UANZISHWAJI KTUO KIPYA CHA INTANETI WAANZA.

Naibu
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba (kulia)
akizungumza na wanahabari mara baada ya mkutano wa wadau wa mawasiliano
Afrika ikiwemo kampuni ya TTCL.

Naibu
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba
akizungumza katika mdahalo wa wadau wa mawasiliano uliofanyika leo
jijini Dar es Salaam.

Naibu
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba
akizungumza katika mdahalo wa wadau wa mawasiliano uliofanyika leo
jijini Dar es Salaam.

Kampuni ya TTCL yaanzisha kituo cha interneti ‘IP Pop’

Ofisa
Mkuu Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota
(kushoto) akizungumza na wanahabari mara baada ya mkutano wa wadau wa
mawasiliano Afrika ikiwemo kampuni ya TTCL.

Ofisa
Mkuu Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota
(kushoto) akizungumza katika mdahalo wa wadau wa mawasiliano uliofanyika
leo jijini Dar es Salaam.

Kampuni ya TTCL yaanzisha kituo cha interneti ‘IP Pop’

Ofisa Mratibu wa Ufundi wa TTCL, Mhandisi Anifa Chingumbe (kushoto) akimwelezea.

Baadhi ya wadau washiriki katika mkutano wa wadau wa mawasiliano Afrika ikiwemo kampuni ya TTCL wakifuatilia mkutano huo.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Ofisa Mkuu Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota alipokuwa akizungumza na wanahabari katika mkutano wa wadau anuai wa mawasiliano kutoka nchi za Afrika Mashariki na baadhi za mataifa ya Afrika unaofanyika Tanzania. Ngota alisema kampuni ya TTCL imekuwa na mchango mkubwa wa kusimamia Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ili kuwawezesha Watanzania na hata nchi jirani kupata mawasiliano mazuri kutoka katika nchi zao hadi katika nchi za ulaya.
“…Kuna juhudi mbalimbali TTCL tunafanya ili kuongeza fursa kwenye mawasiliano ambapo kwa sasa tumefungua kituo cha kuuzia interneti hapa nchini, kinaitwa IP Pop (Internet Protocol Point of Presence). Awali interneti tulikuwa tunaenda kununulia London kwenye makampuni mbalimbali sasa hivi tumeanzisha kituo chetu cha kununulia intaneti hapa hapa nchini…Kwa hiyo tunawakaribisha watumiaji wa interneti kuja kununua huduma hizi kwetu,” alisema Ngota.
Akizungumzia mkutano huo, Ngota alisema wadau wa mawasiliano Afrika ikiwemo TTCL imejipanga vizuri kutumia fursa ambazo zinaweza kupatikana nchini na nje ya nchi ili kuendeleza sekta ya mawasiliano. “…Unapopiga simu lazima uende hadi nchi za nje kupata ile njia alafu ndo unarudi ulipo Afrika sasa hivi tunaangalia namna gani tutajikwamua na huduma kama hizo kuzipata hapa hapa Afrika…” alisema ofisa huyo wa TTCL.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba akizungumzia mkutano huo alisema mkutano huo ni muhimu kwani wadau wa mawasiliano wamekutana kujadili maendeleo ya sekta ya mawasiliano, hasa katika ukanda wa afrika mashariki na afrika kwa ujumla. Alisema Tanzania inategemewa sana na nchi karibia saba ambazo zipo pembezoni mwa bahari kupitia huduma ya mkongo wake wa mawasiliano.
“Mkongo wa mawasiliano wa kimataifa umetua katika bahari yetu na sisi tunauza huduma hiyo kwa nchi nyingine…Tumeupeleka hadi kwenye mipaka ya majirani zetu kama Rwanda, Burundi, Malawi, Zambia na wengineo ambao hawana mawasiliano.”
Makamba alisema mpango wa Serikali ni kuhakikisha kila Mtanzania anapata mawasiliano mazuri na yalio bora maana hiyo ni haki yake. Sera na kanuni za Serikali ni kuhakikisha hilo linafanikiwa. Aliongeza kuwa kwa kulitambua hilo Serikali imewekeza kiasi kikubwa cha fedha kujenga mkongo wa taifa wa mawasiliano.
“..Na sasa tunaingia kwenye awamu ya tatu ya upanuzi wa mkongo huo ikiwa ni sambamba na uboreshaji wa mawasiliano, ili ufike kila wilaya nchini, Watanzania wengi maeneo ya vijijini bado hawana mawasiliano, sehemu nyingine hakuna mawasiliano kabisa au pengine yapo lakini si mazuri.
Aidha alibainisha kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2015 maeneo yote ambayo hayana mawasiliano yanapata mawasiliano, hii ni pamoja na kukaribisha makampuni mapya yaweze kuwekeza katika sekta hii ili uwepo ushindani kwamba kama kuna maeneo kampuni fulani haitaki kwenda basi nyingine ziende huko.
*Imetolewa na www.thehabari.com
0 comments:
Post a Comment