VIDEO: B.O.B N' MICHARAZO - KAZI KWANZA
Hatari nyingine town kutoka kwa B.O.B MICHARAZO 'kazi kwanza'
TZEE MODAL APATA DILI SOUTH AFRICA
Calisah amepata shavu kutoka kampuni moja ijulikanayo kama Ice Model ambayo inadeal modelling...
VIDEO: NEY WA MITEGO - SINA MUDA
Audio from Free Nation / Mr. T - Touch, Video Production : Joowzey
VIDEO: MESEN SELEKTA - SWEET LOVE
Music video by Mesen Selekta performing 'Sweet love'. Video directed by Ivan (Shine Studioz).
VIDEO: RABIT KING KAKA FT RICH MAVOKO - NJOO
Video mpya kutoka kwa Rabbit King Kaka featuring Rich Mavoko. iitwayo 'Njoo'.
Showing posts with label KITAIFA. Show all posts
Showing posts with label KITAIFA. Show all posts
Thursday, 4 December 2014
Friday, 7 November 2014
WAKUU WAPYA WA MIKOA NA MABALOZI KUAPISHWA IKULU DAR ES SALAAM
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Nov
05 amefanya uteuzi wa wakuu wapya wanne wa Mikoa na kuwahamisha wengine
sita na watatu wengine kupangiwa kazi nyingine.
Wakuu wapya wa Mikoa hao ni pamoja na Bi. Halima Omari Dendego ambaye amekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,Dkt. Ibrahim Hamisi Msengi ambaye amekuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Bi. Amina Juma Masenza ambaye amekuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa na Bwana John Vianney Mongella ambaye nae amekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
Wakuu wa Mikoa ambao wamehamishwa vituo vya kazi ni pamoja na Bwn. Magesa S. Mulongo ambaye atakua Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kutoka Arusha,Dkt. Rehema Nchimbi ambaye anakwenda Mkoa wa Njombe kutoka Dodoma,Bwana Ludovick John Mwananzila anakwenda Tabora kutoka Lindi,Kepteni (Mst) Anseri Msangi anayekwenda Mkoa wa Mara kutoka Njombe na Mhandisi Everist Ndikilo ambaye anakwenda Arusha kutoka Mwanza.
Wengine waliohamishwa ni Luteni (Mst) Chiku A.S. Galawa ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kutoka Tanga, Dkt. Rajab Rutengwe ambaye anakwenda Mkoa wa Tanga kutoka Katavi, Bi Fatma Mwasa ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita kutoka Tabora na Bwana Magalula S. Magalula ambaye anahamishiwa Lindi kutoka Geita.
Taarifa hiyo imesema kuwa Wakuu wa Mikoa ya Dar es Salaam, Kigoma, Kilimanjaro, Manyara, Mbeya,Morogoro, Pwani, Rukwa, Shinyanga, Ruvuma, Singida na Simiyu watabakia kwenye vituo vyao vya sasa.
Wengine walioapishwa leo Ikulu ya Dar es salaam na Rasi Jakaya Kikwete ni pamoja na mhe Samwel William Shellukindo kuwa balozi na msaidi wa rais masuala ya diplomasia,Dkt Yohana Budeba kuwa katibu mkuu wizara ya maendeleo ya mifugo na uvuvi,Injinia Mbogo Futakamba kuwa katibu mkuu wizara ya maji.
Mbali na hao pia wengine ni Dkt Donan Mmbando kuwa katibu mkuu wizara ya afya na ustawi wa jamii,Mhe Jack Mugendi Zoka kuwa balozi wa tanzania nchini Canada pia Mhe Charles Pallangyo kuwa katibu tawala wa mkoa wa geita na Bw Adoh Stephen Mapunda kuwa katibu tawala wa mkoa wa arusha.
Picha:issamichuzi.blogspot.com
Thursday, 6 November 2014
JESHI LA POLISI LINAWASHIKILIA WATU WAWILI KWA KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO]
JESHI LA POLISI LINAWASHIKILIA WATU WAWILI 1. HASSAN ADAMU [84], MKAZI WA ILEMI NA 2. ALPHONCE MWAKABANA [45] MKAZI WA MWENJELWA WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI[GONGO] UJAZO WA LITA 10.
TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 05.11.2014 MAJIRA YA SAA 14:30HRS HUKO ENEO LA ISANGA,KATA YA ISANGA,TARAFA YA SISIMBA JIJI NA MKOA WA MBEYA. WATUHUMIWA NI WATUMIAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI[GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NANI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
MTU MMOJA AMEKAMATWA BAADA YA KUWAUZIA WATU NYAMA YA MBWA.
JESHI LA POLISI LINAMSHIKILIA AHADI JESIKAKA [20] MKAZI WA KIJIJI CHA NGYEKYE KWA KOSA LA KUWAUZIA WATU NYAMA YA MBWA.
TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 04.11.2014 MAJIRA YA SAA 13:45HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA NGYEKYE,KATA YA MATEMA,TARAFA YA NTEMBELA WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA. WATU WALIOUZIWA NA KUTUMIA KITOWEO HICHO NI 1. ENOCK NSEMWA [52] MKAZI WA NGYEKYE 2. GEORGE NSEMWA [26],MKAZI WA NGYEKYE NA 3. ANYANDWILE MBWILO [29] MKAZI WA NGYEKYE.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUWA MAKINI HUSUSANI WANAPONUNUA VYAKULA ILI KUJIEPUSHA NA MADHARA YA KIAFYA.
Imesainiwa na:
[ AHMED Z. MSANGI – SACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
SOMA HII KUHUSU MWANAFUNZI ALIYEFARIKI KWA VIBOKO
Mwanafunzi
wa darasa la tano katika Shule ya msingi ya Kiuu Kenya amefariki dunia
baada ya kupigwa na mwalimu wake kwa kufeli somo lake la Kiswahili.
Familia ya mtoto huyo Joseph Waburi mwenye umri wa miaka kumi imesema mtoto huyo alikuwa na nidhamu ya hali ya juu.
Mama wa mwanafunzi huyo Grace Muthoni amesema mtoto wake alienda shule Jumatatu asubuhi na aliporudi alianza kulalamika maumivu ya kichwa na shingo, siku iliyofuatia alimpeleka Zahanati ya Wilaya ya Nyagiti level 4.
Siku ya pili alilazimika kumrudisha Hospitali baada hali yake kuzidi kuwa mbaya daktari akashauri ahamishiwe katika Zahanati ya Muran’ga Level 4 kwa matibabu zaidi wakati akisubiri gari la wagonjwa akafariki dunia.
Mama huyo amesema uchunguzi wa awali unaonyesha mtoto wake alipigwa na Mwalimu na kupata majeraha kichwani na shingoni, mwili wake umehifadhiwa kwa ajili ya uchunguzi kubaini sababu za kifo chake.
Mwalimu anayedaiwa kumpiga Mwanafunzi huyo alikimbia kujificha shimoni baada ya kusikia taarifa za kifo, huku Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Joseph Mwenda akikanusha uvumi kwamba mtoto huyo alifia shuleni.
SOMA TAARIFA KUHUSU AJALI ILIYOHUSISHA TRENI TAZARA JIJINI DAR ES SALAAM
Hii ni taarifa ya ajali ambayo imegharimu maisha ya Watu kumi na mbili,wakiwemo wanaume sita,wanawake wanne na watoto wawili baada ya basi mali ya kampuni ya Al-Jabir yenye namba za usajili T 725 ATD kuigonga na treni ya Shirika la Reli la Tanzania na Zambia(Tazara).
Ajali hiyo imetokea majira ya saa tisa alasiri katika eneo la Kiberege ifakara wilayani kilombero Mkoani Morogoro,Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Sacp Leonard Paulo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
Tuesday, 4 November 2014
RUFAA YA PONDA YATUPILIWA MBALI, KESI YAKE YAAHIRISHWA
Ponda akiingizwa kwenye basi la wafungwa kwa ajili ya kwenda Segerea.
Magari ya Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) yakiwa yametanda eneo la mahakama.
Askari wakiongoza msafara.(P.T)
Wafuasi wa Ponda wakiimba nyimbo mbalimbali nje ya mahakama.
Dola ikifanya mawasiliano kuimarisha ulinzi.
Ukaguzi mkali kwa kutumia kifaa maalumu ukifanyika katika mlango wa kuingilia Mahakama Kuu.
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, jana imetupilia mbali rufaa ya Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda iliyopelekwa na wakili wake Juma Nassoro ya kupinga hatia ya adhabu aliyohukumiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akidai kuwa hapakuwa na ushahidi wa kutosha wa kumtia hatiani kwa mashtaka yaliyokuwa yakimkabili.
Kesi nyingine ya uchochezi inayomkabili kiongozi huyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambayo inasikilizwa na Jaji Augustine Shangwa imeahirishwa hadi Novemba 20, mwaka huu.
Friday, 31 October 2014
SHIWATA WAGAWA MASHAMBA KWA WANACHAMA WAKE
Msanii Maarufu nchini Ahmed Olotu 'Mzee Chilo' wa kwanza kulia akimsikiliza mwenyekita wa SHIWATA Cassim Taalib wa pili kushoto walipokuwa wakigawa mashamba kwa ajili ya wanachama wao |
Watakaohamia kijiji cha wasanii kupewa bustani bure
Na Mwandishi Wetu
MTANDAO
wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umetoa bure kwa wanachama wake
wanaomiliki nyumba katika kijiji chao cha Mwanzega Mkuranga ya eneo la
kulima bustani.
Mwenyekiti wa SHIWATA,Cassim Taalib aliwaambia
waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuwa watakaonufanika na ofa hiyo
ni wale watakaohamia katika nyumba zao kabla ya Desemba mwaka huu ambapo
mtandao unaadhimisha miaka 10 kutoka uanzishwe.
Alisema
wanachama hao wanatakiwa kufika SHIWATA kugaiwa maeneo hayo ambayo
yatalimwa mazao ya muda mfupi (ambayo si ya kudumu) kama vile
pilipili,mahindi, matango, pilipili hoho, mananasi, mbogamboga, matikiti
maji ambayo hustawi kwa wingi maeneo hayo.
Katika hatua nyingine
SHIWATA imeamua kusafisha shamba la ekari 200 ambazo zimekwisha gaiwa
kwa wanachama ambao walijitokeza kulima katika shamba hilo la 500
zinazomilikiwa na mtandao huo kwa ajili ya maandalizi ya kilimo kwanza
msimu huu katika kijiji cha Ngarambe, Mkuranga.
Mwenyekiti Taalib
alisema SHIWATA imeingia mkataba na Kampuni ya Willy Enterprises Ltd ya
Dar es Salaam kukodisha mtambo wa kusafisha shamba (Buldoza) kwa ajili
ya wanachama zaidi ya 100 waliojitokeza kulima.
Alisema SHIWATA
itatumia sh. mil. 22.2 kukodisha buldoza hilo kusafisha shamba la ekari
200 zilizogaiwa kwa wanachama ambapo kila mmoja atalipa gharama ya sh.
111,000 kwa ekari moja.
Jitihada za kusafisha shamba hilo
zinafanywa na SHIWATA ikiwa ni maandalizi ya kufikiwa kwa malengo ya
kuanzishwa mtandao huo utakaoadhimisha miaka 10 ya kuanzishwa mwaka
2004.
Mpaka sasa SHIWATA inao wanachama 8,000 kutoka fani
mbalimbali za uigizaji, muziki wa dansi, muziki wa kizazi kipya, taarab,
soka, netiboli, vijana na waandishi wa habari.
Mwanachama wa siku nyingi wa Shiwata Manase Zabron ambaye ni kocha wa mpira wa kikapu nchiniakienda kuoneshwa shamba lake
Baadhi ya viongozi wa Mtandao wa wasanii Tanzania 'SHIWATA' wakishudia ugawaji wa mashamba kwa wanachama wake juzi Ngarambe Mkulanga Mkoa wa Pwani
Tuesday, 28 October 2014
BOMU LILILOTEGWA (TBC)SONGEA LATEGULIWA NA JESHI LA POLISI PAMOJA NA JWTZ
Jeshi la polisi kwa kushirikiana na Jeshi la Ulinzi la wananchi Tanzania(JWTZ) wamefanikiwa kulipua bomu lililotegwa katika eneo la kituo cha kurushia matangazo kilichopo mshangano cha shirika la utangazaji Tanzania (TBC) Songea Mkoani Ruvuma siku ya jana majira ya saa moja jioni.
Bomu hili linalosadikiwa kutengenezwa kienyeji nawatu wasiojulikana lilitegwa hatua zinazokadiliwa thelathini kutoka kitika kituo kilipo katika eneo ambalo askari wa usalama barabarani wanakaa kwa ajili kufanya kazi zao za kila siku.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela amesema kwamujibu wa wataalamu wa milipuko kutoka jeshi la Ulinmzi la wananchi wa Tanzania bomu hili linaonekakana limetengenezwa kienyeji.
ameitaka jamii kutoa ushrikiano kwa jeshi la polisi ili liweze kuwabaini watu waliowalipua kwa bomu lililotengenezwa kienyeji askari polisi watatu wakiwa katika doria katika kata ya misufini manispaa ya songea.
Msikhela amesema Jeshi la polisi linafanya jitihada za kuwapata watu hawa wanaohusika na mtandao huu wa utegaji wa mabomu na ulipuaji, Aidha ameitaka jamii kutoa ushrikiano kwa Jeshi la Polisi ili liweze kuwabaini watu wanaousika na matukio ya namana hii.
Na hii ni mara ya pili katika manispaa ya songea kutokea kwa matukio haya ambapo tarehe Oktoba 16 mwaka huu askari watatu wa jeshi la polisi katika wilaya ya Songea mkoani Ruvuma, walijeruhiwa kwa kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu la kutupwa kwa mkono ambalo lilisadikiwa kutengenezwa kienyeji, katika eneo la matarawe mjini songea mkoani Ruvuma.
Askari hao walikutwa na mkasa huo saa moja na nusu usiku wakati wakiwa katika doria ambao ni WP Felista Abel, PC John Kaduma na PC Ramadhani Ally
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Joseph Mkirikiti akizungumza na mtandao huu wa demasho kwa njia ya simu amesikitishwa na kitendo hicho cha utegeji wa Mabomu ikiwa nikutaka kuhatarisha amani iliyopo katika mkoa huu wa Ruvuma.
Aidha amesema serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama watahakikisha wanawasaka na kuwakamata walewote wanaohusika na vitendo hivi.
SHUHUDIA PICHA ZA JWTZ WAKITEGUA BOMU KATIKA ENEO LA KITUO CHA KURUSHIA MATANGAZO CHA TBC SONGEA
Bomu lililotengenezwa kienyeji kama linavoonekana katika picha.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela akipata maelekezo kutoka kwa mtaaram wa mabomu ambaye ni kamanda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) kabla ya kulitegua bomu hili.
Hili ni eneo la tukio ambalo limezungushiwa mkanda huu wa polisi uliandikwa hairuhusiwi kupita eneo hili,Lakini chini ya huo mti kama inavyoonekana katika picha kukiwa na udongo umetifuliwa ndipo mahara ambapo lilitegwa bomu hili la kutengenezwa kienyeji pia hapo ndipo huwa wanakaa askari wa Usalama barabarani kwa kujikinga na jua ama kupumzika pindi wanapokuwa kazini
Bomu lililotengenezwa kienyeji
Mtaalamu toka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania akiweka vifaa vyake vya kutegulia bomu hilo lililo tengenezwa kienyeji.
Mtaalamu toka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania akiwa anaonyesha kulitegua bomu bila kuleta madhara yoyote yale katika jamii.
Monday, 27 October 2014
NECTA YAFANIKIWA UDHIBITI WA WIZI NA UDANGANYIFU KATIKA MITIHANI YA TAIFA.
Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limedhibiti na kuondoa kabisa tatizo la wizi wa Mitihani ya Taifa na udanganyifu wakati wa Mitihani katika ngazi mbalimbali za elimu nchini.
Mafanikio hayo yametokana na ushirikiano uliopo kati ya NECTA na kamati za uendeshaji mitihani katika ngazi za mikoa na wilaya ili kutatua tatizo la wizi wa mitihani ya taifa na udanganyifu wakati wa mitihani uliokuwa ukifanywa kinyume na taratibu za baraza la mitihani.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala wa Baraza hilo Bw. Daniel Mafie wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jjijini Dar es salaam uliolenga kueleza mafanikio yaliyofikiwa hadi sasa.
Akifafanunua Mafie amesema kuwa katika mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi mwaka 2013 watahimiwa waliofutiwa matokeo kwa kufanya udanganyifu walikuwa 13 tu ikilinganishwa na watahiniwa 9,736 waliobainika kufanya udanganyifu mwaka 2011.
Aidha Mafie aliongeza kuwa katika Mtihani wa Kidato cha nne mwaka 2013 watahimiwa waliofutiwa matokeo kwa kufanya udanganyifu walikuwa 272 ikilinganishwa na watahimiwa 789 mwaka 2012 na 3,303 mwaka 2011.
Akieleza zaidi kuhusu mafanikio yaliyofikiwa Mafie alisema Baraza hilo limeweza kusanifu mifumo ya Kompyuta yenye uwezo wa kupanga shule katika makundi ya ubora wa ufaulu katika matokeo ya mitihani ya Taifa.
Katika kukabiliana na tatizo la watu wanaotumia vyeti vya watu wengine au kughushi vyeti wakati wa kuomba ajira au nafasi za masomo katika shule mbalimbali ambapo kuanzia mwaka 2008/2009 Baraza hilo lilianzisha utaratibu wa kuweka picha za watahimiwa katika vyeti vyao.
Katika utaratibu huo vyeti hivyo viliwekewa alama za kiusalam hali ambayo imesaidia Baraza hilo kuwa na uwezo wa kubaini kwa haraka na kuwachukulia hatua wale wanaoghushi vyeti au kutumia vyeti vya watu wengine.
Baraza la Mitihani la Tanzania ni Taasisi ya Umma iliyochini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi iliyoanzishwa kwa sheria ya Bunge Namba 21 ya mwaka 1973 na marekebisho yake ya mwaka 1998 na 2002 kwa ajili ya kuendesha mitihani ya Taifa kwa lengo la kuweka misingi ya sera ya mitihani, kuendesha mitihani na kutunuku stashahada mbalimbali na vyeti kwa watahiniwa wanaofuzu na kufaulu mitihani iliyo chini yake kisheria.
Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) Bw. Daniel Mafie akiwaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu mafanikio yaliyofikiwa na Baraza hilo ikiwemo matumizi ya TEHAMA katika usajili wa watahimiwa na uchakataji wa matokeo ya Mitihani ya Taifa. Kulia ni Afisa Habari wa NECTA John Nchimbi.
Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) Bw. Daniel Mafie akiwaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar s salaam kuhusu utaratibu wa kutoa nakala za vyeti kwa watahimiwa waliopoteza vyeti vyao ambapo utaratibu huo unahusisha uchunguzi wa uhalali wa mwombaji. Kulia ni Afisa Habari wa NECTA John Nchimbi na kushoto ni Msaidizi wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania Bi Glee Magemba.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) na Vyombo vya habari uliofanyika leo jijini Dar es salaam ukilenga kuonyesha mafanikio ya Baraza hilo nchini.(picha maelezo)
Sunday, 26 October 2014
TANZANIA IMEOMBA MADKARI ZAIDI KUTOKA SERIKALI YA CHINA.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
Tanzania imeiomba Jamhuri ya Watu wa China kuongeza idadi ya madaktari wake inaowatuma Tanzania kama msaada kutoa huduma ya tiba kama njia ya kuzidi kusaidia kukabiliana na upungufu wa madaktari nchini.
Aidha, Tanzania imeishukuru China kwa kujenga hospitali kubwa inayoweza kulaza wagonjwa 100 kwa wakati mmoja wa magonjwa ya moyo na yenye uwezo wa kuwafanyia wagonjwa wa moyo operesheni.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametoa ombi hilo na shukurani hizo jana, Jumamosi, Oktoba 25, 2014 wakati alipokutana na kuzungumza na Mheshimiwa Jiang Yikang, Katibu wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) cha Jimbo la Shandong, jimbo ambalo tokea mwaka 1968 limekuwa linatuma madaktari kutoka jimbo hilo kuja nchini kusaidia kutoa huduma ya tiba.
