Mwimbaji wa muziki wa kizazi kipya hapa Tanzania maarufu kwa jina la Abbas Hamis aka 20% ambaye aliwahi kuvunja records ya Tuzo za Kilimanjaro Music Awards 2011, kabla Diamond kushikilia records hiyo, amefunguka na kuelezea mchongo wake wa kutoa ngoma ambayo ipo tayari na imepewa jina la 'Akabebabeba' kwa staili tofauti.
"Sasa hivi nimekuwa na mambo mengi coz mimi ni mkulima mzuri, Mwigizaji, pia ni mwimbaji wa Muziki kama ambavyo watu wananifahamu, so tarehe 26 May 2015 nategemea kuachia wimbo wangu wa 'Akabebabeba' online umetengenezwa na Producer Nas B studio ‘Pamoja Records’ ili mashabiki wangu waweze kwenda sawa na mimi kaeni mkao wa kula"- 20%’
0 comments:
Post a Comment