USHINDI MTOTO WA MBUNGE,UTATA WAZUKA MISS TANZANIA
Siku chache baada ya mtoto wa Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu, Sitti
kujinyakulia U-Miss Tanzania 2014, tayari joto la ushindi huo limetikisa
taji hilo na kuibua maswali ‘chungu mbovu’ kuhoji uhalali wa ushindi
huo.
Miss Tanzania Sitti Mtemvu akiwa mwenye nyuso ya furaha baada ya kushinda taji hilo.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, vuguvugu za uhalali wa ushindi ziliibuka
muda mchache kabla ya shindano hilo kuchukua nafasi katika Ukumbi wa
Mlimani City, Ijumaa iliyopita ambapo wadau mbalimbali walianza kuhoji
kulikoni wafuasi wa mrembo huyo waingie na vipeperushi vingi vyenye
picha ya mshindi (Sitti).
“Tatizo lilianzia kwa watu wengi kuingia na vibendera vyenye picha ya
Sitti vikionyesha dhahiri kwamba walijua kabla kwamba ni mshindi hivyo
kuja wakiwa wamejipanga kabisa,” kilisema chanzo.
Chanzo hicho kilienda mbali zaidi kwa kusema hata katika suala zima
la mshindi kuandaliwa gari maalum la Hammer ambalo baadaye lilimchukua
na kumrudisha kivyake tofauti na washiriki wengine ambao waliondoka
ukumbini hapo na basi waliloandaliwa.
Miss Tanzania aliyemaliza muda wake,Happiness Watimanywa akimvika Crown na Taji Miss Tanzania Sitti Mtemvu.
“Waandaaji wanapaswa kutueleza vizuri, haiwezekani watu waandae
Hammer waje nalo ukumbini pasipo kuwa na uhakika wa ushindi, ule ni
utani,” kilinyetisha chanzo hicho.
Aidha, vuguvugu hilo lilijiongeza
zaidi baada ya watu kudai huenda ushindi huo ulitokana na mgongo wa
baba yake (mbunge wa Temeke) madai ambayo kwa pamoja yalikanushwa na
muandaji wa mashindano hayo, Hashimu Lundenga.
“Hakuna kitu kama hicho, malalamiko kila siku hayakosekani,
vipeperushi havikatazwi, majaji sita kati ya tisa waliwekwa na wadhamini
(TBL kupitia kinywaji chao cha Red’s), haiwezekani akawahonga majaji
wote hao.
“Kuhusu
gari, hakuondoka ukumbini na Hammer, aliondoka na basi kama washiriki
wengine, sijui hayo maneno yanatoka wapi,” alisema Lundenga.
Kwenye shindano hilo, Sitti aliwagaragaza washiriki wenzake 29 na
kuondoka na kitita cha shilingi milioni 18. Mrembo huyo ndiye
atakayeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya dunia (Miss World) hapo
baadaye.
0 comments:
Post a Comment