Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Nov
05 amefanya uteuzi wa wakuu wapya wanne wa Mikoa na kuwahamisha wengine
sita na watatu wengine kupangiwa kazi nyingine.
Wakuu wapya wa Mikoa hao ni pamoja na Bi. Halima Omari Dendego ambaye
amekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,Dkt. Ibrahim Hamisi Msengi ambaye
amekuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Bi. Amina Juma Masenza ambaye amekuwa
Mkuu wa Mkoa wa Iringa na Bwana John Vianney Mongella ambaye nae amekuwa
Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
Wakuu wa Mikoa ambao wamehamishwa vituo vya kazi ni pamoja na Bwn.
Magesa S. Mulongo ambaye atakua Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kutoka
Arusha,Dkt. Rehema Nchimbi ambaye anakwenda Mkoa wa Njombe kutoka
Dodoma,Bwana Ludovick John Mwananzila anakwenda Tabora kutoka
Lindi,Kepteni (Mst) Anseri Msangi anayekwenda Mkoa wa Mara kutoka Njombe
na Mhandisi Everist Ndikilo ambaye anakwenda Arusha kutoka Mwanza.
Wengine waliohamishwa ni Luteni (Mst) Chiku A.S. Galawa ambaye
anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kutoka Tanga, Dkt. Rajab Rutengwe ambaye
anakwenda Mkoa wa Tanga kutoka Katavi, Bi Fatma Mwasa ambaye anakuwa
Mkuu wa Mkoa wa Geita kutoka Tabora na Bwana Magalula S. Magalula ambaye
anahamishiwa Lindi kutoka Geita.
Taarifa hiyo imesema kuwa Wakuu wa Mikoa ya Dar es Salaam, Kigoma,
Kilimanjaro, Manyara, Mbeya,Morogoro, Pwani, Rukwa, Shinyanga, Ruvuma,
Singida na Simiyu watabakia kwenye vituo vyao vya sasa.
Wengine walioapishwa leo Ikulu ya Dar es salaam na Rasi Jakaya
Kikwete ni pamoja na mhe Samwel William Shellukindo kuwa balozi na
msaidi wa rais masuala ya diplomasia,Dkt Yohana Budeba kuwa katibu mkuu
wizara ya maendeleo ya mifugo na uvuvi,Injinia Mbogo Futakamba kuwa
katibu mkuu wizara ya maji.
Mbali na hao pia wengine ni Dkt Donan Mmbando kuwa katibu mkuu wizara
ya afya na ustawi wa jamii,Mhe Jack Mugendi Zoka kuwa balozi wa
tanzania nchini Canada pia Mhe Charles Pallangyo kuwa katibu tawala wa
mkoa wa geita na Bw Adoh Stephen Mapunda kuwa katibu tawala wa mkoa wa
arusha.







Picha:issamichuzi.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment