Hii ni taarifa ya ajali ambayo
imegharimu maisha ya Watu kumi na mbili,wakiwemo wanaume sita,wanawake
wanne na watoto wawili baada ya basi mali ya kampuni ya Al-Jabir yenye
namba za usajili T 725 ATD kuigonga na treni ya Shirika la Reli la
Tanzania na Zambia(Tazara).
Ajali hiyo imetokea majira ya saa tisa
alasiri katika eneo la Kiberege ifakara wilayani kilombero Mkoani
Morogoro,Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Sacp Leonard Paulo
amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
0 comments:
Post a Comment