Bondia wa Fransic Cheka
anatarajia kupanda ulingoni kwa mara ya kwanza Mei 30 mwaka huu tangu atoke jela.
Cheka anatarajiwa kucheza na bondia Kiatchai Singwancha kutoka Thailand kwenye pambano la raundi kumi litakalofanyika katika ukumbi wa
P.T.A Sabasaba jijini Dar es salaam.
Kaike Siraju ambaye ndiye mwaandaaji wa pambano hilo amesema
kuwa amejipanga vizuri kwani kila kitu kinaenda vizuri kwa sasa ambapo
mabondia wa utangulizi wote wanatarajiwa kusaini mikataba wiki hili.
Pambano
hilo litasimamiwa na chama cha ngumi za kulipipwa Tanzania (TPBC) chini
ya rais wake Emanuel Mlundwa. Bondia Kiatchai atawasili nchini siku tatu
kabla ya mpambano huo
Credit: BBC
0 comments:
Post a Comment