Followers

VIDEO: B.O.B N' MICHARAZO - KAZI KWANZA

Hatari nyingine town kutoka kwa B.O.B MICHARAZO 'kazi kwanza'

.

TZEE MODAL APATA DILI SOUTH AFRICA

Calisah amepata shavu kutoka kampuni moja ijulikanayo kama Ice Model ambayo inadeal modelling...

VIDEO: NEY WA MITEGO - SINA MUDA

Audio from Free Nation / Mr. T - Touch, Video Production : Joowzey

VIDEO: MESEN SELEKTA - SWEET LOVE

Music video by Mesen Selekta performing 'Sweet love'. Video directed by Ivan (Shine Studioz).

VIDEO: RABIT KING KAKA FT RICH MAVOKO - NJOO

Video mpya kutoka kwa Rabbit King Kaka featuring Rich Mavoko. iitwayo 'Njoo'.

Showing posts with label KIMATAIFA. Show all posts
Showing posts with label KIMATAIFA. Show all posts

Monday, 13 April 2015

GWAJIA KUKISIWA KUWA NI MCHUNGAJI TAJIRI AFRIKA: MALI ZAKE ZAWEKWA WAZI



Sakata la Gwajima limechukua sura mpya baada ya mchungaji huyo kutakiwa na jeshi la polisi kupeleka nyaraka mbalimbali zinazohusu umiliki wa mali zake!
Mchungaji Gwajima katika kupingana na amri hiyo halali ya jeshi la polisi, amekimbilia kwa mawakili, ili tu kuweka pingamizi la yeye kuthibitisha umiliki wake wa mali alizonazo na namna alivyozipata.
Itakumbukwa kuwa jeshi la polisi lilimtaka Gwajima apeleke nyaraka zifuatazo: Hati ya usajili wa kanisa lake, namba ya usajili wa kanisa lake, hati ya umiliki wa helikopta, hati za

HII NDIYO AJALI MBAYA YA GARI LILILOUNGUA MOTO NAKUTEKETEZA WATU 18 LEO


Watu 18 wamekufa papo hapo kwa kuteketea kwa moto na wengine 11 wamejeruhiwa vibaya kutokana na basi walilokuwa wakisafiria kugongana na lori aina ya Mitsubishi Fuso, katika kijiji cha Msimba tarafa ya Mikumi, barabara kuu ya Morogoro – Mbeya.

Ajali hiyo imehusisha basi la Kampuni ya Nganga linalofanya safari zake kutoka Wilaya ya Kilombero kuelekea mkoani Mbeya na kugongana na lori hilo.

Tuesday, 28 October 2014

JE WAJUA KILICHOMFANYA DOMINICA KURUKA UKUTA WA IKULU MAREKANI SOMA HII

 http://i1.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2014/10/White-House-jumper-jpg.jpg

 

Adesanya

Habari zinasema hii si mara ya kwanza kwa Mnigeria Dominica Adesanya (23) kuruka ukuta wa White House, na safari hii baada ya kumfikisha mahakamani imebainika kuwa ana tatizo la akili hivyo hawezi kushitakiwa akiwa na hali hiyo.

Daily Mail imeripoti kuwa baada ya mahakama kuthibitisha vipimo kutoka hospitali kuwa ana tatizo hilo, mahakama iliamuru awekwe chini ya ulinzi huku akipata matibabu ya ugonjwa huo mpaka Desemba 22 kesi yake itakapotajwa tena mahakamani hapo.

Adesanya ametolewa mahakamani hapo akipiga kelele za kuomba msaada huku akilaumu kitendo cha kukamatwa kwake.

Hii ni mara ya pili kwa Mnigeria huyo kuruka ukuta wa White House, ambapo mara ya kwanza Adesanya ambaye ana asili ya Nigeria kufanya hivyo ilikuwa Julai 27 majira ya saa 4 usiku mwaka huu, na kurudia tena Oktoba 23 majira ya saa 1 jioni.


UKIMWI,EBOLA VIMETENGENEZWA MAKUSUDI KUPUNGUZA IDADI YA WATU

                                                                                                                          

WAKATI DUNIA nzima ikizidi kujawa na hofu inayotokana na milipuko ya magonjwa, machafuko ya kivita, maandamano ya watu kudai mabadiliko, kuporomoka kwa maadili; majaribio ya chanjo ya ugonjwa wa Ebola yanatarajiwa kuanza kufanyika mwezi wa kwanza mwakani. Taarifa zilizotolewa na gazeti la ‘The Telegraph News’ la tarehe 22/10/2014 zinasema kwamba kampuni ya kutengeneza madawa ya Johnson & Johnson ya Marekani ndiyo iliyotengeneza chanjo hiyo ambayo inadaiwa kufanyiwa majaribio kwa wanyama na kuonyesha mafanikio makubwa. Majaribio hayo ya chanjo hiyo yatafanyika Amerika, Afrika na Ulaya.
Hii inamaanisha kwamba tatizo la Ebola limepewa muda mrefu zaidi hadi kufika mwezi Januari ili kuendeleza kukuza hofu kwa watu na kuwaandaa kwa ajili ya kukimbilia chanjo kwa haraka!
Ni kanuni gani wanayoitumia? ni kanuni ya kwanza inayosema ‘Thesis x Antithesis = Synthesis’. Wao (freemasons) wanasema: "Manufacture the crisis, then panic the people, and then step in with the solution you wanted in the first place" wakimaanisha “Tengeneza mgogoro, kisha wafanye watu wapate hofu, na kisha chukua hatua ya suluhisho ambalo ulilitaka kabla ya kutengeneza mgogoro’. Hapa mgogoro au ‘Thesis’ ni Ebola na kutokana na mgogoro huu watu wanapata ‘hofu’ ambapo suluhisho linapotolewa, yaani chanjo au ‘Antithesi’, watu wengi watakimbilia chanjo hiyo. Nini matokeo yake? Ni ‘Synthesis’ yaani kutekelezwa kwa ajenda za freemasons ambapo isingekuwa rahisi kutekelezwa kama pasingekuwepo mgogoro! Ni suluhisho gani? Kupunguza idadi ya watu duniani!
Kutokana na ukweli kwamba makao makuu ya dini ya freemasons yapo nchini Marekani, matatizo (crises) hutengengezwa Marekani ikiwa ni pamoja na suluhisho (solution) la matatizo hayo. Karibu kila tatizo kubwa linaloukumba ulimwengu wote, liwe la kiafya, kisiasa, kiuchumi au kidini, chanzo chake ni Marekani. Matatizo haya yanatengenezwa kwa lengo la kuonekana hitaji la kuanzishwa kwa serikali moja ya dunia inayodaiwa kuwa suluhisho la majanga yanayoukumba ulimwengu.
Ili kukuza matatizo, mpango unaoitwa ‘PEACE plan’ yaani mpango wa amani’ ulianzishwa. Kumbuka kwamba kila wakati mpango wowote unapoanzishwa na wafuasi wa dini ya freemasons, huweka maana mbili, moja iliyowazi, yaani ‘Exoteric meaning’ na maana nyingine ni ‘Esoteric meaning’ yaani maana iliyofichika. Kwa maana iliyowazi, PEACE Plan ni mpango mzuri wenye lengo la kuleta amani na mshikamano duniani. Lakini katika maana iliyofichika, kila herufi kwenye neno PEACE ilikuwa na maana yake. Herufi ‘P’ inasimamia lengo la ‘Plant Churches’ and Promote reconciliation’ yaani kupandikiza makanisa na kuleta mapatano. Hapa tunaona kuibuka kwa makanisa mengi katika kila kona ya dunia ambapo wengi wa waanzilishi wa makanisa hayo hupata fedha kutoka kwa wafadhili ili kutekeleza, siyo matakwa ya Mungu, bali matakwa ya wafadhili. Herufi ‘E’ ni ‘Equip servant leaders’(yaani kuweka viongozi katika serikali ambao watakuwa siyo watumishi wa wananchi bali watumishi wa wafadhili. Herufi ‘A’ ‘Assist the poor’ (kuwasaidia maskini) kama ambavyo tunaona misaada mbalimbali ikitolewa na mashirika ya kimataifa yenye lengo maalumu