
MAPEMA mwezi huu, Chama cha Filamu Tanzania kilipata uongozi
mpya, Steven Mengele maarufu Steve Nyerere alichaguliwa kuwa mwenyekiti
akirithi mikoba ya Vicent Kigosi ‘Ray’ aliyemaliza muda wake.
Wengine waliopata nyadhifa za juu katika uongozi
huo ni Makamu Mwenyekiti Mahsein Awadh ‘Dokta Cheni’, Katibu Mkuu
William Mtitu na naibu wake, Devotha Mbaga huku Issa Mussa ‘Cloud’
akichaguliwa kuwa Mweka Hazina.
Kama ilivyo sehemu yoyote duniani uongozi mpya
unapoingia madarakani, huweka malengo na vipaumbele vyake ili
kuwawakilisha vyema wale waliowachagua.
Katika mahojiano maalumu na Mwanaspoti, Steve
Nyerere alizungumzia mikakati yao mitano muhimu wanayotaka kuipa
kipaumbele kuwa ni;
Kudhibiti wizi wa kazi za filamu
Suala kubwa ambalo limekuwa likiwaumiza wasanii ni
wizi wa filamu, hasa unaofanywa na wachuuzi wenye vibanda vya kuuza na
kutengeneza santuli ‘CD’. “Tumekosa utaratibu maalumu wa kudhibiti wizi
wa kazi zetu, watu wamejifungulia vibanda wanatengeneza santuli za
filamu zetu na kuziuza kwa bei chee bila ridhaa yetu.”
“Hili linatuumiza sana wasanii, hivyo uongozi wetu
umepanga kushirikiana na serikali ili kudhibiti suala hilo, hatutakaa
chini kamwe tukiendelea kushuhudia uhalifu huu mkubwa wa kazi zetu,”
anasema Nyerere ambaye ni mwigizaji wa filamu za vichekesho maarufu
komedi.
Mavazi na nidhamu
“Imekuwa ni aibu sasa, wasanii wanavaa mavazi ya
ajabu na udhalilishaji hadi watazamaji wanaona aibu kutazama filamu
zetu. Uongozi mpya kwa kushirikiana na wadau muhimu tumepanga kupambana
na kadhia hii ili kurejesha heshima ya Bongo Movie.”
“Tunataka mtu avae kutokana na uhusika wa sehemu
anayocheza, kama ni mama wa nyumbani avae kama mama wa nyumbani na kama
ni changudoa avae kama changudo si filamu nzima wote wamevaa kama
machangudoa,” anasema.
Ubora wa filamu
Nyerere anasema suala la ubora mdogo wa filamu za
Bongo si jambo geni, filamu za Bongo zimekuwa zikifyatuliwa kama njugu,
kila siku kuna filamu mpya jambo ambalo amedai hawezi kulifumbia macho
0 comments:
Post a Comment