VIDEO: B.O.B N' MICHARAZO - KAZI KWANZA
Hatari nyingine town kutoka kwa B.O.B MICHARAZO 'kazi kwanza'
TZEE MODAL APATA DILI SOUTH AFRICA
Calisah amepata shavu kutoka kampuni moja ijulikanayo kama Ice Model ambayo inadeal modelling...
VIDEO: NEY WA MITEGO - SINA MUDA
Audio from Free Nation / Mr. T - Touch, Video Production : Joowzey
VIDEO: MESEN SELEKTA - SWEET LOVE
Music video by Mesen Selekta performing 'Sweet love'. Video directed by Ivan (Shine Studioz).
VIDEO: RABIT KING KAKA FT RICH MAVOKO - NJOO
Video mpya kutoka kwa Rabbit King Kaka featuring Rich Mavoko. iitwayo 'Njoo'.
Showing posts with label MICHEZO. Show all posts
Showing posts with label MICHEZO. Show all posts
Wednesday, 5 November 2014
Tuesday, 4 November 2014
MWAKIBINGA AONDOKA BODI YA LIGI
OfisaMtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Silas Mwakibinga amemaliza mkataba wake tangu Oktoba 31 mwaka huu.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na TPLB wanamshukuru Mwakibinga kwa mchango wake kwa kipindi ambacho ameitumikia Bodi, na kumtakia kila la kheri katika majukumu yake mapya huko aendako.
TPLB hivi sasa iko katika mchakato wa kupata Ofisa Mtendaji Mkuu mpya kwa ajili ya kuziba nafasi hiyo iliyoachwa wazi na Mwakibinga baada ya muda wa mkataba wake kumalizika.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
KOCHA NOOIJ KUTAJA KIKOSI STARS
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij keshokutwa (Novemba 5 mwaka huu) atatangaza kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya mechi ya kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) itakayochezwa ugenini Novemba 16 mwaka huu.
Nooij atatangaza kikosi hicho mbele ya waandishi wa habari katika mkutano utakaofanyika saa 4.30 asubuhi kwenye ofisi za TFF zilizoko ghorofa ya tatu, Jengo la PPF Tower jijini Dar es Salaam.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itacheza na Swaziland, mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa wa Somhlolo jijini Mbabane.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
NGASA KUWA MFUNGAJI BORA LIGI YA MABINGWA AFRIKA
MSHAMBULIAJI wa Yanga, Mrisho Ngassa amepata zali Afrika, baada ya kumaliza kinara wa mabao kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, licha ya klabu yake kuaga mashindano hayo alfajiri kabisa.
Ngassa amemaliza kinara baada ya kufunga mabao sita na kufungana na Ndombe Mubele wa AS Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Haythem Jouini wa Esperance de Tunis ya Tunisia na El Hedi Belameiri wa ES Setif ya Algeria.
Ni baada ya Ligi ya Mabingwa Afrika kufikia tamati wikiendi iliyopita na ES Setif kutangazwa mabingwa wapya wakibebwa na bao la ugenini kutokana na matokeo ya sare bao 1-1 mchezo wa Algeria na sare mabao 2-2 mchezo uliochezwa Kinshasa.
Ngassa aliyafunga mabao hayo katika raundi ya kwanza walipocheza na Komorozine ya Comoro mchezo wa kwanza walishinda 7-0 na marudiano walitoka kifua mbele kwa mabao 5-2.
Yanga ilitolewa kwenye mashindano na Al Ahly ya Misri kwa penalti 3-4. Lakini Ngassa hawezi kupewa zawadi yoyote kwavile wamefungana na kiutaratibu hata mchezaji akishinda tuzo hiyo CAF huitoa kwa klabu yake.
Chanzo:Mwanaspoti
Monday, 27 October 2014
FIFA: TANZANIA YAPIGA HATUA, KENYA YAPATA PIGO.
Hivi karibuni vyombo vya habari vya michezo vimepambwa na taarifa za Tanzania kupanda viwango vya soka kwa mujibu wa takwimu za Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
Habari hizo zimepokewa katika namna nzuri ya kuonyesha kwamba Tanzania imepiga hatua na hivyo jambo hilo kuonekana ni la kujivunia.
Si nia yetu kubeza wanaojivunia mafanikio hayo kwani ndio ukweli wenyewe hasa unapoviangalia viwango hivyo na kuvifananisha na vilivyopita.
Kwa mfano takwimu za Fifa za mwezi Septemba, zilionyesha kwamba Tanzania ilikuwa ya 115 na takwimu zilizotolewa mwezi huu zinaonyesha kwamba Tanzania sasa ni ya 110.
