‘UKAWA’ YAZALIWA BONGO MOVIE
Stori: Gladness Mallya na Gabriel Ng’osha
WASANII
wa filamu ambao hivi karibuni waliripotiwa kujitoa katika kundi la
Bongo Movie Unity wamedaiwa kuunda la kwao linalojulikana kama Ukawa
ambalo litakuwa chini ya uongozi wa Mwenyekiti aliyetimuliwa, Steven
Mengere maarufu kama Steve Nyerere.
Baadhi ya Wasanii wa bongo Movies waliokuwa pamoja katika uongozi kabla ya mzozano.
Baadhi ya wasanii wanaotajwa kuunda kundi hilo kwa mujibu wa chanzo
chetu makini ni pamoja na Devotha Mbaga, Salama Salmin ‘Sandra’, Halima
Yahya ‘Davina’ na wengineo.
“Yaani sasa hivi haya makundi mawili kuna
vita kali sana, kila moja linataka lionekane kwamba lina nguvu kuliko
lingine, hata jina la Bongo Movie Unity limebadilishwa sasa hivi
linaitwa Bongo Movie Stars,”kilisema chanzo hicho.
Aliyekuwa Katibu msaidizi wa Bongo Movies Unity, Devotha Mbaga.
Mussa Issa ‘Cloud’ alikiri kubadilishwa jina kwa Bongo Movie Unity na
pia amesikia habari za kuwepo kwa kundi la Ukawa wakati Steve Nyerere
alisisitiza kuwa bado ni mwanachama wa Bongo Movie Unity na kwamba mtu
anayetaka kuwagombanisha wasanii anajulikana.
0 comments:
Post a Comment