
Anafahamika zaidi kama Rose Ndauka ni mmoja warembo wenye mvuto
wa pekee ndani ya tasnia ya bongo movies kwa vipaji vyake vingi sana.
Licha ya kuwa na uwezo mkubwa wa kuigiza pia rose ni mwandishi na
mwongozaji wa Filamu. Akiwa ameshaigiza kwenye zaidi ya Filamu kumi na
saba (17) na kupata tuzo mbalimbali ikiwemo ya best actress in mini ziff
2011; Rose Pia ni mfanyabishara na anamiliki kampuni yake binafsi
iitwayo Ndauka Entertainment inayojihusha na mambo ya Filamu na
burudani. Rose Hupenda kusikiliza muziki, kuogelea, na kusoma vitabu
akiwa yupo nyumbani
Picha.
Filamu
Historia & familia
Historia ya Rose inaanza tarehe saba (7) mwezi wa kumi (10)
mwaka 1989. Huu ni mwaka tarehe na siku alipozaliwa. Alizaliwa hapa hapa
Tanzania na kupata elimu yake katika shule ya sekondari zanaki- Dar es
salaam alipomaliza mnamo mwaka 2008. Toka alipokuwa mdogo sana Rose
alipenda kuigiza. Na kipaji chake Kiligunduliwa na mama yake mzazi kabla
ya yeye mwenyewe kuamua kujiingiza rasmi kwenye tasnia ya Filamu
nchini.
Historia katika sanaa
Rose alionekana kwa mara ya kwanza kwenye Filamu ya
“SWAHIBA” aliyoigiza kama “Aisha” mnamo mwaka 2007. Filamu hii ilipigiwa
kura kama Filamu bora ya mwaka na kituo cha redio cha clouds FM. Baada
ya Filamu hiyo Rose aliweza kupata nafasi ya kuigiza katika Filamu
mbalimbali zikiwemo Mahabuba na na Solemba na nyota yake ilionekana sana
pale alipoigiza Filamu ya Deception na marehemu Steven Kanumba kama
mmoja wa waigizaji wakuu pamoja na Lost Adam aliyoigiza na mkali
mwingine wa bongo movies Jacob steven “JB”
Mwaka 2010 Rose Ndauka alifungua kampuni yake mwenyewe ya
“Ndauka Entertainment” na pia alipata nafasi ya kuigiza kwenye Filamu
inayohusu mauaji ya halaiki ya Rwanda iliyopewa jina la “RWANDA BAADA YA
VITA” ama (URWANDA NYUMA U’GENOCIDE) kwa kirwanda.
Mwaka huo huo chin ya kampuni yake Rose alitoa filamu mbili za “BAD GIRL” na “THE DIARY” ambazo zilifanya vizuri sana sokoni.
Mashabiki wake wanapenda kuita “Rosie” na mara nyingi amekuwa
akipata “attention” kubwa kwenye vyombo vya habari na magazeti kutokana
na mvuto wake na umbo lake zuri.
0 comments:
Post a Comment