
Hoteli moja ya kifahari ya wanyama wa kufugwa nyumbani imefunguliwa nchini Singapore.
Hoteli hiyo inatoa huduma kama vile vidimbwi vya kuoga vya wanyama
hao,vyumba vyenye hewa safi na vyakula vya kuvutia, na hivyobasi
kuimarisha viwango vya kuwabembeleza wanyama hao katika taifa hilo lenye
utajiri mkubwa.
Hoteli hiyo yenye urefu wa futi 4,317 kwa jina Wagington Hotel
imejengwa katika nyumba za zamani za wakolini wa Uingereza
zilizobadilishwa katika makaazi ya wanadiplomasia.
Vyumba vya kulalia katika hoteli hiyo vinagharimu dola 271 kwa mbwa
watatu wanaotumia kwa pamoja chumba cha kifalme,kilicho na maeneo ya
kifahari ya kuweka balbu,runinga,na vitanda vilivyotengezwa na ngozi.
Hoteli hiyo iliojengwa hususan kwa mbwa pia huwakaribisha paka.
''iwapo tunajitakia mema katika maisha yetu, kwa nini marafiki zetu
walio waaminifu nao tusiwafanyie mambo mazuri'' aliuliza mmiliki wa
hoteli hiyo Estelle Taylor.
''Kama watu tunaowapenda wanyama,tuna hisi kwamba ni vyema kuwa na
eneo ambalo wanyama wanaweza kuwekwa ili nao wajisikie nyumbani''
aliongezea.
Wanaomiliki wanyama hao pia wanaweza kupata eneo la kufanya
mafunzo,kunyoa, kukata kucha,kubadilisha rangi za wanyama hao pamoja na
masaji.
Hoteli hiyo pia hutoa huduma ya gari la kifahari aina ya Limousine
kwa wanyama hao kutoka makaazi yao hadi hoteli hiyo na kutoka hoteli
hiyo hadi makaazi yao.
Nchini Singapore kuna zaidi ya maduka 250 ya wanyama, mengi yakiwa katika maduka makubwa ya jumla.
Mfanyibiashara mmoja hutoa huduma za kitalii kila wikendi ambapo
wamiliki wa wanyama hao na wanyama wenyewe hutembezwa katika maboti.BBC
0 comments:
Post a Comment