Baada
ya stori kibao zilizothibitishwa na team nzima ya East Africa kupitia
kupitia kipindi chake cha Planet Bongo kusema kuwa Jumamosi ya tarehe
30/05/2015 ndiyo itakuwa mwisho wa kipindi hicho kilichokuwa kinaongozwa
na Abdallah Ambua na kufanya mashabiki wa kipindi hicho kutokuwa na
raha baada ya taarifa hizo.
Hatimaye
leo taarifa rasmi imetoka nini kitafuata baada ya kipindi hicho kufa
ambacho kilikuwa kinarushwa kila siku ya Jumamosi lakini sasa Team nzima
ya EATV kupitia kipindi hicho kimeamua kuwa kipindi hicho kitakuwa
kinarushwa kwa siku tano kwenye wiki ambapo itakuwa ni kuanzia siku ya
Jumatatu mpaka Ijumaa.

Siku
ya leo katika kipindi hiki kilinoga baada ya baada ya kuudhuriwa na Dj
John Dilinga, Prof Jay, Mwana Fa, Jay Mo, Enika, Mwasiti, huku Salama
Jabir na Dj Kim ndiyo walikuwa wanakiongoza kipindi hicho kwa leo.
Timu
mpya ambayo imetangazwa itakayo kuwa inaongoza kipindi hicho cha Planet
Bongo kwa sasa ni Abdallah Ambua aka Mjukuu wa Ambua, Annah Peter,
Kennedy The Remedy, Dj Ommy Crazy na Dj wa kike Sinyorita.
0 comments:
Post a Comment