AUNT AKANUSHA UHUSIANO WAKE NA NYALANDU.
STAA wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel, amesema hakuna ukweli wowote wa yeye kutanua na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu nchini Marekani, kwani alikutana naye ukumbini, akiwa amealikwa na blog iitwayo Vijimambo ambayo hutangaza utalii wa Tanzania nchini humo kila mwaka.GPL(P.T)
Staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel .
Alisema wakati wa safari yake hakuelewa lolote kuhusu Waziri Nyalandu na anashangazwa na yanayozungumzwa hivi sasa kwani baada ya kumsalimia walipokutana, hawakuwahi kuonana tena hadi aliporejea, kwani yeye alikuwa amepangiwa kwenye hoteli ambayo pia ndiyo ukumbi wa shughuli hiyo ulipokuwa.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza jambo.
0 comments:
Post a Comment