NHC
Yatumia shilingi milioni 731,360,000/= kusaidia miradi ya vijana nchini
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)
limetumia jumla ya shilingi milioni 731,360,000/= kusaidia miradi ya vijana ya
kufyatua tofali nchini.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Kitengo cha
Huduma na Mawasiliano wa NHC, Bi Suzan Omari wakati wa Kikao kazi cha Maafisa
Vijana kilichofanyika hivi karibuni mkoani Tabora.
Bibi Suzan amefafanua kuwa fedha hizo zinahusisha ununuzi wa mashine uliyogharimu
shilingi 297,000,000/=, mafunzo ya wakufunzi yaliyogharimu shilingi
47,000,000/= na uwezeshaji mtaji wa
kuanzia kazi za vikundi vya vijana kufyatua matofali shilingi 81,500,000/=.
Ameongeza kuwa matumizi mengine kuwa ni
usambazaji wa mashine uliyogharimu shilingi 30,000,000/=, uhakiki wa ubora wa
mashine uliofanywa na wataalamu kutoka VETA shilingi 6,400,000/=, fedha za
kununulia vifaa vya mafunzo katika kila halmashauri vilivyogharimu shilingi
130,400,000 na posho ya wakufunzi wa VETA ni shilingi 139,060,000/=.
Bi Suzan amewataka vijana kote nchini
kutumia fursa hii kwa ajli ya maendeleo yao ikiwemo na kuondokana na tatizo la
kukukosa ajira. Amayetaka mashirka mengine nchini kuiga mfano wa NHC ili
kunusuru nguvu kazi hii kubwa.
Kwa upande mwingine, Meneja wa Huduma
kwa Jamii wa NHC, Bw, Muungano Saguya amesema kuwa wadau zikiwemo Halmashauri,
Maafisa Vijana wa Mikoa na wilaya kwa kushirkiiana na mamameneja wa mikoa wa
NHC wathamini mradi huu kwa kufuatilia ufanisi wake ili mradi huo uwe endelevu.
Ameongeza kuwa mradiukiwa endelevuna
kusaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana, bajeti itaongezeka kwa mwaka wa
fedhaujao ilikusaidia zaidi mradi huo kwa vijana.
Naye Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa Mkoa wa
Tabora, Bw. Erasto Chilambo amesema maafisa vijana wawaunganishe vijana katik a
vikundi ili watumie fursa hii kujiendeleza na kuacha kubweteka na kulalamika
kwa kukosa ajira. Aliongeza kuwa vijana wasiwe sehemu ya tatizo la ajira bali
wawe watatuzi wa changamoto inayowakabili
ya kukosa ajira.
Kikao hiki ni kikao cha kuwakumbusha
maafisa vijana majukumu yao kuwasaidia
kupata uzoefu toka kwa wenzao. Kimeandaliwa na Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo.
0 comments:
Post a Comment