Wamekuwa kwenye mahusiano kwa muda mrefu sana lakini hatimaye hapo juzi kati walivishana pete ya uchumba ndani ya club Kakala iliyopo Kigamboni jijini Dar es salaam.
Msanii wa Bongo Fleva kutoka kundi la Gangwe Mob - Luteni Kalama na msanii wa kike kutoka Scorpion Girls ambaye aliwahikuwa Miss Ruvuma - Bella Fasta, mara baada ya kuvishana pete ya uchumba wamefunguka juu ya mpango wao wa kubariki ndoa ifikapo mwezi wa 12.
"Tumepanga mwezi wa kumi na mbili Inshaallah mambo yakienda kama tulivyopanga basi tutaingia kwenye ndoa rasmi na kuanza maisha rasmi ya mke na mume" - Aliongea Luteni Kalama alipokwenda kumsindikiza Bella kuitambulisha rasmi video ya ngoma yake aliyomshirikisha Baby Madaha ndani ya Friday Night Live ya EATV.
0 comments:
Post a Comment