Followers

Thursday, 23 October 2014

SOMA HII SIRI KUHUSU UHUSIANO ANTI LULU NA BONDI.

Stori: Gladness Mallya na Hamida Hassan SIRI imefichuka juu ya wasanii wawili waliokuwa wapenzi wa muda mrefu na kumwagana, Lulu Semagongo ‘Anti Lulu’ na Bondi Sinan kwamba walipeana kiapo kizito, Ijumaa limetonywa.

Staa wa filamu Bongo, Lulu Semagongo ‘Anti Lulu’.

Chanzo makini kilichoomba hifadhi ya jina lake kilidai kuwa, katika mapenzi yao waliapizana kwamba hakuna ruhusa kwa mmoja wao kuzaa na mtu mwingine na ndiyo maana wote walipokiuka, yaliwafika mazito.

“Kiapo ni kitu kibaya sana, hivi karibuni Bondi alifiwa na mwanaye na Anti Lulu aliwahi kuwa na mimba ya mwanaume mwingine ikatoka, ukiunganisha matukio unaona kiapo chao kinafanya kazi,” kilidai chanzo hicho.

Bondi Sinan akiwa na Wastara.

Baada ya kuzinyaka habari hizi paparazi wetu alimtafuta Anti Lulu ambaye alifunguka: “Ni kweli tuliapizana lakini mwenzangu alikiuka na kwenda kuzaa na mwanamke, mtoto amefariki na mimi nilibeba ujauzito mimba ikatoka.

“Mimi na Bondi tumetoka mbali sana na naamini hawezi kumuoa mwanamke mwingine zaidi yangu nikishamaliza mambo yangu na kuamua kutulia nitarudi tu kwake na huyo Wastara atamuacha,” alisema Anti Lulu.

0 comments: