KWA MWENENDO HUU NDOA ITAKUWEPO KWELI.
LICHA ya kutothibitishwa juu ya kuwepo au kutokuwepo kwa ndoa yake na mwanamuziki Judith Wambura Mbibo ‘Jide’, mtangazaji maarufu Bongo, Gardner G. Habash ‘Kepteini’ amenaswa na kabinti akiwa kwenye pozi tata za kimahaba hivyo baadhi ya watu kuhoji anasaliti ndoa? Risasi Jumamosi lilifuatilia hatua kwa hatua.
Mtangazaji maarufu Bongo, Gardner G. Habash ‘Kepteini’ akiwa katika pozi la kimahaba na binti huyo.
OFM KAZINI, TUJIUNGE COCO
Tukio hilo lililojaa viulizo kibao bila majibu, lilifuatiliwa na Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers hatua kwa hatua ambapo lilijiri Jumatano iliyopita kwenye Ufukwe wa Coco uliopo Oysterbay jijini Dar kulipokuwa tamasha la wazi la kuibua vipaji vya wasaniii mbalimbali.
Awali, vijana mbalimbali walipanda katika onesho hilo na kuonesha vipaji huku binti huyo jina halikupatikana mara moja, alionekana na rafiki yake ambapo wote walikuwa ni washiriki katika onesho hilo.
GARDNER AMUIBUKIA
Wakati
mtangazaji huyo akiwa katika mizunguko yake ufukweni hapo, ghafla jicho
lake lilitua kwa binti huyo na kumfuata kisha kumnong’oneza kitu
(haikujulikana alimwambia nini).
Huku wapenda ‘ubuyu’ wakimfuatilia kwa ukaribu, ndani ya muda mfupi, binti huyo alionekana kuelewa mazungumzo ya Gardner kwa kutingisha kichwa kuashiria ujumbe umemfika vizuri.
WACHEPUKA
Baada
ya Gardner na mrembo huyo kusikilizana, wanahabari wetu waliwashuhudia
wawili hao wakishikana mikono na kuondoka eneo hilo kwenda kununua
vinywaji kisha wakajitenga sehemu wakinywa vinyaji huku Gadner akiwa
amemkubatia kwa nyumba mtoto huyo mzuri na mwembamba kama Jide.
WAKIHAMA PAMOJA
Mashushushu
wetu waliwashuhudia wawili hao wakipiga misele pamoja katika maeneo
mbalimbali ya ufukwe huo huku mtoto wa kike akiachia tabasamu zito huku
jamaa akiwa amemzungushia mkono kiunoni, wakizungumza maneno yalioonesha
kuwa wapo kwenye urafiki mzuri.
Akimnong'oneza jambo.
WAPENDA MAJAMBO NAO!
Wakati
Gardner akiwa bize akifanya yake huku akiwa ameongeza umakini, baadhi
ya watu ambao ni wepesi kufuatilia mambo ya watu (wapenda ubuyu/umbeya),
walianza kuibua minong’ono kwamba kulikoni mtangazaji huyo ambaye
amekuwa mzito kutamka kwamba hawako pamoja na Jide, ajiachie kiasi hicho
na mrembo huyo.
“Jamani huyu si ni Gardner? Vipi tena mbona anaambatanaambatana na huyu mtoto? Kwa vyovyote ni wazi kabisa kuna kitu kinaendelea kati yao, maana muda wote wapo beneti.“Duh! Sijui Jide akiwaona katika pozi kama hizi atajisikiaje kama kweli hawajaachana,” alisikika mmoja wa wapenda ubuyu.
Baada ya wanahabari wetu kupata walakini na kutaka kuthibitisha hilo, walianza kumfuatilia hatua kwa hatua mpaka waone mwisho wa mchezo utakavyokuwa baada ya kuona dalili hizo, kwa kuwa kadiri muda ulivyozidi kwenda ndivyo mambo yalipozidi kujianika hadharani huku wakijitahidi kukwepa kamera lakini waligonga mwamba.
WAKIBADILISHANA VINYWAJI
Kuonesha
kwamba urafiki wao si wakubahatisha, kuna wakati Gardner na mrembo huyo
walibadilishana vinywaji jambo ambalo lilifanyika chini ya wapambe wa
Gardner ambao walikuwa wakimzingira ili mapaparazi wasiweze kupata picha
kwa urahisi.
Akizidi kuwanaye bega kwa bega.
0 comments:
Post a Comment