Rose Ndauka Afunguka kuwa haitaji mwanaume
SIKU chache
baada ya uchumba wake kuvunjika, msanii wa filamu Bongo, Rose Ndauka
amefunguka na kusema kuwa kwa sasa haitaji tena mwanaume kwani anajikita
zaidi katika kufanya kazi.
Akizungumza
na waandishi juzikati, Rose alisema katika maisha yake ya uchumba
alijifunza mambo mengi na anamshukuru Mungu amempa zawadi ya mtoto hivyo
anafanya kazi kwa bidii ili aweze kumlea mwanaye vizuri.
Alisema
hajutii kwa yaliyomtokea kwa mchumba wake Malik Bandawe, kwani makosa
yaliumbwa makusudi ili watu wapate kujifunza, hivyo akili yake kwa sasa
anaiwekeza katika kazi zake za sanaa.
0 comments:
Post a Comment