
Ni siku chache zimepita tangu mwaka wa 2015 uanze, mwanadada mwenye
umbo matata Bongo, Lulu Semagongo ‘Anti Lulu’ amekiri kuuanza vizuri
baada ya kupima ngoma.Akipiga stori na gazeti hili, Anti Lulu alisema
anafurahi kwa kuwa ameuanza mwaka vizuri baada ya kwenda kupima Ukimwi
akiongozana na mama yake na kujikuta yupo salama.
“Yaani nina furaha ya ajabu baada ya kukutwa niko mzima kwani nilikuwa
na wasiwasi sana kutokana na njia nilizopitia kutokuwa salama, mama
yangu ndiye aliyenishauri na kunisindikiza hospitali, nawasihi wasanii
wenzangu nao wakapime ili wagundue afya zao na waweze kuishi bila
wasiwasi,” alisema Anti Lulu.
chanzo:Global Publishers
0 comments:
Post a Comment