ndani yake; herufi ‘C’ inasimamia Care for the sick (yaani kuwajali wagonjwa ili kupunguza vifo vya watoto, kupambana na Ebola, surua, ukimwi nk) na hapa tunaona rais Obama akichukua muda mrefu kurekebisha sheria ya huduma za afya ‘health reform’ kama inavyojulikana kwa jina la  Obamacare kule Marekani, lakini lengo siyo kusaidia wagonjwa bali kusaidia kukuza ugonjwa; herufi ‘E’ Educate the next generation (kuwawezesha wanawake na usawa wa jinsia, elimu ya msingi kwa wote, na utunzaji wa mazingira) kwa ajili ya maendeleo ya kizazi kijacho. Neno PEACE linamaanisha AMANI na hakuna mtu asiyependa amani lakini neno hilo limetumiwa kama kiini macho cha kuwafanya watu wakubali mpango wa amani bila kujua lengo la mpango huo. Biblia inatuambia kwamba “Wakati wasemapo, Kuna amani (PEACE) na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafla…” 1 Wathes. 5:3.
Tayari rais Barack Obama amemteua Ron Klain kuongoza mapambano dhidi ya Ebola duniani. Hata hivyo Ron Klain ni mtu ambaye amekuwa akiona ongezeko la watu duniani kuwa ni tatizo kubwa kwa serikali za dunia. Yeye aliwahi kusema: “I think the top leadership challenge issue in our world today is how to deal with the continuing, growing population in the world and all the resource demands it places on the world and burgeoning populations in Africa and Asia that lack the resources to have a healthy, happy life,” akimaanisha kwamba ‘Nadhani changamoto kubwa ya uongozi katika ulimwengu wetu leo ni jinsi ya kutatua ongezeko la watu ulimwenguni pamoja na mahitaji yaliyopo ulimwenguni na ongezeko la watu huko Afrika na Asia linalosababisha upungufu wa mahitaji yanayotakiwa kwa afya nzuri na maisha yenye furaha’. Kwa nini Rais Obama amemteua Ron Klain kuongoza mapambano dhidi ya Ebola?  Ron Klain hakuchaguliwa kupambana na ugonjwa wa Ebola bali kupambana na ongezeko la watu ulimwenguni ambapo moja ya silaha za kufanikisha kupunguza idadi ya watu ni kutumia Ebola. Hebu tujikumbushe kile walicholenga Illuminati katika ajenda zao juu ya ongezeko la watu duniani: "Take control of the world ... to reduce ... the world to a safe level by a process of benevolent slavery and genocide ... The only alternative left to the world's ruling elite was to increase the death rate ... Dr. Aurelio Peccei of the Club of Rome ... advocated that a plague be introduced that would have the same effect as the Black Death of history." (Bill Cooper, “Behold a Pale Horse”, p. 49, 167). Bill Cooper mwandishi wa kitabu cha Behold a Pale Horse anasema kwamba idadi ya watu duniani inapaswa kuwa sawa na uwiano wa kile kinachozalishwa. Njia pekee ya kupunguza idadi ya watu ni kuongeza kasi ya vifo ambapo Dk. Aurelio Poccei wa kundi la Club of Rome aliagiza kwamba ugonjwa hatari utengenezwe ambao utakuwa na madhara sawa na janga lililojulikana kama ‘Black Death’ katika historia. Hivyo basi njia pekee ni kuongeza kasi ya vifo kuliko kasi ya kuzaliwa, (increase death rate vs birth rate). Kule China sheria inawataka wanandoa kuzaa si zaidi ya watoto wawili ili kupambana na ongezeko la watu. Hata hivyo inadaiwa kwamba kuna ongezeko kubwa la vifo ukilinganisha na ongezeko la watu kumaanisha kwamba idadi ya watu inazidi kupungua!
Sasa tujiulize swali muhimu: Je, chanjo imewahi kutumiwa kama silaha ya kupunguza idadi ya watu? Jibu la haraka ni ndiyo! Dk. Horowitz anazungumzia jambo hili katika kitabu chake alichokiita “Emerging Viruses: AIDS and Ebola.” Dk. Horowitz anatumia karibu kurasa 600 kuthibitisha kwamba Marekani kwa makusudi ilitengeneza virus vya AIDS kama silaha kisha wakaanza kuwasambaza virus hao barani Afrika kupitia chanjo zilizotolewa bure katika mpango unaojulikana kama ‘United Nations Vaccination campaign’ yaani ‘kampeni ya chanjo ya umoja wa mataifa’. Dk. Horowitz anasema yeye akiwa ni daktari mzoefu ameandika kitabu hicho akiwa anafahamu ukweli aliouandika. Hebu tumnukuu akiandika kwenye kitabu chake “Emerging Viruses: AIDS and Ebola” na hapa anasema: “Suala la kwanza lililoelezewa na Strecker ni kwamba AIDS haukuwepo Afrika kabla ya mwaka 1975, na kama ugonjwa huo ungetokana na kung’atwa na sokwe miaka ya 1940 kama inavyoelezewa, ugonjwa huo ungeonekana miaka ya 1960 na siyo miaka ya 1970. Kisha Dk. Horowitz anasema: "The World Health Organization started to inject AIDS-laced smallpox vaccine into over 100 million Africans (population reduction) in 1977. And over 2000 young white male homosexuals (Trojan horse) in 1978 with the hepatitis B vaccine through the Centers For Disease Control/New York Blood Center." [Horowitz, p. 4-5], akimaanisha kwamba ‘Shirika la afya ulimwenguni lilianza kuingiza wadudu wa AIDS kupitia chanjo ya surua kwa waafirika wapatao milioni 100 (kwa lengo la kupunguza idadi ya watu) mwaka 1977. Zaidi ya vijana wavulana 2000 wa kizungu ambao walikuwa mashoga walipewa chanjo ya hepatitis B mwaka 1978 kupitia kitengo cha kuzuia magonjwa huko New York” [rejea Horowitz: “Emerging Viruses: AIDS and Ebola” p. 4-5].
Mei 11, 1987, gazeti la London Times liliandika makala iliyoitwa “Smallpox Vaccine ‘Triggered AIDS Virus’,”  iliyoandikwa na Pearce Wright aliyekuwa mhariri wa gazeti hilo ambaye aliihusisha chanjo hiyo na mlipuko wa ugonjwa wa AIDS huko Afrika ya kati kwa sababu ndilo eneo lililokusudiwa kuanzisha ugonjwa wa AIDS na likawa eneo lililoathirika zaidi na ugonjwa huo kwa kipindi hicho. Hapa madaktari wetu wanapaswa kutusaidia kufanya uchunguzi wa kila chanjo inayoingizwa nchini kama ni salama au italeta madhara siku za usoni. Madaktari mpo?
Mwinjilist mmoja anayehubiri kwa njia ya Redio, bw. R.G. Stair, alipokea barua kutoka kwa mwanasayansi ya Bailojia (ambaye hakutaka kutaja jina lake maana alituma barua hiyo kwa siri ili mwinjilisti huyo awaambie watu). Mwandishi wa barua hiyo alisema anafanya kazi kwenye maabara pamoja na Dr. Robert C. Gallo ambaye ni mtaalamu wa bailojia ya ‘molecules’ aliyehusika katika utafiti wa asili ya virus vya AIDS. Mwandishi alisema kwamba Dr. Gallo ndiye aliyetengeneza virus vya AIDS na kuviingiza kwenye chanjo kwa nia ya kuambukiza watu. Mwandishi huyo alisema kwamba aligundua hilo alipotembelea ofisi ya Dr. Gallo na kuona barua nyingi zilizoandikwa ‘New World Order’. Kwa nini tunapata habari hizi zilizokusudiwa kuwa siri? Ndiyo! Yesu alisema: “Hakuna neno lililositirika ambalo halitafunuliwa; wala lililofichwa ambalo halitajulikana.” [Rejea Matthayo 10:26,27]; na huu ni utimilifu wa maneno hayo ya Yesu, ili kwamba tupate kujua siri za freemasons zilizokusudiwa kutuangamiza.
