Ni
masaa machache tu yamepita tangu muziki wa kizazi kipya Tanzania, Bongo
Fleva kumpoteza aliyekuwa staa wa muziki huo kutoka kundi la TMK
Wanaume Family, aliyekuwa akifahamika kwa jina la YP, taarifa nyingine
ya simanzi inahusu msiba wa aliyekuwa muigizaji wa Bongo Muvi.
Katika ukurasa wake wa instagram, muigizaji na mchekeshaji maarufu
anayefahamika kwa jina la Kitale ama Mkude Simba (@mkudesimbaoriginal),
amepost picha ya muigizaji Shery Mwana aliyefariki masaa machache yaliyopita.
Kwa mujibu wa Kitale, muigizaji huyo mbaye jina lake halisi ni Sherry Charles Magali, aliwahi kushiriki na Kitale katika movie mbali mbali ikiwemo Kipotabo na Nyumba Nne.
0 comments:
Post a Comment