Snura Mushi
Anafahamika kama Snura Mushi ni wanadada mwenye
vipaji vingi ndani ya tasnia ya bongo movies. Pamoja na kuwa mwigizaji
aliyekuja kwa kasi sana pia Snura ni mwanamuziki wa bongo fleva
anayefanya vizuri sana sokoni kwa nyimbo zake mbalimbali zenye mahadhi
ya pwani mithili ya mduara. Pamoja na kuwa na umbo na sura nzuri ya
kuvutia snura pia amekuwa akitawala sana vichwa vingi vya
habari,magazeti na redio kutokana na uwezo wake mkubwa wa kukata kiuno
kwenye nyimbo zake.
PICHA

FILAMU

MAISHA YAKE ZAMANI
Snura Mushi (Jina lake halisi) alizaliwa tarehe kumi na
mbili (12) mwezi wa kwanza (1) mwaka 1984 Jijini Dar es salaam ambako
aliweza kukua na kupata elimu yake hapo hapo Dar es salaam.
Tofauti na watu wengi wanavyofahamu, kipaji cha mwanadada
Snura kilianzia kwenye muziki kabla ya kuigiza na alikuwa na mwimbaji
wa taarabu na kundi la “new best star” mwaka 2004. Baada ya hapo
alianzisha kundi lake la muziki aliloliita “chanya na hasi” pamoja na
vijana wawili mmojawapo akiwa marehemu sharo Milionea kabla hajajiunga
rasmi na sanaa ya maigizo.
Kipaji cha mwanadada Snura Kiligunduliwa na mtu aliyefahamika
kwa jina la Siasa. Ambaye ndiye aliyemfuata na kumshauri kuigiza baada
ya kuvutiwa na uzuri na umbo lake ambalo kwa mujibu wa mtu huyo alikuwa
na “star look” na angeweza kufanya vizuri kama angejiingiza katika
sanaa. Hiyo ilikuwa ni mwaka 2006. Na mwaka huo alipata nafasi ya
kuigiza kwenye Filamu ya Mfalme Seuta iliyodirectiwa na Gumbo Kihorota.
Baadaye aliweza kucheza movie za Zinduna na Hitimisho.
Snura alianza kujipatia umaarufu sana kupitia Filamu ya
ITUNYAMA, na pia kupitia igizo la Jumba la dhahabu alizofanya akiwa
chini ya director Tuesday Kihangala “Mr Chuzi”.
Akizungumzia maisha yake ya ustaa, Snura anasema kuwa huwa
anaumizwa sana pale anapoona habari kwenye vyombo vya habari
zinazomuhusu ambazo mara nyingi anasema huwa si za kweli.
Katika maisha yake ya kila siku Snura hupendelea sana kukaa
ndani na kutazama Filamu mbalimbali kwa ajili ya kujifunza mambo
mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment