Followers

Tuesday, 14 October 2014

KIINGILIO MECHI YA SIMBA NA YANGA

HIKI NDICHO KIINGILIO MECHI ZA SIMBA NA YANGA.

Published in Michezo

Geilson Santana ‘Jaja’ akishangilia goli na wachezaji wenzake.
Kiingilio cha chini kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga na Simba itakayochezwa Jumamosi (Oktoba 18 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 7,000.

Mshambuliaji wa Simba Emmanuel Okwi akishangilia.
Washabiki watakaolipa kiingilio hicho ni wale watakaokaa viti vya rangi ya bluu na kijani ambavyo jumla yake ni 36,693 katika uwanja huo wenye viti 57,558. Viingilio vingine ni sh. 10,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 20,000 kwa VIP B na C wakati VIP A itakuwa sh. 30,000.
Tiketi zitakazotumika kwenye mechi hiyo ni za elektroniki, na zimeanza kuuzwa jana (Oktoba 13 mwaka huu). Tiketi zinapatikana kwa mtandao wa M-PESA, CRDB Simbanking na maduka ya CRDB Fahari Huduma ambayo yapo zaidi ya mia moja sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam.

0 comments: