
Akiwa mmoja wa wasanii wanaofanya vizuri sana kwenye soko La
bongo movies nchini, Jina lake halisi ni Simon Mwapagata, ila kwa
“fans” wake anafahamika kama Rado na kwa waigizaji wenzako anafahamika
zaidi kwa jina la baba Mage kutokana na mapenzi makubwa aliyonayo kwa
binti wake huyo. Ameshaigiza kwenye filamu zaidi ya kumi, na kwa sasa ni
katibu wa club ya bongo movies. Kwa upande mwingine ni msanii wa muziki
wa kizazi kipya (bongofleva) akiwa amefanya kazi na wasanii wachache
kwenye fani hiyo.
Picha
Historia & familia
Rado alizaliwa tarehe kumi na tatu (13) mwezi wa (3) huko
kasulu mkoa wa kigoma na kupata elimu yake ya awali huko huko kigoma.
Alianza kuonesha kipaji cha kuigiza toka akiwa shuleni ila alipendelea
sana kucheza mpira wa miguu na alitaka kuwa mmoja wa wachezaji wa
kimataifa lakini baadaye aliachana nao na kuamua kujikita zaidi kwenye
uigizaji
Historia ya sanaa.
Ameanza kuigiza rasmi mwaka 1999 katika maigizo ya ukimwi
huko tabora kabla ya kujiunga na jumba la dhahabu ambako nipo alipopata
umaarufu zaidi na kujiingiza kwenye upande wa filamu.
Baadhi ya filamu alizocheza ni pamoja na Ndoto yangu, I think I
hate my wife, Maduhu, Jumba bovu, Mahaba niue, Gongo la mboto, Fall in
love, Nakwenda kwa Mungu , laptop n.k.
Ni mmoja wa wasanii waliioa na anaishi na mke wake jijini Dar es salaam. Anamilki gari aina ya Altezza new model.
0 comments:
Post a Comment