CHAMA CHA RENAMO CHATOA MAONI KUHUSU MATOKEO YA URAIS.
Alfonso Dlakama
Chama cha
kikuu cha upinzani nchini Msumbiji cha RENAMO,kimetoa yake ya moyoni
kuwa hawatayakubali matokeo yajayo ya uraisi na ubunge pamoja na
serikali za mitaa.
Msemaji
wa chama hicho Antonio Muchanga amesema kwamba kumekuwa na ukiukwaji wa
taratibu katika upigaji kura huo na udanganyifu wa kura.
Matokeo
ya awali katika uchaguzi huo zinaonesha kwamba chama cha FRELIMO
kinaongoza katika uchaguzi huo.Wakati haya yakitokea kumekuwa na
uvunjifu wa amani wakati polisi walipo ingia katika ghasia na
waandamanaji waliokusanyika nje ya vituo vya kupigia kura kufuatilia
zoezi la uhesabuji wa kura .
Ingawa
wafuatiliaji wa uchaguzi nchini Zimbabwe wanaeleza kuwa pamoja na yote
hayo,uchaguzi huo ulikua huru na wa haki.ikumbukwe kuwa chama cha Renamo
na chas Frelimo walipigana vita ya wenyewe kwa wenyewe vilivyomalizika
mnamo mwaka 1982.BBC
0 comments:
Post a Comment