SHULE YAGEUZWA KUWA DANGURO.
Danguro
hatari linaloendesha shughuli zake katika eneo la shule limefichuliwa
baada ya kumnasa mwanamke aliyedai ni mke wa mtu akifanya uzinzi na mtu
ambaye hakufahamika mara moja.
Tukio
hilo la aibu lilijiri ndani ya eneo la shule ya msingi Shekilango,
iliyopo Mapambano, Sinza jijini Dar es salaam, hivi karibuni ambapo mke
huyo wa mtu alikuwa akichepuka.
Wawili
hao, baada ya kukamatwa wakifanya ngono hadharani walitiwa kizuizini
kabla ya vijana wanaodaiwa kuchukua posho kwa wanaofanyia mambo yao
kwenye danguro hilo kuanzisha vurumai ingawa walidhibitiwa huku jamaa
aliyekuwa anahudumiwa akitoka nduki.
Akizungumza
na mwandishi, mwanamke huyo aliomba asamehewe na kusema kwamba
kinachomsababishia kufanya shughuli hiyo ni ugumu wa maisha na kundi la
watoto anaowalea ambao baba yao hana ajira.
Baada
ya mwandishi kutaka kuzungumza na mumewe ili kujua kama anafahamu kuwa
mkewe anafanya biashara haramu ya kuuza mwili, mwanamke huyo alidai
kwamba mumewe hana simu.
“Ni aibu, asubuhi watoto wanafagia
kondom, tunakosa cha kuwaambia, hii ni hatari kwa kweli na tunaomba
mamlaka zinazohusika zilifanyie kazi jambo hili,” alisema mwalimu Kilavo Charles wa shule hiyo baada ya kuzungumza na mwandishi kuhusiana na sakata hilo.
0 comments:
Post a Comment