
Ameshawahi kupata tuzo kama Msanii bora wa kiume toka Mnet
2011-2012, na pia ashawahi kuwa finalist katika Tuzo za Egol za afrika
kusini na kuwa mshindi wa pili, ni mwigizaji, mwandishi wa script,
muongozaji na mtayarishaji wa Filamu, pia anajulikana kama mwanzilishi
wa modern drama Tanzania.
Pamoja na mambo yote haya yeye ndiye aliyewatoa kisanii
waigizaji wakubwa na wanaotamba sasa kwenye tasnia ya bongo movies kama
Jacob Steven (JB), haji Adamu, John kalage,Rose ndauka na Vicenti
Kigosi (Ray). Ni baba wa watoto wawili na ashawahi kuzamia meli na
kwenda msumbuji kutafuta maisha kabla ya kurudi nchini na kujikita
kwenye sanaa za ya Uigizaji. Huyu si mwingine bali ni Single Mtambalike
maarufu kama “Richie” kwa wapenzi wote wa Filamu nchini na duniani kote.
Picha
Historia & familia.
Richie alizaliwa tarehe tano (5) mwezi wa kumi (October)
maeneo ya ilala jijini Dar es Salaam na kupata elimu yake ya msingi
katika shule ya msingi Mnazi mmoja jijini Dar es salaam na baadaye.
Aliweza kusoma katika shule ya sekondari Al haramain.
Kabla ya kuingia kwenye sanaa Single mtambalike alikuwa na ndoto
ya kuwa baharia wa meli ili aweze kuzamia meli na kwenda ulaya ama
Marekani kama ilivyokuwa ndoto ya vijana wengi wa miaka ya tisini.
Katika mpango huo aliweza kupata kazi kwenye idara ya bandari. Baada ya
kufanya kazi kwa muda wa kama miezi mitatu aliacha na kurudi nyumbani
ambako nako alishindwana na wazazi baada ya kuwa na tabia za ukorofi
sana na akaamua kuhamia kwa shangazi yake.
Baada ya muda alikutana na msichana mmoja aliyetoka uingereza
ambaye alifanya ndoto yake ya kuzamia meli kuwa kweli na ndipo alipoweza
pata kazi kwenye meli moja ya wagiriki na wakaondoka kuelekea msumbiji
ambako alikaa kwa muda wa mwaka miezi sita kabla ya kurudi Tanzania
Historia katika sanaa.
Baada ya kurudi Tanzania alikutana na Bishanga (mwigizaji)
ambaye alikuwa fundi wa magari kipindi hicho na baadaye walikutana na
waridi (mwigizaji) ambao ndo waliomshawishi kujiunga na sanaa. Hii
ilikuwa ni mwaka 1997.
Baada ya kujiingiza kwenye sanaa aliweza kufanya kazi mbalimbali za Filamu zikiwemo Uyoga ,Swahiba ,Kwa Heshima Ya
Penzi ,Chaguo Langu ,Tamaa Yangu,Diana ,Gentlemen ,Jesica ,Zawadi ya
Birthday ,Mtaani Kwetu ,Kimya ,Basilisa ,Unexpected Truth ,Solemba
,Lerato ,The Perfect Man ,Hazina ya Marehemu ,The Stranger ,Illegal
Sisters, Mahabuba
Nje ya sanaa, Single mtambalike ni baba wa watoto wawili, Prince
na Darlin, na pia ni mkurugenzi mtendaji wa Kampuni yake ya Bulls
Entertainment ambayo inajihusisha na marketing na promotion ya mambo
mbalimbali. Ameafanya kazi na kampuni mbalimbali na ashawahi kuwa
marketing and promotional manager wa kampuni ya chai kwenye mikoa ya
Dodoma na Singida.
Single ni ndugu wa Msanii JB na pia ameshiriki katika kuwatoa
kiugizaji wasanii wengine wakubwa kama JB, Vicenti Kigosi, Kalage,
Shija, Adam Haji, vyonne Cherry, pamoja na watu wengine maafuru kama
John Kalage, John Lisa, Fatma shemweta, Mackline mdoe na wengine wengi.
0 comments:
Post a Comment