Serikali
ya Mali imethibitisha kuhusiana na taarifa za mtoto wa miaka 2 kukutwa
na maambukizi ya Ebola akiwa ni mtu wa kwanza kupata maambukizi ya
ugonjwa huo nchini humo tangu ugonjwa huo ulipozuka mwezi Machi 2014.
Taarifa kutoka mtandao wa the World Post
zimesema, mtoto huyo amegundulika kuwa na maambukizi ya ugonjwa huo
aliporejea nchini humo akitokea Guinea, moja ya nchi zilizoathiriwa
zaidi na Ebola Afrika Magharibi.
Mali inakuwa nchi ya sita kutangaza
kupatikana mgonjwa mwenye maambukizi ya Ebola katika ukanda wa Afrika
Magharibi, lakini ndani ya siku 7 nchi za Senegal na Nigeria zimetangaza
kutokuwa na mgonjwa mwenye maambukizi ya Ebola.
Ripoti iliyotolewa na WHO imeonesha vifo zaidi ya 4,900 vimetokea katika nchi za Sierra Leone, Guinea na Liberia.
Timu ya wanasayansi wa kimataifa
imejipanga kutafiti uwezekano wa kutumia damu ya mtu aliyewahi kupona
Ebola kama tiba ya ugonjwa huo.
Mali inapakana na nchi ya Guinea kwa
upande wa Kusini Magharibi, lakini mtoto huyo anakuwa mgonjwa wa kwanza
kuripotiwa kuwa na maambukizi ya Ebola nchini humo.
0 comments:
Post a Comment