Mheshimiwa Profesa Makame Mbarawa ambaye ni waziri wa mawasiliano, sayansi na teknolojia ametoa taarifa rasmi kuhusu sheria ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015 kwa waandishi wa habari.
Isome hapa..
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA

TAARIFA YA MHE. PROF. MAKAME MBARAWA (MB), WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA KUHUSU SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAO YA MWAKA 2015 KWA WAANDISHI WA HABARI
TAREHE 8 MEI, 2015
Ndugu Wananchi,
Ndugu Waandishi wa Habari,
Kukua kwa kasi kwa matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kumeleta mafanikio mengi katika nyanja mbalimbali za maisha ya kila siku. Mafanikio haya yanathibitika kwa kuongezeka kwa huduma za mawasiliano, huduma za kifedha na matumizi ya mitandao ya kijamii. Aidha, mafanikio hayo yameleta changamoto nyingi katika jamii. Changamoto hizo ni pamoja na kuibuka kwa makosa mapya ya jinai na pia mbinu mpya za kutenda makosa ya zamani.
Ndugu Wananchi,
Makosa hayo yanajumuisha uhalifu wa mitandao ambapo simu za mkononi, kompyuta au mifumo ya kompyuta hutumika kama nyenzo za kutenda uhalifu huo. Mifano ya makosa hayo ni pamoja na yafuatayo:
1. Wizi wa fedha kwa njia ya mtandao;
2. Ugaidi unaofanyika kupitia kwenye mitandao;
3. Maudhui potofu yanayosababisha mmomonyoko mkubwa wa maadili,
4. Uharibifu wa miundombinu muhimu ya Taifa unaofanywa kwa makusudi. Kwa mfano kukatwa kwa makusudi Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano. Hii imepelekea Serikali na watoa huduma na wananchi kwa ujumla kupata hasara na kusababisha ukosekanaji wa huduma mbalimbali za kiuchumi na za kijamii.
Ndugu Wananchi,
Kama mnavyofahamu kwamba kwenye Mkutano wa 19 wa Bunge la 10 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililopita, Serikali ilipeleka Mswada wa kutunga Sheria ya Uhalifu wa Mtandao (The Cyber Crimes Act) ambayo ilipitishwa na Bunge hilo. Madhumuni ya kutunga sheria hii kama ilivyo kwa sheria nyingine zilizotungwa na Bunge hapa nchini ni kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii hususan kwenye matumizi ya TEHAMA.
Ndugu Wananchi,
Ndugu Wandishi wa Habari,
Tanzania siyo nchi ya kwanza kutunga sheria kama hii. Zipo nchi nyingi duniani zilizo na sheria kama hii. Mfano wa nchi hizo ni Uingereza (UK Computer Misuse Act, 1990), India (IT Act, 2000), Malaysia (Computer Crime Act), Uganda (Computer Misuse Act, 2010), Korea ya Kusini (Information and Communications Network Act na Information and Communication Infrastructure Protection Act), Singapore (The Computer Misuse and Cybersecurity Act), Mauritius (Computer Misuse and Cybercrime Act, 2003), Marekani (Computer Fraud and Abuse Act, 1984) na nyingi nyinginezo.
Ndugu Wananchi,
Kutungwa kwa Sheria hii itasimamia makosa ya mtandao, kunawapa wananchi uhakika zaidi wa matumizi ya mtandao kwani mtu akitendewa uhalifu kupitia kwenye mtandao, sheria hii itamsaidia kupata haki. Ninawashangaa sana wale wanaopinga kutungwa kwa sheria hii hapa Tanzania. Haikubaliki hata kidogo kuona Watanzania wakiendelea kukumbana na uhalifu kupitia kwenye mtandao na watu wachache kwa faida zao binafsi wakitaka Serikali ikae kimya. Sheria hii ambayo haina tofauti na sheria za nchi nyingine nilizozitaja hapo awali na ambayo imetungwa kwa kuzingatia mazingira ya nchi yetu imekuja kwa wakati kudhibiti hali hii.
Ndugu Wananchi,
Sheria hii ambayo sasa imekwisha sainiwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa sheria kamili imepitia hatua zote za uandishi na uboreshwaji. Hatua ya mwisho ilikuwa ni ile ya marekebisho yaliyofanywa na Bunge ambapo baadhi ya vifungu vilivyolalamikiwa na wadau mbalimbali viliboreshwa. Kwa hiyo ninawaomba wananchi sasa muipokee sheria hii na kuitumia. Sheria hii ni nzuri na itasaidia sana kuwalinda wananchi na kuhakikisha kuwa mitandao yetu inakuwa salama zaidi na miundombinu yetu muhimu ya kitaifa inalindwa.
Katika kuitumia sheria hii ni budi kuwa mapungufu kadhaa wa kadhaa yatajitokeza. Hali hiyo itakapotokea, kama ilivyo kwa sheria nyingine yoyote, mapungufu hayo yatarekebishwa. Kwa hiyo, kama kuna mtu yeyote mwenye maoni ya kuiboresha sheria hii basi alete maoni yake Serikalini ambapo yatafanyiwa kazi. Ninapenda kurejea tena jambo hili, iwapo Waheshimiwa Wabunge, Waheshimiwa Mabalozi, Wadau mbalimbali wa Sekta ya Mawasiliano, Waandishi wa Habari, Wana-blogger, na Wananchi kwa ujumla, kama kuna yeyote mwenye maoni ya kuboresha kifungu chochote cha sheria hii, basi alete maoni hayo hapa Wizarani. Serikali kupitia Wizara yangu itapokea maoni au ushauri huo, itautafakari na kuufanyia kazi kwa kina. Haitasaidia sana kwa mtu kusema juu ya mapungufu hayo huko pembeni. Mahali na jukwaa sahihi la kuleta maoni hayo ni kupitia Wizara yangu; Na itakapobidi sheria hii itafanyiwa marekebisho. Hii haitokuwa sheria ya kwanza kufanyiwa marekebisho kama umuhimu huo utajitokeza.
Ahsanteni na ninawashukuru sana kwa kunisikiliza.

0 comments:
Post a Comment