Followers

Tuesday, 21 October 2014

JE UNAHITAJI KAZI AU AJIRA SOMA HII.

AFISA KAZI II ( LABOUR OFFICER II) – NAFASI 21

Wizara ya Kazi na Ajira

Date Posted: Oct 18, 2014

Region: Dar-Es-Salaam
Application Deadline: Oct 31, 2014

Position Description:

 

Nafasi hizi ni kwa ajili ya Wizara ya Kazi na Ajira

1.1.1 MAJUKUMU YA KAZI

· Kupokea na kuchambua malalamiko mbalimbali yanayohusu Sheria za kazi

· Kufanya Ukaguzi wa Utekelezaji wa Sheria za Kazi.

· Kukusanya taarifa na takwimu za kazi kutoka sehemu za kazi.

· Kupokea na kuchambua taarifa za migogoro ya kazi.

· Kupokea na kuchambua maombi ya kuandikisha mikataba ya hiari.

· Kupokea na kuchambua madai ya fidia na kiinua mgongo

· Kuandikisha watafuta kazi (job Seekers)

· Kupokea na kuandikisha nafasi za kazi toka kwa waajiri.

· Kupokea na kuchambua maombi ya vibali vya ajira ya wageni na kutunza

kumbukumbu za ajira za wageni nchini

· Kukusanya taarifa na takwimu zinazohitajika kwa ajili ya kamusi ya Kazi

(Dictionary of Occupational Titles )

1.1.2 SIFA ZA MWOMBAJI

· Kuajiriwa wenye Shahada ya Sheria au Sayansi ya Jamii (Sociology)

1.1.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi

Application Instructions:

 

Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa

mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa

na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo

hiki pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi

zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya

Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza Nafasi za kazi 21 kwa ajili ya Katibu Mkuu

Wizara ya Kazi na Ajira.

NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.

Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45

i. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.

ii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia

katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za

kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.

iii. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya bahasha, kutozingatiwa hili

kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.

iv. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye

anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)

watatu wa kuaminika.

v. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya

kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya

2

kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho

hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka au kupotea.

- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.

- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI

- Computer Certificate

- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)

- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.

vi. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za

kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)

HAVITAKUBALIWA.

vii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na

kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).

viii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba

isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.

ix. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko

katika utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo

yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.

x. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za

kisheria.

xi. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 31 Oktoba, 2014

xii. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira

HAURUHUSIWI.

xiii. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe

kupitia posta kwa anuani ifuatayo.

Katibu

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishiwa Umma

S. L. P 63100,

DAR ES SALAAM.

AU  

Secretary

Public Service Recruitment  Secretariat,

P. O. Box 63100

 DAR  ES SALAAM.

0 comments: