utaka jimbo njoo kwa hoja si majungu na kuchafuana.
“Kwanza kwa taarifa yenu mimi sikuja hapa nikitokea mtaani, nilitoka kwenye kazi yangu, mimi nilikuwa DC (Mkuu wa Wilaya) tena faili langu hadi leo linaonyesha niko likizo…embu waambieni hao, kwanza nani kwaambia watu wa Temeke hatuna hela,” alisema Mtemvu huku akishangiliwa na baadhi ya wana kikundi hicho.
Licha ya kutomtaja mlengwa lakini wachambuzi wa siasa za Temeke walisema kuwa kauli hiyo ilielekezwa kwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Phares Magesa, ambaye inadaiwa kuwa ameonesha nia ya kugombea ubunge jimboni humo mwakani.
Magessa, kwa nyakati tofauti amekuwa akishiriki matukio mbalimbali ya kuimarisha chama hicho Wilaya ya Temeke, huku akitoa misaada mbalimbali kwa makundi ya kijamii ikiwamo vikundi vya Jogging na wasanii.
Misaada ya hivi karibuni ni pamoja na kuchangia mradi wa maji mtaa wa Tambukareli na Oktoba 24, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Jamvi la Katiba.
Alipotafutwa kuzungumzia tuhuma hizo, Magesa alisema hakuna ukweli wowote na kwamba hawezi kutumia u-NEC wake kumchafua kiongozi yeyote wa chama chake.
“Mimi kazi yangu ni kuhakikisha wabunge wangu yeye (Mtemvu) na Ndugulile wanatekeleza vema ilani ya chama chetu ili ukifika wakati wa uchaguzi tukainadi kwa wananchi, hivyo siwezi kumhujumu,” alisema.

Sitti Mtemvu "ndiye miss Tanzania halali"

 

 

Ushindi wa Bi Sitti Abbas Mtemvu katika kinyang'anyiro cha mashindano ya urembo ya Miss Tanzania ya mwaka 2014 umezua shutuma juu ya uhalali wa mrembo huyo kuvikwa taji hilo.

Siku chache baada ya kutangazwa kwake kuliibuka shutuma mbalimbali dhidi ya Bi Sitti na kumwondolea vigezo vya umalkia huo wa urembo.Tuhuma hizo zilianza kuzagaa katika mitandao ya habari ya kijamii zikiwemo shutuma za kufanyika udanganyifu wa umri.

Kamati ya kuandaa mashindano hayo, siku ya Jumanne imelitolea ufafanuzi suala hilo,mjini Dar es Salaam, ambapo mkurugenzi mtendaji wa kamati hiyo, Hashim Lundenga amesema, Sitti ndiye mshindi halali wa mashindano hayo ya mwaka 2014, na kwamba shutuma dhidi yake hazina msingi wowote zaidi ya kuwa uzushi: "Mimi nasema shutuma zote zilizotolewa hapa ni shutuma za uongo, kwa sababu kulingana na taratibu nilizozieleza hapo awali, sisi kama kamati kama waandaaji wa Miss Tanzania hatuna matatizo yoyote" anasema Bwana Lundenga.

Akizungumzia tuhuma kwamba Bi Sitti alidanganya umri kuwa ana miaka 18, mkurugenzi mtendaji wa kamati ya Miss Tanzania, Bwana Lundenga ameshangazwa na uzushi huo, akisema mrembo huyo hajawahi kutaja umri huo kama ndio umri wake. "hakuna mahala popote alipozungumza kuwa ana miaka 18...Kwa hiyo ni rumours ambazo zinaendelea tu na wameshindwa kuhakikisha"

Kwa ufafanuzi wa waandaaji wa mashindano hayo, Sitti Abbas Mtemvu ni mshindi halali wa Miss Tanzania 2014 na ndiye anayetarajiwa kuiwakilisha nchi katika mashindano makubwa ya mrembo wa dunia ya Miss World yatakayofanyika 2015.BBC

PICHA ZA MATUKIO MSIBA WA YP.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

PIGO:MSANII TMK WANAUME AFARIKI DUNIA

MSANII WA MUZIKI YP AFARIKI LEO. 

