JAMBAZI SUGU KUUAWA MJINI ARUSHA

Hatimaye jambazi sugu lililokuwa likiwaua wanawake jijini
Arusha limeuawa,na jeshi la polisi,jambazi huyo aliyejulikana kwa jina la Ramadhani
Abdalah Jumanne.
Jambazi huyo aliye kuwa akitafutwa kwa muda mrefu na jeshi
la polisi aliuwa usiku wa kuamkia Octoba, 10 ,ambapo polisi waliamua kufanya
msako na hatimaye kufika anapo ishi ambapo majibishano ya risasi yalipelekea
kuuawa kwa jambazi huyo.
Akithibitisha kamanda mkuu wa polisi jijini Arusha Liberatus
Sabas,amesema kuwa jambazi huyo alitambuliwa na baadhi ya wanawake na pia
alifariki muda mchache akiwa anapelekwa hospitali.
0 comments:
Post a Comment