
Emmanuel Adebayor

STRAIKA wa Tottenham Hotspur, Emmanuel Adebayor amewatolea uvivu ndugu zake ambao wamekuwa wakimwandama kwamba hawapi msada wowote mbali na utajiri mkubwa alionao.
Miezi michache tu baada ya kumlaumu mamake mzazi kwa kumroga na kumfanya apoteze fomu yake, Emmanuel Adebayor anayeichezea timu ya Tottenham inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Uingereza, amejitokeza na kufichua jinsi familia yake ilivyomfanya afilisike bila shukrani.
Kupitia ukurasa wake wa facebook, Adebayor ameeleza kuwa

Picha iliyosindikiza ujumbe huu ndani ya Facebook account yake
"Nimekuwa
nikiziweka taarifa hizi kwa muda mrefu lakini leo nimehisi kuwa ni
muhimu kuwaeleza nanyi pia. Ni ukweli kuwa masuala ya familia
hayastahili kuwekwa hadharani lakini nafanya hivi ili familia nyingine
nzao zipate funzoi kupita yaliyonisibi. Aliandika

Anasema wakati alipokuwa na umri wa miaka 17, aliutumia mshahara wake wa kwanza kuijengea familia yake nyumba.Kama mnavyojua nilipokea tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika wa mwaka mwaka 2008.Nilimpandisha mama yangu jukwaani kumshukuru yeye kwa mambo yote. Mwaka ule ule nilimleta London kwa ajili uchunguzi wa afya yake.
Wakati binti yangu alipozaliwa niliwasiliana na mama yangu kumweleza lakini alikata simu na sikujua ni kwanini.Soma maoni yangu ya hivi karibuni watu wanasema mimi na familia yangu twende tupate ushauri kwa mhubiri maarufu wa dini ya kikristo T.B Joshua.Mwaka 2013 nilimpa mama yangu pesa ili aende kupata ushauri kwa mhubiri huyo nchini Nigeria.
Alipaswa kukaa huko kwa wiki moja, lakini siku mbili tu alipofika nilipokea simu kwamba ameondoka. Zaidi ya hayo nilimpa mama yangu pesa nyingi kuanzisha biashara kupika pamoja na bidhaa nyingine. Kiuhalisia niliwaruhusu kuweka jina langu na picha yangu kwenye biashara hiyo hiyo ili waweze kuvutia wateja.
Ni kitu gani kingine mtoto wa kiume anaweza kufanya ndani ya uwezo wake kusaidia familia yake?
Miaka kadhaa iliyopita, nilinunua nyumba huko East Lagon nchini Ghana kwa dola milioni 1.2 za kimarekani. Nikaona ni sawa dada yangu mkubwa Yabo Adebayor kuishi katika nyumba hiyo. Vile vile nilimruhusu kaka yangu Daniel naye aishi kwenye nyumba hiyo.
Miezi michache baadae nilifukuzwa kwenye nyumba niliyokuwa naishi ikianibidi kwenye hiyo nyumba yangu. Kilichonishangaza niliona magari mengi kwenye barabara. Kwa kweli dada yangu aliamua kuikodisha hiyo nyumba pasipo kunieleza. Alimfukuza Daniel kwenye hiyo nyumba.
Mfahamu
kwamba nyumba hiyo ina vyumba 15. Nilipompigia dada yangu anipe
ufafanuzi alichukua karibu nusu saa kunishambulia na kunitukana kwenye
simu. Nilimpigia mama yangu anaelezee kisa kizima naye akafanya kama
dada yangu alivyofanya. Hivyo ni kama dada yangu alivyosema sina
shukrani.

Emmanuel Adebayor akiwa na mama yake mzazi

0 comments:
Post a Comment