
Ushindi wa Bi Sitti Abbas Mtemvu
katika kinyang'anyiro cha mashindano ya urembo ya Miss Tanzania ya mwaka
2014 umezua shutuma juu ya uhalali wa mrembo huyo kuvikwa taji hilo.
Siku
chache baada ya kutangazwa kwake kuliibuka shutuma mbalimbali dhidi ya
Bi Sitti na kumwondolea vigezo vya umalkia huo wa urembo.Tuhuma hizo
zilianza kuzagaa katika mitandao ya habari ya kijamii zikiwemo shutuma
za kufanyika udanganyifu wa umri.
Kamati ya kuandaa mashindano
hayo, siku ya Jumanne imelitolea ufafanuzi suala hilo,mjini Dar es
Salaam, ambapo mkurugenzi mtendaji wa kamati hiyo, Hashim Lundenga
amesema, Sitti ndiye mshindi halali wa mashindano hayo ya mwaka 2014, na
kwamba shutuma dhidi yake hazina msingi wowote zaidi ya kuwa uzushi:
"Mimi nasema shutuma zote zilizotolewa hapa ni shutuma za uongo, kwa
sababu kulingana na taratibu nilizozieleza hapo awali, sisi kama kamati
kama waandaaji wa Miss Tanzania hatuna matatizo yoyote" anasema Bwana
Lundenga.
Akizungumzia tuhuma kwamba Bi Sitti alidanganya umri
kuwa ana miaka 18, mkurugenzi mtendaji wa kamati ya Miss Tanzania, Bwana
Lundenga ameshangazwa na uzushi huo, akisema mrembo huyo hajawahi
kutaja umri huo kama ndio umri wake. "hakuna mahala popote alipozungumza
kuwa ana miaka 18...Kwa hiyo ni rumours ambazo zinaendelea tu na
wameshindwa kuhakikisha"
Kwa ufafanuzi wa waandaaji wa mashindano
hayo, Sitti Abbas Mtemvu ni mshindi halali wa Miss Tanzania 2014 na
ndiye anayetarajiwa kuiwakilisha nchi katika mashindano makubwa ya
mrembo wa dunia ya Miss World yatakayofanyika 2015.BBC
0 comments:
Post a Comment