Jacqueline Wolper


Anaitwa Jacqueline Wolper. Ni mmoja kati ya warembo
wenye umaarufu wa aina yake nchini na kwenye “industry” ya bongo movies.
Jack ni mwanadada mwenye mvuto unaokubalika na wengi na ameweza
kujipatia umaarufu mkubwa sana kupitia Filamu mbalimbali
alizoshirikishwa na mpya alizoanza kuzifanya chini ya kampuni yake
mwenyewe. Licha ya kuwa mwigizaji mwenye uwezo wa kipekee, Jack pia ni
mwongozaji mzuri wa Filamu na mwandikaji “script” mwenye viwango vya
kimataifa.
PICHA
FILAMU

MAISHA YAKE ZAMANI
Jacqueline Wolper alizaliwa tarehe sita (6), mwezi wa kumi
na mbili (12) wa mkoani Moshi –Kilimanjaro na kupata elimu yake ya
msingi katika shule ya msingi Mawenzi huko huko moshi na baadaye elimu
ya sekondari katika shule ya sekondari Magreth ekenywa iliyopo jijini
Arusha na baadae nchini Kenya.
Baada ya kumaliza elimu yake hiyo ya sekondari Jackline aliamua
kujiendeleza kwa kusomea mambo ya “sales and marketing” na baade alianza
kujihusisha na biashara za promotion na baadae allingia kwenye biashara
za saluni maeneo ya tandale jijini Dar es Salaam, kabla ya kujiingiza
kwenye sanaa ya uigizaji.
Jack aliingia kwenye sanaa kupitia kwa mwanadada Lucy komba
ambaye pia ni mwigizaji mwenzake ndani ya tasnia ya bongo movies nchini.
Yeye mwenyewe anasema kuwa Lucy ndiye aliyemfuata na kumshawishi
ajiunge naye kwenye maigizo kwani anaona anaweza na atafanya vizuri kama
ataamua kujiingiza kwenye sanaa. Kufahamiana kwa wawili hawa kulitokana
na wao kuwa majirani na kwa Lucy kuwa mteja wa mara kwa mara katika
“saloon” ya mwanadada Jack. Hii ilikuwa ni mwaka 2009.
Baada ya kushauriwa kwa muda mrefu ndipo Jack alipoamua
kujiingiza kwenye sanaa na kwa mara ya kwanza alionekana kwenye Filamu
ya “Ama Zangu Ama zao” aliyoifanya na mwanadada Lucy Komba.
Baada ya hapo alianza kupata mialiko toka kwa watu mbalimbali
ili aweze kuigiza kwenye Filamu zao ikiwemo Wiliam Mtitu pamoja na
Marehemu Steven Kanumba na aliweza kufanya Filamu mbalimbali
zilizomjengea jina ndani na nje ya nchi zikiwemo Red Valentine na Pusi
na Paku.
Akiwa nyumbani jackline wolper katika muda wa mapumziko,
hupendelea kujifunza kupiga gitaa, ushauri alioupata toka kwa marehemu
steven Kanumba na pia hupenda kupumzika na kufanya usafi wa nyumbani
kwakwe. Mida ya jioni huependelea kwenda kuogelea na kwenda kutazama
movie kwenye sehemu za cinema.
0 comments:
Post a Comment