Rais Kikwete ambaye yuko katika ziara rasmi ya Kiserikali katika China amesimama kwa siku nzima katika mji mkuu wa Jimbo la Shandong wa Jinan akiwa njiani kutoka Beijing kwenda Jimbo la Shenzhen ambako atafanya ziara kesho, Jumapili,Oktoba 26.
Rais Kikwete na ujumbe wake ambaye amesafiri kwa treni iendayo kasi kutoka Beijing, amewasili kwenye Kituo cha Treni cha Jinan Magharibi kiasi cha saa 5:53 na kupokelewa na viongozi wa Serikali na wa CPC wa Jimbo hilo, siyo mbali na nchi jirani ya Korea kusini.
Rais Kikwete amemwambia Mheshimiwa Yikang: “Tunalishukuru sana Jimbo la Shandong ambalo kwa miaka 46 tokea mwaka 1968 limekuwa linatuma madaktari wake kuja Tanzania kutoa huduma ya tiba kwa msaada. Tumepokea makundi 23 ya madaktari zaidi ya 1,000 ambao huja kila baada ya miaka miwili. Tunalishukuru sana Jimbo hilo kwa msaada huu mkubwa.”
Ameongeza Rais Kikwete: “Lakini bado tunazidi kuwaomba muendelee kutusaidia. Tunahitaji madaktari wengi zaidi kwa sababu uwiano kati ya daktari na wagonjwa nchini kwetu bado ni mkubwa. Katika mazungumzo yangu na Rais Xi Jinping jana nilitoa ombi hili, lakini nalitoa tena hapa kwa sababu madaktari wanatoka Jimbo hili.”
Rais Kikwete pia amelishukuru Jimbo hilo kwa msaada uliowezesha kujengwa kwa Hospitali ya Moyo kwenye Hospitali Kuu ya Taifa ya Muhimbili, Dar Es Salaam. “Hospitali hii ya kisasa kabisa sasa imeanza kufanya kazi. Imeiweka nchi yetu kwenye ngazi tofauti kabisa. Tunawashukuru sana kwa kuendelea kuuunga mkono.”
Jimbo la Shandong ni la tatu kwa utajiri na uchumi imara katika China ambalo pato lake mwaka jana lilikuwa ni dola za Marekani bilioni 882.9 kiasi kikubwa kuliko nchi nyingi za Afrika zikiwekwa kwa pamoja. Thamani ya biashara kati ya Jimbo hilo na Tanzania kwa maka jana ilikuwa dola za Marekani milioni 470.
Baadaye jioni, Rais Kikwete alikutana na baadhi ya madakati waliopata kufanya kazi katika Tanzania na akawashukuru kwa mchango wao katika maendeleo ya huduma ya tiba nchini.
Amewaambia madaktari hao kwenye Hospitali Kuu ya Jimbo la Shandong: “Nimeomba niwaone ili niwashukuru sana kwa kuokoa maisha ya watu wetu. Mnashikilia nafasi ya pekee katika mioyo ya Watanzania. Kama mnavyojua fika, madaktari wa Shandong wamekuwa wanatusaidia katika Tanzania tokea 1968 na mpaka sasa kiasi cha madaktari 1223 wametusaidia. Kuna wakati lilikuja hapa kundi kubwa la madaktari 84 kwa wakati mmoja. Nyie mnajua Kiswahili – Nasema asanteni sana.”
Hospitali hiyo ni moja ya hospitali za Jimbo hilo ambazo zimekuwa zinapeleka madaktari wake Tanzania tokea mwaka 1968. Mwaka huo, hospitali hiyo iliweka katika kundi la madaktari waliokwenda Tanzania madaktari wake wanne.
Katika miaka yote 46, Hospitali hiyo imepeleka Tanzania madaktari 70 na kwa sababu ya kazi hiyo nzuri Mei mwaka 2004, Rais Benjamin William Mkapa aliitembelea Hospitali hiyo, akakutana na kuwashukuru madaktari waliokuwa wametoa ujuzi wao kuokoa maisha ya Watanzania. Hospitali hiyo iliyoanzishwa mwaka 1897, ina historia ya miaka 117 ya kutoa huduma za tiba.
Wakati huo huo, Rais Kikwete ametembelea Kampuni ya Kompyuta ya Inspur iliyoko mjini Jinan na baada ya kutembelea Kampuni hiyo ameondoka mjini Jinan kwenda mji wa Shenzhen ambako atafanya ziara ya siku mbili kuanzia baadaye leo.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
25 Oktoba, 2014
MATUKIO MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA KICHWA KIKUBWA DUNIANI.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dkt. Othmani Kiloloma akiwaeleza waandishi wa habari(hawapo pichani) majukumu wanayotekeleza katika kuhakikisha wanakabiliana na tatizo la Mgongo wazi na Vichwa vikubwa ikiwamo kutoa elimu bora kwa madaktari wanaosomea somo hilo, kwenda mikoani kutoa tiba kwa watoto wenye matatizo hayo,wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na na Mgongo wazi duniani jana Jijini Dar es salaam. Kushoto ni mwenyekiti wa chama cha wazazi wenye watoto wa kichwa kikubwa na mgongo wazi(ASBHAT) Bw. Abdulhakim Bayakub.
Mwenyekiti wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) Bw. Abdulhakim Bayakub akitoa rai kwa watanzania wanaoguswa na tatizo hili kujitokeza na kusaidia chama hicho ikiwa ni njia ya kuwasaidia watoto wenye tatizo hilo ili kuokoa maisha yao kwa mpaka sasa Chama kina mfadhili mmoja.Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dkt. Othmani Kiloloma
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dkt. Othmani Kiloloma akimkabidhi Mama Dorcas Membe kitabu cha Mpango shirikishi wa Mtoto wa kichwa kikubwa na Mgongo Wazi na kumuomba kuwa Mlezi wa chama cha Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) ambapo ameahidi kushirikiana na chama hicho katika harakati za kukabiliana na Tatizo la Kichwa Kikubwa na Mgongo wazi. kulia ni Mwenyekiti wa Chama hicho Bw. Abdulhakim Bayakub.
Mwenyekiti wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) Bw. Abdulhakim Bayakub akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dkt. Othmani Kiloloma cheti shukrani kwa mchango wanaoendelea kuutoa cha chama hicho ikiwamo kutoa matibabu kwa Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi.
Baadhi ya wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi waliojitokeza katika sherehe hizo za Maadhimisho ya ya siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na na Mgongo wazi duniani yaliyofanyika Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) jana Jijini Dar es Salaam.
Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Bi. Germana Gasper akitoa maaelezo kwa wananchi waliojitokeza katika banda wakati wa sherehe na kuwaasa wazazi hasa wakike waliokatika umri wa kubeba mimba kutumia vyakula vyenye vitamin ya Foliki kama maembe, Mchicha, Mihogo,machungwa, maharage, mahindi,mayai, ndizi, parachichi, papai, maini na kabichi, ili kukabiliana na tatizo la Kichwa kikubwa na Mgongo wazi kwa watoto wanaozaliwa.
Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Bi. Germana Gasper akiwaonyesha wananchi kipimo cha hali lishe kwa mtoto wakati wa Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na Mgongo wazi duniani jana Jijini Dar es salaam.
Mlezi wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) Mama Dorcas Membe akiteta jambo na moja ya mtoto mwenye tatizo la kichwa kikubwa anayepata huduma Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI).
Mlezi wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) Mama Dorcas Membe, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dkt. Othmani Kiloloma(Kulia), Mwenyekiti wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) Bw. Abdulhakim Bayakub(mwenye T-shirt nyeupe) na Moja ya mtoto mwenye tatizo la Kichwa Kikubwa wakikata keki katika sherehe za Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na Mgongo wazi duniani jana Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dkt. Othmani Kiloloma akimlisha keki Moja ya mtoto mwenye tatizo la Kichwa Kikubwa wakikata keki katika sherehe za Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na Mgongo wazi duniani jana Jijini Dar es salaam.
Mlezi wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) Mama Dorcas Membe akimlisha keki Moja ya mtoto mwenye tatizo la Kichwa Kikubwa wakikata keki katika sherehe za Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na Mgongo wazi duniani jana Jijini Dar es salaam.
Mlezi wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) Mama Dorcas Membe akikabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa Mwenyekiti wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) Bw. Abdulhakim Bayakub.
Mlezi wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) Mama Dorcas Membe akiwapa msaada kinamama wenye watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi.(PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO).
Subscribe to:
Posts (Atom)







