Wastara Juma
Wastara Juma si jina geni kwenye ulimwengu wa
bongomovies. Ni mmoja wa wanadada wanofanya vizuri sana kwenye filamu
nchini na wenye ushawishi mkubwa sana ndani ya tasnia hii. Ifuatayo ni
historia fupi ya mwanadada huyu.
PICHA
MAISHA YAKE ZAMANI
Wastara Juma Issa alizaliwa Septemba 27, mwaka 1983 huko
mkoani Morogoro. Mwaka 1989 akajiunga na Shule ya Msingi Mvomelo ‘A’ na
kufanikiwa kumaliza elimu yake ya msingi mwaka 1995. .Mwaka 1996
alijiunga na Sekondari ya Agricalture mkoani humo.
Career
Mwaka 1999 Wastara aliingia rasmi kwenye sanaa ya maigizo na
filamu yake ya kwanza kucheza iliitwa Utaishia kunawa akiwa na gwiji wa
vichekesho nchini King Majuto.
Mwaka 2004 mpaka 2006 alianza kuonekana kwenye mchezo wa Miale uliokua unarushwa na kituo cha television cha ITV
KUKUTANA NA JENIFA MGENDI
Wastara hakudumu sana kwenye kundi hilo, alikutana na kina
Jenifa Mgendi ambaye pia walifanikiwa kuigiza naye filamu
iliyowashirikisha baadhi ya wasanii wa kitambo akiwamo Dino na wengineo.
Mwaka 2007, Wastara alifanya usahili kwenye filamu ya mdau Ande
John iliyofahamika kama Pelemende, akafaulu na kuigiza kwenye filamu
hiyo kisha zikafuata filamu nyingine kama Penina kabla ya kutimkia
nchini Kongo kufanya biashara.
KUKUTANA NA SAJIKI
Aliporejea kutoka Kongo, Julai, 2007, Wastara aliitwa na
mwigizaji Shija ambaye alimuomba aigize naye filamu baada ya kumuona
kupitia kazi mbalimbali alizowahi kufanya hapo nyuma.
Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa Wastara kukutana na Sajuki ambaye
sasa ni mumewe wa ndoa kwani Shija alikuwa akifanya kazi zake za
uigizaji kwa kupata msaada mkubwa kutoka kwa Sajuki.
Wastara alicheza filamu kadhaa akiwa na Shija pamoja na Sajuki
hadi baadaye walipokuja kugundua kuwa matatizo ya uhusiano yaliyowakuta
(Sajuki na Wastara) yanafanana kwani kila mmoja wao alitendwa na mpenzi
wake ndipo walianzisha uhusiano wa kimapenzi.
“Eeeeh! Kazi na dawa, tuligundua kuwa matatizo yetu yanafanana. Taratibu tukaanza uhusiano ili kufarijiana,” anasema Wastara.
FILAMU WALIZOZALISHA
Wakiwa ndani ya umoja wao, Sajuki na Wastara, walifanikiwa
kuporomosha filamu zaidi ya 20 ikiwemo Mboni yangu iliyopata umaharufu
mkubwa
APATA AJALI
Wakati harakati za ndoa zikiwa zimepamba moto, mwaka 2009 Wastara alipata ajali ya pikipiki iliyosababisha akatwe mguu.
Wakati huo tayari alikuwa ameshachumbiwa na Sajuki.
Juni mwaka huo huo,
wasanii hao waliopitia changamoto kadhaa za maisha, walifunga ndoa na kuanza rasmi maisha ya mume na mke.
Baada ya hapo, kupitia kampuni yao ya Wa-Jey waliendelea kuzalisha filamu kama Briefcase, The Killers, Seven Days na nyinginezo.
Tarehe 2 mwezi wa kwanza (1) mwaka 2013 Wastara alimpoteza mume
wake kipenzi Juma Kilowoko (sajuki) jambo lillilosababisha kupumzika
sanaa kwa muda na badae alilejea kwenye tasnia na kutoa filamu ya
Shaymaa amabayo ilipata umaharufu mkubwa
Nampaka sasa anaendelea kufanya filamu nchini Tanzania
0 comments:
Post a Comment