Mwaka 1975, Dr. Gallo pamoja na wanasayansi wengine wanane (wakiwa wanafanya kazi kwenye kituo cha utafiti wa ugonjwa wa kansa – Bethesda Cancer Research Center – huko Maryland Marekani, walifanya utafiti wa kuvifanya virus vya AIDS viweze kuambukizwa kirahisi zaidi kwa binadamu ambapo badala ya chanjo waliwezesha AIDS kuambukizwa kwa njia ya ngono kwa sababu watu wengi wanaendekeza tabia hiyo kinyume na sheria ya Mungu. Je ni wewe? Tafakari!
Mwaka huo huo, baada ya kituo cha kijeshi cha afya kiitwacho ‘Fort Detrick’ kufungwa, kilianzishwa kituo kipya kilichopewa jina la ‘Fredrick Cancer Research Facility’ kikiwa chini ya kituo cha ‘Bathesda Cancer Research Center’, ambapo Dr. Gallo alikuwa ndiye mkurugenzi wa kituo hicho. Utafiti uliofanyika mwezi Machi mwaka 1976 ulionyesha kwamba kulikuwa na kitengo cha serikali kilichokuwa kinazalisha virus vya AIDS, na kitengo hicho kilisimamiwa na Dr. Gallo pamoja na Dr. Novakhatskiy wa kituo cha ‘Ivanosku Institute’ nchini Urusi. Baadaye Dr. Gallo alipatikana na hatia katika taaluma yake lakini Rais Bill Clinton alitoa msamaha, na hivyo Dr. Gallo akawa huru.
Akijibu swali kwamba virus vya AIDS vilitengenezwa kama silaha ya kibaolojia, mwezi February, 1987, Kanali wa jeshi la Marekani David Huxsoll alisema: “Studies at army laboratories have shown that the AIDS virus would be an extremely poor biological warfare agent.” Kwamba “utafiti katika maabara za kijeshi umeonyesha kwamba virus vya AIDS ni silaha hafifu ya kibaolojia vitani.” Sasa nini kilihitajika? Bila shaka ni kutengeneza silaha nyingine ya kibaolojia ambapo Ebola ilionekana kuwa silaha yenye nguvu zaidi kwa sababu Ebola inaambukiza kirahisi zaidi kuliko AIDS!
Hebu tutulie kidogo hapa na tutafakari kile tulichokiona hadi sasa. Kwanza wanasema Marekani iliingiza mwilini AIDS kwa njia ya ‘chanjo zilizotolewa bure mwaka 1977!’ Hii inamaanisha kwamba baadhi ya chanjo za ugonjwa wa ‘small pox’ zimekuwa zikitumika kupunguza idadi ya watu wasio na hatia!
William Cooper anasema: “Whatever causes AIDS was in the Vaccine.” [rejea ‘Behold a Pale Horse’ p. 168]. Hapo anamaanisha kwamba ‘chochote kilichosababisha ugonjwa wa AIDS kilikuwa ndani ya chanjo’! Je, umepata ufunuo huo? Tafakari!
Nakushauri ndugu msomaji ujipatie nakala ya vitabu hivi viwili, “Emerging Viruses: AIDS and Ebola” cha Dk. Horowitz na “Behold a Pale Horse” cha William Cooper.
Wakati tunaelekea kuanza kuiangalia ajenda ya 36, tujikumbushe kwa ufupi ajenda ya 35 inayohusu kuanzishwa kwa serikali ya dunia katika vipengele vitano. Vipengele hivyo ni ‘A king’ yaani Mfalme, ambapo kutakuwepo na mfalme mmoja atakayetawala dunia nzima; ‘A kingdom’ yaani Ufalme ambao utakuwa umeugawa ulimwengu katika majimbo 10; ‘A seat of Kingdom’ yaani kiti cha ufalme kitakachowekwa mahali patakapokuwa makao makuu au ikulu ya serikali ya dunia; ‘A council’ yaani baraza ambapo tuliona muundo wa baraza hili ukiwa katika umbo la pembe tatu huku kukiwa na vitengo vingi vinavyofanya kazi za baraza kuu la ‘Supreme council of 13’ na mwisho tumetazama kipengele cha ‘constitution’ yaani ‘katiba’ ya serikali ya ulimwengu. Kwa ufupi hiyo ndiyo ajenda ya 35. Na sasa kuwa tayari kwa ajili ya ajenda ya 36 inayohitimisha ajenda zote za freemasons.
Usiondoke…..Itaendelea wiki ijayo
Makosa – makosa ndani ya mioyo ya watu – huchafua hisia za watu.
Kweli  –  kweli ndani ya mioyo ya watu   – hutakasa nafsi.
Mungu ni Mwema!
tafakari2010@yahoo.com

                                 Tazama news papers

Thursday, 23 October 2014

MTOTO AKUTWA NA EBOLA HII NCHI SOMA HAPA.

Ebola BillboardSerikali ya Mali imethibitisha kuhusiana na taarifa za mtoto wa miaka 2 kukutwa na maambukizi ya Ebola akiwa ni mtu wa kwanza kupata maambukizi ya ugonjwa huo nchini humo tangu ugonjwa huo ulipozuka mwezi Machi 2014.

Taarifa kutoka mtandao wa the World Post zimesema, mtoto huyo amegundulika kuwa na maambukizi ya ugonjwa huo aliporejea nchini humo akitokea Guinea, moja ya nchi zilizoathiriwa zaidi na Ebola Afrika Magharibi.

Mali inakuwa nchi ya sita kutangaza kupatikana mgonjwa mwenye maambukizi ya Ebola katika ukanda wa Afrika Magharibi, lakini ndani ya siku 7 nchi za Senegal na Nigeria zimetangaza kutokuwa na mgonjwa mwenye maambukizi ya Ebola.

Ripoti iliyotolewa na WHO imeonesha vifo zaidi ya 4,900 vimetokea katika nchi za Sierra Leone, Guinea na Liberia.

Timu ya wanasayansi wa kimataifa imejipanga kutafiti uwezekano wa kutumia damu ya mtu aliyewahi kupona Ebola kama tiba ya ugonjwa huo.

Mali inapakana na nchi ya Guinea kwa upande wa Kusini Magharibi, lakini mtoto huyo anakuwa mgonjwa wa kwanza kuripotiwa kuwa na maambukizi ya Ebola nchini humo.

Tuesday, 21 October 2014

SOMA HII KUHUSIANA NA DAWA YA EBOLA

Watafiti na dawa ya Ebola, A.Magharibi

 
Kampeni ya Ebola

Shirika la afya ulimwenguni WHO limesema dawa ya Ebola ambayo imetengenezwa kwa mchanganyiko na damu ya watu waliambukizwa na kisha kupona ugonjwa wa Ebola inatarajiwa kuanza kupatikana wiki chache zijazo huko Afrika Magharibi.

Afisa mwandamizi wa W.H.O. Dr Marie Paule Kieny amesema vifaa vimetolewa Liberia kwaajili ya kupata damu na vifaa vya kufanyia utafiti huo wa dawa ili kupata dawa Serum.

Dr Kieny akizungumza mjini Geneva amesema kuwa kazi ya mapambano dhidi ya Ebola harakati za upatikanaji chanjo ya ugonjwa huo .

Maelfu ya watu wanatarajiwa kutumiwa katika majaribio hayo yanayolenga kupatikana kwa chanjo na dawa ya ugonjwa huo.

AFARIKI AKISHABIKIA MPIRA.

Mchezaji wa soka nchini India, Peter Biaksangzuala amefariki kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kuanguka vibaya uwanjani akisherehekea bao lake.

