PICHA ZA BAADHI YA WAJUMBE WALIOSHIRIKI KATIKA MKUTANO.
Baadhi
ya viongozi wa Wizara ya fedha wakifuatilia kwa makini mkutano uliokuwa
ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa
serikali Dr. Servacius Likwelile, ambapo ujumbe kutoka Tanzania
ulikutana na Mwakili Mkazi wa Benki ya Dunia kwa Tanzania, Rwanda,
Uganda na Burundi Bw. Phippe Dongier hawapo kwenye picha kwa madhumuni
ya kujadili masuala mbalimbali yanayohusu uchumi wa Tanzania. Kutoka
kushoto ni Bw. John Cheyo ambaye ni Kamishna wa Bajeti, anayefuata ni
Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar Bi Amina na wa kushoto kwake
ni Bw. Said Magonya ambaye ni Kamishna wa Fedha za nje Wizara ya
Fedha.(Picha zote na Ingiahedi Mduma – Washington DC).
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius
Likwelile alipokuwa akitoa msimamo wake kuhusu sera zinazopendekewa na
Benki ya Dunia kwa mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia kwa Tanzania,
Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Phippe Dongier.
Dr.
Servacius Likwelile Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa
serikali akiwa pamoja na ujumbe kutoka Tanzania. Kutoka kulia ni Gavana
wa Benki kuu ya Tanzania na kutoka kushoto ni Bi. Natu Mwamba Naibu
Gavana wa Benki kuu ya Tanzania wakimsikiliza kwa makini Bw. Phippe
Dongier ambaye ni mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia kwa Tanzania,
Rwanda, Uganda na Burundi hayupo kwenye picha, alipokuwa akijibu hoja
zilizowekwa mezani.
Bw.
Phippe Dongier ambaye ni mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia kwa
Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi alipokuwa akijibu hoja zilizotolewa
na Dr. Servacius Likwelile Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji
Mkuu wa serikali na kuahidi kuzifanyia kazi.
0 comments:
Post a Comment