Bwana mmoja nchini Zimbabwe amedai kuwa kahaba aliyekuwa akifanya naye mapenzi amegeuka ghafla na kuwa punda.
Bwana huyo, Sunday Moyo ambaye amefikishwa
mahakamani siku ya Jumatatu kwa kosa na kukutwa akifanya mapenzi na
mnyama huyo amesema anampenda sana mpenzi wake huyo. Bwana Moyo
aliiambia mahakama mjini Zvishavane kuwa huyo waliyemkuta naye sio punda
bali ni mwanamke ambaye alikutana naye katika klabu ya usiku ya
starehe.
Gazeti la Metro limesema polisi wa Zimbabwe
wakiwa katika doria saa za alfajiri, walimkuta bwana huyo mwenye umri wa
miaka 28, katika mji wa Mandava, akifanya mapenzi na punda nje ya
nyumba yake. Mnyama huyo alikuwa amelala chini huku shingo yake ikiwa
imefungwa kamba, na kamba hiyo kufungwa kwenye mti. Kwa mujibu wa
mtandao wa New Zimbabwe.com bwana Moyo amekiri makosa ya kujamiiana na
mnyama, lakini aliiambia mahakama kuwa "Mheshimiwa Jaji, niligundua tu
kuwa ni mnyama, wakati polisi waliponikamata". Bwana huyo amesema
alipata kahaba aliyekubali kulipwa dola ishirini, lakini amesema
hafahamu ilikuwaje hadi akageuka na kuwa punda. "Lakini bado nampenda
sana" amesema bwana Moyo. Bwana huyo ameswekwa rumande na kuamriwa
kufanyiwa uchunguzi wa akili.
0 comments:
Post a Comment