Mchezaji huyo alikuwa na umri wa miaka 23 na alijeruhi uti wake wa mgongo baada ya kupiga pindu uwanjani akisherehekea bao lake la kusawazisha kw atimu yake Bethlehem Vengthlang FC dhidi ya Chanmari West FC.

Biaksangzuala alikimbizwa hospitalini na kufanyiwa upasuaji lakini baadaye alifariki.

Mechi hiyo ambapo alipata jerehe la mgongo, ilikuwa mechi muhimu katika ligi ya nchi hiyo.

Taarifa kutoka kwa ligi hiyo kpitia kwa mtandao wa Facebook, ilisema : ''imekuwa siku yenye huzuni mkubwa kwa ligi ya Mizoram na kifo cha mchezaji wetu kimetushtua sana pamoja na wachezaji wenzake, wachezaji wa soka na mashabiki wa Mizoram. ''

"Peter alikuwa mchezaji mzuri na milizni mzuri sana, na pia alikuwa mchapa kazi.'

HII HAPA MPYA KUTOKANA NA CHANJO YA EBOLA.

Ebola NewShirika la afya duniani, WHO limearifu kuwa liko mbioni kufanya majaribio ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa Ebola, ambao umeripotiwa kuua takribani watu 4,500 huku nchi za Afrika Magharibi zikiripotiwa kuathirika zaidi tangu kulipuka kwa ugonjwa huo.

Taarifa iliyoripotiwa na CNN imesema kuwa shirika hilo limepanga kuanza utekelezaji wa jaribio hilo mapema Januari mwaka 2015 katika nchi za Afrika Magharibi, huku wakisisitiza kuwa chanjo zote hazina madhara kwa afya ya binadamu, japo chanjo hiyo haitowahusu wagonjwa ambao tayari wana maambukizi Ebola.

Mratibu wa zoezi hilo Dk. Marie Paule Kieny amesema, chanjo hiyo itatolewa kwa mtu yoyote atakayekuwa tayari kujitolea kushiriki.

Amezitaja nchi za Mali, Uingereza na Marekani kuwa ni baadhi ya nchi ambazo jaribio la chanjo hiyo litafanyika.

Shirika la afya limesema limeagiza wataalamu kufanya ziara Afrika Magharibi katika nchi ambazo wananchi wake wameathirika zaidi na ugonjwa huo, ambapo pia ziara hiyo itahusisha pia zoezi la ukaguzi wa vituo ambavyo vitatumika kutolea huduma hiyo ya chanjo.

Iwapo chanjo hii itafanikiwa itafufua matumaini kwa watu wa Afrika ya Magharibi ambao wameshuhudia athari kubwa zilizosababishwa na Ebola ambapo watu zaidi ya 4,500 wameripotiwa kufariki na wengine zaidi ya 9,000 wana maambukizi ya ugonjwa huo.

HII HAPA HUKUMU YAOSCAR PISTORIOUS

MIAKA 5 JELA.

 

Pistorius alipatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake bila kukusudia

Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius amehukumiwa jela miaka 5 baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mpenziwe Reeva Steenkamp.

Hii ni baada ya mwanariadha huyo mlemavu kupatikana na hatia ya kumuua mpenziwe Reeva Steenkamp mwaka uliopita bila ya kukusudia.

Jaji aliyetoa hukumu hiyo,Thokozile Masipa,alianza kutoa kauli yake ya mwisho kabla ya kutoa hukumu saa mbili na nusu asubuhi na akasema ni changamoto kubwa kwake kupata adhabu ambayo itaridhisha pande zote kwenye kesi hiyo.

Upande wa mashitaka ulitaka mwanariadha huyo kupewa kifungo cha miaka 10 gerezani baada ya kupatikana na makosa ya kuua bila kukusudia.

Pistorius alisema kuwa alifyatua risasi baada ya kudhani kuwa jambazi alikuwa amevamia nyumba yake.

