
Jina lake halisi ni Mohamed Nurdin ila kwa mashabiki wake
anafahamika kama “Chekibudi”. Ni mmoja wa waigizaji wakongwe hapa
nchini. Alianza kama muigizaji na sasa anatengeneza, anaongoza Filamu na
pia ni mwandishi wa “script” kwa ajili yake na watu wengine. Pia ni
mshereheshaji (MC) kwenye shughuli mbalimbali za sherehe. Ni baba wa
watoto saba na mchezaji mzuri wa mpira wa mguu.
Picha
Historia ya familia.
Mohamed Nurdin alizaliwa tarehe kumi na tatu (13) mwezi wa kwanza (1) mjini Dar es Saalam katika hospitali ya ocean Road.
Alisoma na kupata elimu yake hapo hapo jijini Dar es salaam
katika shule ya msingi Ilala Kasulu na baadaye akejiunga na chuo cha
kiislamu, Markas Islamic kilichopo chang’ombe – Dar es salaam amabako
hakumaliza baada ya kuamua kutorokea Kenya mnamo mwaka 1997 kutokana na
matatizo kati yake na familia yake ambako alikaa huko kwa muda wa mwaka
mmoja na nusu kabla ya kurudi Tanzania mwaka 1999.
Baada ya kurudi alipata kazi kwenye kiwanda cha azam ambako alifanya kazi kama mfagiaji na mtu wa usafi.
Historia katika sanaa.
Safari ya chekibudi kwenye sanaa ilianzia mwaka huo huo wa
1999. Alipofukuzwa kazi toka kwenye kiwanda cha azam na kuamua kujikita
kwenye kucheza mpira wa miguu. Baada ya mechi moja ya mpira wa miguu
alifuatwa na Dude (mwigizaji) kumuomba akaigize nao ili kuziba nafasi ya
Dr. Cheni (Mwigizaji) ambaye kwa kipindi hicho alikuwa anahama toka
kundi la Splendid group na kuhamia Kaole sanaa group kutokana na
mwonekano wake na pia uchangamfu wake.
Baada ya kukaa splendid kwa muda mrefu alienda kwenye kundi la
nyota academia ambako alikutana na waigizaji kama Jacob steven (JB),
George Tyson, Monalisa, Natasha na Single Mtambalike ambao ye mwenyewe
anasema kutokana na uwezo wao wa kuigiza walizidi kumvutia zaidi
kuipenda sanaa.
Filamu alizocheza ni pamoja na Sabrina, Tunu, Riyama, Machozi, out of mind, libwata, mimba, mapito na nyingine nyingi.
Akiwa nyumbani Chekibudi hupenda kukaa na watoto wake na kutazama Filamu.
0 comments:
Post a Comment