Wengi waliopata taarifa hizo walijifariji hasa baada ya kuona Tanzania imepiga hatua hiyo na kuizidi hata nchi ya Kenya ambayo kwa mujibu wa viwango hivyo inashika nafasi ya 116.
Tuesday, 21 October 2014
AFARIKI AKISHABIKIA MPIRA.
Mchezaji wa soka nchini India, Peter Biaksangzuala amefariki kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kuanguka vibaya uwanjani akisherehekea bao lake.
Mchezaji huyo alikuwa na umri wa miaka 23 na alijeruhi uti wake wa mgongo baada ya kupiga pindu uwanjani akisherehekea bao lake la kusawazisha kw atimu yake Bethlehem Vengthlang FC dhidi ya Chanmari West FC.
Biaksangzuala alikimbizwa hospitalini na kufanyiwa upasuaji lakini baadaye alifariki.
Mechi hiyo ambapo alipata jerehe la mgongo, ilikuwa mechi muhimu katika ligi ya nchi hiyo.
Taarifa kutoka kwa ligi hiyo kpitia kwa mtandao wa Facebook, ilisema : ''imekuwa siku yenye huzuni mkubwa kwa ligi ya Mizoram na kifo cha mchezaji wetu kimetushtua sana pamoja na wachezaji wenzake, wachezaji wa soka na mashabiki wa Mizoram. ''
"Peter alikuwa mchezaji mzuri na milizni mzuri sana, na pia alikuwa mchapa kazi.'
Thursday, 16 October 2014
TAARIFA KUTOKA TFF
Mkutano Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) utafanyika Novemba 15 mwaka huu jijini Dar es Salaam ambapo moja ya ajenda ni uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi moja ya uongozi kwenye bodi hiyo.
Nafasi hiyo ya ujumbe kwenye Kamati ya Uendeshaji ya TPLB iliyokuwa ikishikiliwa na Kazimoto Muzo imebaki wazi baada ya klabu yake ya Pamba ya Mwanza kushuka daraja kutoka la Kwanza hadi la Pili.
Hivyo, wagombea wa nafasi hiyo ni kutoka kwenye klabu za Ligi Daraja la Kwanza (FDL). Klabu hizo zina nafasi mbili kwenye Kamati ya Uendeshaji ya TPLB ambapo nyingine inashikiliwa na Omari Mwindadi wa klabu ya Mwadui ya Shinyanga.
SDL WAONGEZEWA MUDA WA USAJILI
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeongeza muda wa usajili wa wachezaji kwa timu za Ligi Daraja la Pili (SDL) kwa siku saba ambapo sasa utamalizika Oktoba 21 mwaka huu.
Awali usajili huo unaofanyika kwa njia ya mtandao (online) ulikuwa umalizike jana (Oktoba 14 mwaka huu), lakini ni klabu chache ndizo zilizoweza kusajili ndani ya muda uliopangwa.
Klabu ambazo hazijakamilisha shughuli hiyo ya usajili, zinatakuwa kukamilisha ndani ya siku hizo saba kwani TFF haitaongeza tena muda wa usajili. Vilevile klabu za SDL zinakumbushwa kuwasilisha majina ya viwanja vya nyumbani ambavyo timu zao zitatumia kwenye ligi hiyo.
TFF ilifanya mafunzo ya usajili kwa maofisa usajili wa klabu hizo Oktoba 6 na 7 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Timu za SDL zimegawanywa katika makundi manne ya timu sita zitakazocheza ligi kwa mtindo wa nyumbani na ugenini. Kundi A lina timu za Mpanda United ya Katavi, Ujenzi (Rukwa), Mvuvumwa FC (Kigoma), Mji Mkuu FC (Dodoma), Milambo (Tabora) na Singida United (Singida).
Kundi B ni Mbao FC (Mwanza), Bulyanhulu FC (Shinyanga), Eleven Stars (Kagera), JKT Rwamkoma (Mara), Pamba (Mwanza) na AFC (Arusha). Kundi C ni Navy, Mshikamano, Transit Camp na Abajalo za Dar es Salaam, Kiluvya United (Pwani) na Kariakoo (Lindi(.
Timu zinazounda kundi D ni Magereza (Iringa), Town Small Boys (Ruvuma), Njombe Mji (Njombe), Volcano FC (Morogoro), Wenda FC (Mbeya) na Mkamba Rangers (Morogoro).
MAREKEBISHO YA RATIBA FDL KUNDI A
Mechi nne za Kundi A la Ligi Daraja la Kwanza (FDL) zimefanyiwa marekebisho ili kutoa fursa ya matumizi ya Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam.
