Followers

Saturday, 9 May 2015

ALICHOKISEMA DIAMOND JUU YA KUTOOMBA KURA KWA FANS WAKE

 Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz ambaye mara kadhaa amekuwa akiingia kwenye headlines kwa news mbalimbali, time hii ametoa sehemu ya kwanza ya majibu kwa mashabiki wake juu ya maswali juu yake kuwa kwanini haombi kupigiwa kura kama wafanyavyo wasanii wengine walioingizwa kwenye kuwania tuzo za Kilimanjaro msimu huu.


Majibu hayo ya sehemu ya kwanza ameyatoa kupitia akaunti zake mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii leo hii saa 3 na dakika zake usiku, yanasomeka hivi...

"Well Nimekuwa nikipokea maswali na comment nyingi eti kwanini sitangazi vipengele vyangu vya Tunzo watu wanipigie kura...tafadhali naomba mniskilize kwa umakini:
Ikiwa MOE MUSIC hakuonekana ni mmoja ya mwanamuziki bora chipukizi.. 

NDAGUSHIMA ya Ommy Dimpoz haikuonekana inafaa kugombea kama moja ya video bora..YAMOTO BAND licha ya kuvuma na kujaza kila show ya kila pembe ya Tanzania ila mwisho wa siku wameambulia category mbili tu unafkiri mimi nina haja gani ya kuomba kura???? Hivi kuna Nyimbo zimependwa na kuvuma kama NITAJUTA ama NISEME ya YAMOTO BAND Tanzania?? Eti mwisho wa siku, watoto wa watu licha ya Juhudi zote eti hazikustahili wameambulia category mbili tu... Hivi kweli tunakuza muziki wetu au Tunaua??? Mimi Kuwa na Categories 10 na Kuongoza kwa vipengele vingi hakunifanyi eti nifurahie Wengine wanapoumizwa...kwani Kwangu mimi sifanyi mziki ili Nifaidike bali nafanya ili wasanii na Taifa langu pamoja na Tasnia yangu izidi kufika mbali na tuheshimike... I have been to this Industry zaidi ya Miaka Mitano (5 ) so panapo NAMNA Napajuaga mapema na Ndiomaana sitaki kuwapotezesha watu pesa zao wanipigie kura halaf ziende na maji... Wakiona kuna mahala nilistahili watatoa wakiona sijastahili ni haki yangu kutopewa...Nilishawai hata kutopewa tunzo kabisa ila Mpaka leo sijawai shuka na Sitokaa Nishuke labda Waniue!...."

Diamond ndiye msanii anayeshikilia rekodi ya kuchukua tuzo saba za KTMA kwa wakati mmoja, nini maoni yako juu ya taarifa hii?
 

Well Nimekuwa nikipokea maswali na Comment nyingi eti kwanini sitangazi vipengele vyangu vya Tunzo watu wanipigie...
Posted by Diamond Platnumz on Saturday, 9 May 2015

0 comments: