
MREMBO
na muigizaji wa filamu hapa nchini Wema Isaac Sepetu amerudi kutoka
nchini Marekani na sasa yupo
katika maandalizi ya filamu yake mwenyewe akiwa kama mtayarishaji na
muigizaji tofauti na siku za nyuma ambapo alikuwa akishiriki katika
filamu za watayarishaji wengine filamu hii ambayo bado hata jina
amelificha ipo mbioni kuanza kurekodiwa wakati wowote na akiwa location
ndiyo atataja jina la filamu hiyo. Wema huku akiwa ameongozana
na mchumba wake mpya kwa sasa Nassib Abdul ( Diamond) alisema kuwa
safari yake ya Marekani amejifunza mengi kuhusu masuala ya filamu kwa
hiyo anataka kutumia fursa hii kutengeneza filamu yenye ubora mkubwa
tena ikiwa chini yake mwenyewe anajua kwa kufanya hivyo ataweza
kutekeleza yale ambayo anaona ni bora kufanyika katika filamu za
kisasa.
“Nimerudi kwa nia moja tu ya kutengeneza filamu bora na ya kisasa,
unajua toka nimerudi kila mtu anataka kucheza filamu na mimi, lakini kwa
sasa siwezi kufanya hivyo hadi nitimize ndoto zangu za kuwa na filamu
yangu ambayo ni nzuri na itavutia wengi, mara nyingi nimekuwa
nikishiriki filamu za watu wengine lakini sasa ni yangu mwenyewe”
Alisema Wema.
Wema amefanya vizuri katika filamu ambazo aliwahi kuigiza hasa filamu
yake ya mwisho ya 14 Days aliyoigiza na Jacob Stephen (JB) ilikuwa
gumzo kiasi cha kila mtayarishaji kuona umuhimu wa binti huyu katika
tasnia ya filamu, lakini burudani unayopata ni kwamba na mchumba wake
naye inasemekana yupo katika harakati za kurekodi filamu yake naye,
wanakutana katika fani au nje ya fani?
|
0 comments:
Post a Comment