Timu za African Lyon na Kimondo FC ambazo awali zilikuwa zicheze Oktoba 25 mwaka huu kwenye Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani, sasa zitacheza Oktoba 26 mwaka huu Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Nayo mechi ya Polisi Dar es Salaam na Majimaji ya Songea iliyokuwa ichezwe Oktoba 26 mwaka huu Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, sasa itachezwa Oktoba 27 mwaka huu kwenye uwanja huo huo.
Mechi ya Friends Rangers na Ashanti United iliyokuwa ichezwe Mabatini mkoani Pwani, Oktoba 26 mwaka huu, sasa itachezwa Uwanja wa Karume, Oktoba 28 mwaka huu.
Pia mechi ya Lipuli FC na JKT Mlale iliyokuwa ichezwe Oktoba 25 mwaka huu kwenye Uwanja wa Samora mjini Iringa, imesogezwa mbele kwa siku moja. Mechi hiyo sasa itachezwa Oktoba 26 mwaka huu kwenye uwanja huo huo.
Mabondia wazichapa Nyerere day
MABONDIA KUZICHAPA SIKU YA NYERERE DAY
Bondia Suma Ninja akitunishiana misuli na Shomali Mirundi baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika katika ukumbi wa Musoma Bar Tandika Maguluwe siku ya Nyerere Day Picha na SUPER D
Bondia
Azizi Abdalla akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake utakaofanyika
siku ya nyerere Day Oktoba 14 katika ukumbi wa musoma bar tandika
maguluwe kulia ni mpinzani wake Azizi Rashid Picha na SUPER D
Bondia Imani Daudi 'Imana Mapambano' kushoto akitunishiana misuli na Ally Sufiani baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika siku ya Nyerere Day katika ukumbi wa Musoma Bar Tandika Maguluwe
Bondia Suma Ninja akitunishiana misuli na Shomali Mirundi baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika katika ukumbi wa Musoma Bar Tandika Maguluwe siku ya Nyerere Day
Mabondia Azizi Abdalla na Azizi Rashid wakitunishiana misuli baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika siku ya Nyerere Day katika ukumbi wa musoma bar tandika maguluwe
Bondia Imani Daudi 'Imana Mapambano' kushoto akitunishiana misuli na Ally Sufiani baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika siku ya Nyerere Day katika ukumbi wa Musoma Bar Tandika Maguluwe katikati ni Rais wa TPBO Yassin Abdallah Picha na SUPER D BLOG
Na waandishi Wetu
MABONDIA Imani Daudi 'Imani wa Mapambano' na Ally Sufiani wamepima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa raundi nane utakaofanyika katika ukumbi wa musoma bar tandika maguluwe
Akizungumza na wahandishi wa habari wakati wa zoezi la upimaji uzito Promota Kelvin Mapunda amesema mbali na mpambano huo kutakuwa na mapambano mengine mbalimbali ambapo bondia Suma Ninja atavaana na Shomari Mirundi na Azizi Abdallah atapambana na Azizi Rashidi
Ngumi hizo zilizopangwa kufanyika oktoba 14 siku ya kumbukumbu ya kufanyiki baba wa taifa zitakuwa chachu ya kufufua mchezo wa masumbwi katika kitongoji cha tandika na maeneo ya jirani
Tuesday, 14 October 2014
KIINGILIO MECHI YA SIMBA NA YANGA
HIKI NDICHO KIINGILIO MECHI ZA SIMBA NA YANGA.
Published in
Michezo
Geilson Santana ‘Jaja’ akishangilia goli na wachezaji wenzake.
Kiingilio
cha chini kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga na
Simba itakayochezwa Jumamosi (Oktoba 18 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam ni sh. 7,000.
Mshambuliaji wa Simba Emmanuel Okwi akishangilia.
Washabiki
watakaolipa kiingilio hicho ni wale watakaokaa viti vya rangi ya bluu
na kijani ambavyo jumla yake ni 36,693 katika uwanja huo wenye viti
57,558. Viingilio vingine ni sh. 10,000 kwa viti vya rangi ya chungwa,
sh. 20,000 kwa VIP B na C wakati VIP A itakuwa sh. 30,000.
Tiketi
zitakazotumika kwenye mechi hiyo ni za elektroniki, na zimeanza kuuzwa
jana (Oktoba 13 mwaka huu). Tiketi zinapatikana kwa mtandao wa M-PESA,
CRDB Simbanking na maduka ya CRDB Fahari Huduma ambayo yapo zaidi ya mia
moja sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam.KWATA LA WAHESHIMIWA
WAHESHIMIWA WAKIPIGA JERAMBA UWANJANI

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera na Mkuu wa Mkoa wa Dsm Meck Sadick;wakionyesha ufundi wa hali ya juu wa kuuchezea mpira
Subscribe to:
Posts (Atom)








