Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amewaambia mawaziri wa Afrika
Mashariki kwamba endapo atachaguliwa kuiongoza nchi hiyo mwezi June
mwaka huu ,kwa muhula wa tatu basi itakuwa ni kipindi cha ukomo wa yeye
kuendelea kusalia madarakani ,msemaji wa serikali ya Burundi Gervais
Abayehorwa amesema hayo mapema Jumatano .
Rais Pierre Nkurunziza
uamuzi wake wa kugombea kuiongoza nchi hiyo kwa muhula wa tatu uliibua
hisia tofauti tofauti na kuzusha maandamano makubwa. Waandamanaji
wanadai kwamba kwa muujibu wa katiba ya nchi hiyo rais anapaswa
kuiongoza nchi kwa mihula miwili tu.nayo mahakama ya katiba wameeleza
kwamba hawahesabu muhula wa kwanza wa raisi huyo madarakani kwasababu
aliteuliwa na wabunge na si kuchaguliwa kwa kupigiwa kura.
0 comments:
Post a Comment