Clifford
Joseph Harris, Jr. a.k.a T.I mkali kutoka Marekani aliyeangusha show ya
nguvu katika jukwaa la Serengeti Fiesta 2014 siku ya Jumamosi Oktoba 18
mwaka huu katika viwanja vya Leaders Club Dar es Salaam, bado
ameendelea kuyasimulia mazuri na makubwa ya kuvutia aliyojionea
Tanzania.
Katika mahojiano aliyofanya jijini New York na kituo cha redio cha Power 105.1
kwenye kipindi cha Breakfast Club, T.I amesema tangu aanze kufanya
muziki hajawahi kufanya show kwenye jukwaa lolote mbele ya mashabiki
zaidi ya 50,000.
T.I amelinganisha idadi hiyo ya kutisha
kuwa ni sawa na kufanya show katika uwanja wa mpira wa miguu na kuujaza
kwa show moja, kitu ambacho sio rahisi kutokea.
Swali la kuhusu Ebola bado liliulizwa
kwa T.I, ambaye amesema hakuwa anahofu chochote alipokuja Tanzania,
zaidi zaidi alikuwa akifikiria kuhusu mpenzi wake.
“Afrika ni Kubwa ukilinganisha Nigeria
ambayo kiukubwa ni kama Texas, idadi ya watu waliopo Nigeria inalingana
nawatu waliopo Marekani. Sasa pata picha watu wote tuliopo Marekani
tukusanyike Texas. Kama kuna waathirika wanne, idadi hiyo yote haiwezi
kuathirika..”—T.I
0 comments:
Post a Comment