Msanii YP ambaye alitamba na kundi la muziki wa kizazi kipya TMK Wanaume Family amefariki dunia katika hospitali ya Temeke baada ya kusumbyuliwa na maradhi ya kifua. Kwa mujibu wa Said Fella ni kuwa taratibu za mazishi bado kujulikana mapaka sasa ila mpaka saa saba leo tayari ndugu zake watakuwa wameshapanga ratiba ya mazishi.

msanii YP

Thursday, 16 October 2014

Diamond"nipo tayari kumsaidia Alikiba"



 DIAMOND ASEMA YUPO TAYARI KUMPA COLLABO KIBA.

Msanii wa muziki wa bongo fleva nchini Nasib Abdul (Diamond) amesema yupo tayari kumsaidia collabo Alikiba ili aweze kuendelea kimziki.



Akiongea kupitia xxl ya clouds fm Diamond alijibu swali alilo ulizwa“je upo tayari kufanya collabo na kiba kutokana na tofauti zinazozungumzwa kati yenu?’’, “kama akija kuniomba nipo tayari kumsaidia kama nimeweza kufanya na wasanii wa nje itakuwaje nikatae kufanya na wasanii wetu wa nyumbani...nimeshasaidia wengi so akija yoyote nipo tayari kufanya naye’’.



Alisema Dimond na kuendelea“ kiukweli mi nashafika levo fulani hivyo ni kumtangaza mtukimataifa...’’



Diamond aliya jibu hayo ikiwa ni majibu kwa watanzania kuhusiana na kile kinachozungumzwa kuhusu hali ya sintofahamu kati yao.

Eeee;Bhana huyu ndiye mshindi wa Serengeti supa nyota diva 2014

HELLEN GEORGE AIBUKA MSHINDI WA SERENGETI SUPER NYOTA DIVA 2014

  • Posted by mbalamwezi forum 

Mshindi wa shindano la Serengeti Fiesta Super Nyota Diva 2014 Hellen George jijini Dar es Salaam, akionyesha makeke yake muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi wa shindano hilo.


Hellen George akifuta machozi muda mfupi baada ya kuibuka mshindi.


...Akiwa amejiinamia chini baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa Dar es Salaam 2014 katika shindano la Serengeti Super Nyota Diva ndani lililokuwa likifanyika mapema leo ndani ya Ukumbi wa Sun Cirro Sinza jijini Dar es Salaam.(P.T)

 

Mchujo wa kumpata mshindi wa Serengeti Fiesta Super Nyota Diva kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, umefanyika leo mchana ndani ya Ukumbi wa Suncirro Shekilango, ambapo tayari vijana mbalimbali wamejitokeza kuchuana na hatua ya kwanza tayari imemalizika kwa kupata washindi 5, ambao watachuana ili kuhakikisha anapatikana mshindi mmoja atakayeingia kwenye fainali za shindano hilo ambalo linatarajiwa kufanyika Ijumaa hii ndani ya Ukumbi wa Suncirro kwa kushirikisha wasanii wote waliopatikana kwenye jumla ya mikoa 14, ambayo imepitiwa na Tamasha la Serengeti Fiesta 2014.

Mmoja wa washiriki wa Serengeti Super Nyota Diva, akiwania nafasi ya kuwa Diva wa Jiji la Dar mapema leo ndani ya Ukumbi wa Suncirro.

Jaji wa mashindano hayo, Elias Barnabas akitafakari jambo wakati mchujo huo ukiendelea.

Mmoja wa washiriki akionyesha uwezo wake katika kuimba.

Majaji wa shindano hilo kutoka kulia ni mtayarishaji wa nyimbo, Tudi Thomas, DJ Fetty na Elias Barnabas wakiwajibika kuhakikisha wanampata mshindi bora wa shindano hilo.

Baadhi ya washiriki wakimshangilia mwenzao wakati akitafuta nafasi ya ushindi jukwaani hapo.

Mmoja wa washiriki hao akikamua kuwania nafasi hiyo.

Washiriki walioingia kwenye tano bora ya Shindano la Serengeti Super Nyota Diva 2014 jijini Dar es Salaam, wakiwa jukwaani.

Mshiriki akiwania nafasi ya kuwa Super Nyota Diva wa mkoa wa Dar es Salaam.

Majaji wa mchujo huo, Barnaba na DJ Fetty wakijadiliana jambo muda mfupi kabla ya kutaja washiriki walioingia kwenye tano bora.

Mrembo akiwajibika jukwaani kuwania nafasi ya kuwa Diva wa Dar.

Baadhi ya washiriki wakifuatilia shindano hilo.

Mshiriki akiwa stejini mbele huku baadhi ya washiriki wenzake wakimshuhudia wakati akiimba.