
OfisaMtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Silas Mwakibinga amemaliza mkataba wake tangu Oktoba 31 mwaka huu.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na TPLB wanamshukuru Mwakibinga kwa
mchango wake kwa kipindi ambacho ameitumikia Bodi, na kumtakia kila la
kheri katika majukumu yake mapya huko aendako.
TPLB hivi
sasa iko katika mchakato wa kupata Ofisa Mtendaji Mkuu mpya kwa ajili
ya kuziba nafasi hiyo iliyoachwa wazi na Mwakibinga baada ya muda wa
mkataba wake kumalizika.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
0 comments:
Post a Comment