Msanii
Maarufu nchini Ahmed Olotu 'Mzee Chilo' wa kwanza kulia akimsikiliza
mwenyekita wa SHIWATA Cassim Taalib wa pili kushoto walipokuwa wakigawa
mashamba kwa ajili ya wanachama wao
|
Watakaohamia kijiji cha wasanii kupewa bustani bure
Na Mwandishi Wetu
MTANDAO
wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umetoa bure kwa wanachama wake
wanaomiliki nyumba katika kijiji chao cha Mwanzega Mkuranga ya eneo la
kulima bustani.
Mwenyekiti wa SHIWATA,Cassim Taalib aliwaambia
waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuwa watakaonufanika na ofa hiyo
ni wale watakaohamia katika nyumba zao kabla ya Desemba mwaka huu ambapo
mtandao unaadhimisha miaka 10 kutoka uanzishwe.
Alisema
wanachama hao wanatakiwa kufika SHIWATA kugaiwa maeneo hayo ambayo
yatalimwa mazao ya muda mfupi (ambayo si ya kudumu) kama vile
pilipili,mahindi, matango, pilipili hoho, mananasi, mbogamboga, matikiti
maji ambayo hustawi kwa wingi maeneo hayo.
Katika hatua nyingine
SHIWATA imeamua kusafisha shamba la ekari 200 ambazo zimekwisha gaiwa
kwa wanachama ambao walijitokeza kulima katika shamba hilo la 500
zinazomilikiwa na mtandao huo kwa ajili ya maandalizi ya kilimo kwanza
msimu huu katika kijiji cha Ngarambe, Mkuranga.
Mwenyekiti Taalib
alisema SHIWATA imeingia mkataba na Kampuni ya Willy Enterprises Ltd ya
Dar es Salaam kukodisha mtambo wa kusafisha shamba (Buldoza) kwa ajili
ya wanachama zaidi ya 100 waliojitokeza kulima.
Alisema SHIWATA
itatumia sh. mil. 22.2 kukodisha buldoza hilo kusafisha shamba la ekari
200 zilizogaiwa kwa wanachama ambapo kila mmoja atalipa gharama ya sh.
111,000 kwa ekari moja.
Jitihada za kusafisha shamba hilo
zinafanywa na SHIWATA ikiwa ni maandalizi ya kufikiwa kwa malengo ya
kuanzishwa mtandao huo utakaoadhimisha miaka 10 ya kuanzishwa mwaka
2004.
Mpaka sasa SHIWATA inao wanachama 8,000 kutoka fani
mbalimbali za uigizaji, muziki wa dansi, muziki wa kizazi kipya, taarab,
soka, netiboli, vijana na waandishi wa habari.

Mwanachama wa siku nyingi wa Shiwata Manase Zabron ambaye ni kocha wa mpira wa kikapu nchiniakienda kuoneshwa shamba lake
Baadhi ya viongozi wa Mtandao wa wasanii Tanzania 'SHIWATA' wakishudia
ugawaji wa mashamba kwa wanachama wake juzi Ngarambe Mkulanga Mkoa wa
Pwani
0 comments:
Post a Comment