Upande wa mashitaka unasisitiza afungwe jela wakati wakili wa Pistorius wakimtaka jaji ampe kifgungo cha nyumbani cha miaka mitatu na pia apewe usaidizi na ushauri wa kubadili tabia yake. HABARI BBC

Friday, 17 October 2014

HATUTAKUBALI MATOKEO YA URAIS-RENAMO

CHAMA CHA RENAMO CHATOA MAONI KUHUSU MATOKEO YA URAIS.


Alfonso Dlakama

Chama cha kikuu cha upinzani nchini Msumbiji cha RENAMO,kimetoa yake ya moyoni kuwa hawatayakubali matokeo yajayo ya uraisi na ubunge pamoja na serikali za mitaa.

Msemaji wa chama hicho Antonio Muchanga amesema kwamba kumekuwa na ukiukwaji wa taratibu katika upigaji kura huo na udanganyifu wa kura.

Matokeo ya awali katika uchaguzi huo zinaonesha kwamba chama cha FRELIMO kinaongoza katika uchaguzi huo.Wakati haya yakitokea kumekuwa na uvunjifu wa amani wakati polisi walipo ingia katika ghasia na waandamanaji waliokusanyika nje ya vituo vya kupigia kura kufuatilia zoezi la uhesabuji wa kura .

Ingawa wafuatiliaji wa uchaguzi nchini Zimbabwe wanaeleza kuwa pamoja na yote hayo,uchaguzi huo ulikua huru na wa haki.ikumbukwe kuwa chama cha Renamo na chas Frelimo walipigana vita ya wenyewe kwa wenyewe vilivyomalizika mnamo mwaka 1982.BBC

Thursday, 16 October 2014

Grace Mugabe: Matebeleland Uvivu na Ngono

Grace Mugabe Atoa tamko zito Matebeleland

  • Posted by mbalamwezi forum 
  • Habari BBC

Dr Grace Mugabe na Mumewe Rais Robert

Mke wa Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe Grace Mugabe siku hizi ni dokta, cheo kilichozua mtafaruku nchini mwake akikinzwa katika udaktari wake wa masuala ya sosholojia alioupatia katika chuo kikuu cha nchi hiyo, amewatemea cheche wanaume wa eneo la Matabeleland nchini humo kuwa ni hodari wa kuoa wake wengi kila uchao na kuwazalisha watoto na kushindwa kuendeleza makazi yao .

Dokta Mugabe aliyasema hayo katika mkutano wa hadhara unaokisiwa kuhudhuriwa na watu wapatao elfu nne katika viwanja vya Gwanda mapema wiki hii. Dokta Mugabe amewashangaa wanaume hao kutoka kabila la Ndebele kwa kuwa maarufu wa kuzalisha na kuwatelekeza watoto bila matunzo yoyote huku wakiendekeza ngono Zaidi.BBC

Dr Grace anasema ni jambo la kawaida kumkuta mwanamume ana wake watano hadi kumi na kuuita ni upuuzi mkubwa.

Pmaoja na hayo ,Dr Mugabe amewashutumu pia wanaume hao wa Matabele kusini kwa kushindwa kufanya maendeleo yao binafsi na badala yake mawazo yao ni kusafiri kuelekea Africa Kusini hasa katika jiji la Johannesburg kufanya kazi za nyumbani.

Hii ni mara ya pili katika kipindi cha miaka miwili familia ya Mugabe kuwakosoa wanaume wa Matebele hadharani kwa kukimbilia Africa Kusini kuajiriwa kama watumishi wa ndani.

Mara ya kwanza alikua ni Rais Mugabe aliyezua mjadala mkali kutoka kwa watu wa Matebele, ambapo alitoa kauli kama za mkewe katika eneo hilo hilo mwaka wa jana.Dr Grace Mugabe pia amewashutumu wanaume wa eneo hilo kwa ubakaji na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake.

Pamoja na kuwatemea cheche hizo Dokta Grace Mugabe alishangazwa na umati mkubwa uliojitokeza kumlaki katika mkutano huo , huku wakimpigia makofi mazito,akiwemo waziri wa michezo na utamaduni Andrew Langa,mwenyekiti wa ZANU PF Simon Khaya Moyo na waziri Abdenico Ncube