Followers

VIDEO: B.O.B N' MICHARAZO - KAZI KWANZA

Hatari nyingine town kutoka kwa B.O.B MICHARAZO 'kazi kwanza'

.

TZEE MODAL APATA DILI SOUTH AFRICA

Calisah amepata shavu kutoka kampuni moja ijulikanayo kama Ice Model ambayo inadeal modelling...

VIDEO: NEY WA MITEGO - SINA MUDA

Audio from Free Nation / Mr. T - Touch, Video Production : Joowzey

VIDEO: MESEN SELEKTA - SWEET LOVE

Music video by Mesen Selekta performing 'Sweet love'. Video directed by Ivan (Shine Studioz).

VIDEO: RABIT KING KAKA FT RICH MAVOKO - NJOO

Video mpya kutoka kwa Rabbit King Kaka featuring Rich Mavoko. iitwayo 'Njoo'.

Showing posts with label VITUKO. Show all posts
Showing posts with label VITUKO. Show all posts

Wednesday, 5 November 2014

HOTELI YA WANYAMA YAFUNGULIWA SINGAPORE

Hoteli moja ya kifahari ya wanyama wa kufugwa nyumbani imefunguliwa nchini Singapore.

Hoteli hiyo inatoa huduma kama vile vidimbwi vya kuoga vya wanyama hao,vyumba vyenye hewa safi na vyakula vya kuvutia, na hivyobasi kuimarisha viwango vya kuwabembeleza wanyama hao katika taifa hilo lenye utajiri mkubwa.

Hoteli hiyo yenye urefu wa futi 4,317 kwa jina Wagington Hotel imejengwa katika nyumba za zamani za wakolini wa Uingereza zilizobadilishwa katika makaazi ya wanadiplomasia.

Vyumba vya kulalia katika hoteli hiyo vinagharimu dola 271 kwa mbwa watatu wanaotumia kwa pamoja chumba cha kifalme,kilicho na maeneo ya kifahari ya kuweka balbu,runinga,na vitanda vilivyotengezwa na ngozi.

Hoteli hiyo iliojengwa hususan kwa mbwa pia huwakaribisha paka.

''iwapo tunajitakia mema katika maisha yetu, kwa nini marafiki zetu walio waaminifu nao tusiwafanyie mambo mazuri'' aliuliza mmiliki wa hoteli hiyo Estelle Taylor.

''Kama watu tunaowapenda wanyama,tuna hisi kwamba ni vyema kuwa na eneo ambalo wanyama wanaweza kuwekwa ili nao wajisikie nyumbani'' aliongezea.

Wanaomiliki wanyama hao pia wanaweza kupata eneo la kufanya mafunzo,kunyoa, kukata kucha,kubadilisha rangi za wanyama hao pamoja na masaji.

Hoteli hiyo pia hutoa huduma ya gari la kifahari aina ya Limousine kwa wanyama hao kutoka makaazi yao hadi hoteli hiyo na kutoka hoteli hiyo hadi makaazi yao.

Nchini Singapore kuna zaidi ya maduka 250 ya wanyama, mengi yakiwa katika maduka makubwa ya jumla.

Mfanyibiashara mmoja hutoa huduma za kitalii kila wikendi ambapo wamiliki wa wanyama hao na wanyama wenyewe hutembezwa katika maboti.BBC

Tuesday, 28 October 2014

KISA CHA MWIZI KUIBA NA KUJISAIDIA HAJA ANAPO MALIZA WIZI WAKE

Mwizi mmoja nchini Uchina aliyekuwa na tabia ya kujisaidia haja kubwa katika nyumba anazofanywa wizi wake, hatimaye amekamatwa kutokana na teknolojia ya DNA.

Polisi jijini Cixi, katika jimbo la Zhejiang wamesema mwizi huyo aitwaye Chen mwenye umri wa miaka 29 akiwa na mwenzake walivunja nyumba moja na kuingia jikoni na kula chakula, kabla ya bwana Chen kujisaidia kwenye sakafu karibu na mlango.

Baada ya kufanya hayo, wawili hao wakaanza kutafuta vitu vya kuiba ndani ya nyumba hiyo, lakini kutokana na kukuru kakara zao, mwenye nyumba alishtuka, na wezi hao kukimbia bila ya kuiba chochote. Miezi michache baadaye, wezi hao waliingia katika nyumba nyingine na kuiba kompyuta mpakato-- yaani Laptop na fedha taslimu yuan elfu moja.

Kama kawaida, waliingia jikoni na kujipakulia chakula, na bwana chen kuacha muhuri wake wa kawaida, wa kinyesi chenye harufu kali karibu na mlango wa mbele. Mtandao wa china daily umesema polisi walifanikiwa kulinganisha vipimo vya DNA na mwizi Chen, ambaye aliwahi kutupwa gerezani kwa kosa jingine mwaka 2003. Baada ya kukamatwa, bwana Chen alikiri kujisaidia katika nyumba anazofanya wizi, akisema, amekuwa akisoma katika vitabu mbalimbali jinsi wezi wanayokuwa na mitindo yao ya kipekee, wanapofanya wizi. Polisi bado wanamsaka mwizi mwenzake.

Thursday, 23 October 2014

HUYU HAPA NGAMIA ALIYEUA KWA KUKOSA SODA SOMA STORI YOTE.



Camel-Coke-addict-1040x900_cRichard Mileski (60), aliyekuwa mmiliki wa hifadhi ya wanyama pori nchini Mexico ameuawa kikatili na ngamia aliyekuwa akimfuga katika hifadhi hiyo kutokana na kutompatia ngamia huyo ‘dozi’ ya soda aliyomzoesha kumpatia.

Taarifa kutoka mtandao wa rt.com zinasema ngamia huyo alimvamia Mileski ndani ya hifadhi hiyo na kumpiga mpaka kuishiwa nguvu, na baada ya kuanguka chini ngamia huyo alimkalia juu yake kitendo kilichopelekea mtu huyo kufariki.

Maafisa usalama waliofika katika eneo hilo, walilazimika kumfunga kamba ngamia huyo na kumvuta kwa gari ndogo ili waweze kuutoa mwili wa marehemu huyo.

Taarifa za awali zinasema huenda ngamia huyo alikasirishwa na kitendo cha Mileski kutompatia soda aina ya Coca cola alichozoea kumpatia.

Mileski alianzisha hifadhi hiyo maalum aliyoipa jina la ‘Tulum Monkey Sanctuary’ kwa ajili ya kuhifadhi nyani na buibui ambao walikuwa wakitoweka nchini humo, na baadaye aliongeza wanyama wengine, japo serikali imesema alianzisha hifadhi hiyo bila ya kuwa kibali wala leseni.

Richard Mileski, mmiliki wa hifadhi aliyeuawa na ngamia.

Richard Mileski, mmiliki wa hifadhi aliyeuawa na ngamia.

Kwa miaka 15 Mileski amejitolea maisha yake kwa kuhifadhi wanyama katika hifadhi hiyo iliyojizolea umaarufu kwa shughuli za utalii. Mtandao wa China.org.cn wa China umemtaja ngamia huyu ni mnyama wa kwanza kufanya mauaji ya kikatili zaidi duniani.

Tuesday, 21 October 2014

MAAJABU YA DADA ALIYEGEUKA PUNDA.

Bwana mmoja nchini Zimbabwe amedai kuwa kahaba aliyekuwa akifanya naye mapenzi amegeuka ghafla na kuwa punda.

Bwana huyo, Sunday Moyo ambaye amefikishwa mahakamani siku ya Jumatatu kwa kosa na kukutwa akifanya mapenzi na mnyama huyo amesema anampenda sana mpenzi wake huyo. Bwana Moyo aliiambia mahakama mjini Zvishavane kuwa huyo waliyemkuta naye sio punda bali ni mwanamke ambaye alikutana naye katika klabu ya usiku ya starehe.

Gazeti la Metro limesema polisi wa Zimbabwe wakiwa katika doria saa za alfajiri, walimkuta bwana huyo mwenye umri wa miaka 28, katika mji wa Mandava, akifanya mapenzi na punda nje ya nyumba yake. Mnyama huyo alikuwa amelala chini huku shingo yake ikiwa imefungwa kamba, na kamba hiyo kufungwa kwenye mti. Kwa mujibu wa mtandao wa New Zimbabwe.com bwana Moyo amekiri makosa ya kujamiiana na mnyama, lakini aliiambia mahakama kuwa "Mheshimiwa Jaji, niligundua tu kuwa ni mnyama, wakati polisi waliponikamata". Bwana huyo amesema alipata kahaba aliyekubali kulipwa dola ishirini, lakini amesema hafahamu ilikuwaje hadi akageuka na kuwa punda. "Lakini bado nampenda sana" amesema bwana Moyo. Bwana huyo ameswekwa rumande na kuamriwa kufanyiwa uchunguzi wa akili.