Msanii Elizabeth Michael
aka Lulu leo ametambulisha Filamu yake Mpya ambayo imeingia sokoni leo
iitwayo MAPENZI YA MUNGU, huku akiwa amemshirikisha Msanii wa Bongo
Fleva Linah Sanga na Mama Kanumba.
Wakati akiilezea filamu
hiyo leo mbele ya wanahabari Lulu amesema Kuwa Ni Filamu inayofundisha
na Kutoa somo kwa mtu yoyote yule ambae yupo hapa duniani kwa kuendelea
kuonyesha kuwa MUNGU YUPO. Akiongezea kuwa…”Sisi kama binadamu tumekuwa
tukifanya mambo mengi sana hapa Duniani na kupelekea kumsahau Mungu na
pengine kuendelea kufikiria kuwa yote tuyafanyayo ni kwa uwezo wetu
kumbe Sio uwezo wetu na Ni Mapenzi ya Mungu tu ndio yanayofanya sisi
kufikia hapa tulipo leo”
Filamu ya MAPENZI YA MUNGU
imekuwa gumzo kabla ya kutoka kutokana na watanzania wengi kuwa na
shauku ya Kutaka kumuona Lulu tena mara baada ya Kuonekana katika
Filamu Zake Mbili zilizotangulia za FOOLISH AGE na FAMILY CURSE. Sasa
Lulu kuonekana tena katika kiwango cha Juu katika Filamu hii Mpya ambayo
imeingia Sokoni Leo.
Filamu ya MAPENZI YA MUNGU ni filamu inayosambazwa na Kampuni ya Proin Promotions Ltd.
Msanii wa Sanaa ya
Maigizo Nchini, Elizabeth Michael (Lulu) akiongea na
waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa alipokuwa akiitambulisha
filamu yake Mpya iitwayo MAPENZI YA MUNGU ambayo amewashirikisha Flora
Mtegoha (Mama Kanumba) na Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Linah Sanga.

Msanii Wa Maigizo
Nchini, Elizabeth Michael (Lulu) akiitambulisha filamu yake
Mpya iitwayo MAPENZI YA MUNGU leo mbele ya wanahabari (hawapo
pichani).,Kulia ni Mmoja kati wa wasanii walioshiriki katika filamu hiyo
ajulikanae kama Flora Mtegoha (Mama Kanumba)
Meneja Masoko wa
Kampuni ya Proin Promotions Ltd, Evance Stephen akiongea na wanahabari
leo katika Ofisi za Proin Promotions Ltd zilizopo Mikocheni mtaa wa
Ursino wakati wa Utambulisho wa Filamu mpya ya Lulu Iitwayo MAPENZI YA
MUNGU.
0 comments:
Post a Comment