
Kocha
Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij keshokutwa (Novemba 5 mwaka huu)
atatangaza kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya mechi ya kalenda ya
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) itakayochezwa ugenini
Novemba 16 mwaka huu.
Nooij
atatangaza kikosi hicho mbele ya waandishi wa habari katika mkutano
utakaofanyika saa 4.30 asubuhi kwenye ofisi za TFF zilizoko ghorofa ya
tatu, Jengo la PPF Tower jijini Dar es Salaam.
Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itacheza na Swaziland,
mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa wa Somhlolo jijini Mbabane.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
0 comments:
Post a Comment